Iyerdoy
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,755
- 1,939
Chanzo cha nyama inayouzwa bei rahisi au bei poa a.k.a kwa mafungu:-Wale kinamama wanaodamka na ndoo zao kwenda vingunguti wanaenda kuuziwa nyama za ngombe ,,,wale walofia njiani ama wale waliokuwa wajawazito,,,vile vitoto hukatwa katwa na kuuzwa ! Wewe hushangai hapa mjini kuna mama ntilie wanauza mpaka supu za jero ? Nyama unawekewa kubwa kubwa mbili,,,, ! Supu ya buku unashiba kabisa ,,! Unadhani hizo nyama ndo wananunua Buchani 10k-12k per kg ? Sio kweli wananunua zile za bei rahisi!
1. Nyama zilizokataliwa i.e. condemned carcasses kutokana na nyama hiyo kuwa tepetevu mno imejaa maji mengi na mautelezi-malenda, imekonda kupitiliza i.e. on Borderline(cadavar). Nyama aina hii huzuiliwa ili walau inyauke.
2. Nyama zinazoamriwa kuchemshwa kwanza kabla ya kuuzwa e.g. nyama inayopatikana na kiasi kidogo cha CB (cystcercus bovis)
3. Sehemu au badhi ya Nyama/viungo zinazopatilizwa kutokana na kitu kinaitwa for aethetic reasons. e.g. utumbo wenye pimply guts nyingi, figo zenye congenital cysts nyingi au hydronephrosis n.k.
4. Nyama zilizochafuliwa (soiled meat)na uchafu au mavi ya mnyama, mchanga/udongo wakati wa uchunaji, ukataji n.k. ikiwemo milopoo
5. Nyama wanazoiba (wanachomoa au wenyewe wanaita Kusokoza) wachunaji
Hizo zote 1-5 ndo za bei poa/maelewano.