Kuku kibudu aliyekufa akachinjwa ana shida gani?

Kuku kibudu aliyekufa akachinjwa ana shida gani?

Eti wakuu kwa mfano kuku kafa na na ndani ya nusu saa akachinjwa ana shido gani kuliwa?mimi sielewi mantiki ya kuku kutoliwa baada ya kufa nachojua ili mfugo aliwe lazima AFE kwanza..
Kama jibu unalo unataka wachangiaji wachangie nn hapo?
 
Eti wakuu kwa mfano kuku kafa na na ndani ya nusu saa akachinjwa ana shido gani kuliwa?mimi sielewi mantiki ya kuku kutoliwa baada ya kufa nachojua ili mfugo aliwe lazima AFE kwanza..
Kama kuna dharura kwa maana hakuna chakula ila huyo mnyama aliyekufa bila ya kuchinjwa unaweza ukakata njaa, hivyo ni kwa imani ya kiislamu. Si vizuri kula nyama ya mnyama aliyekufa, kwani hujui kifo chake kimesababishwa na nini? Huenda alikuwa na maradhi ambayo ukila nyama yake yanaweza kukudhuru wewe mlaji. Ndiyo maana unashauriwa ukitaka kuchinja umchinje mnyama mwenye afya, ambaye hana maradhi ili hata wewe mlaji usidhurike.
 
Nyama ya kuku kwenye mabar na vibanda vingi vya chips ni vibudu. Walinyongwa kabla ya kuchinjwa baadae na wengi ni wa wizi
Kwa mujibu wa Taratibu za Kisheria kuhusu Uandaaji wa Nyama itakayoliwa na Binadamu (Slaughter Practices ) zinadai pamoja na mengine, mnyama aliyekusudiwa huchinjwa (Hukatwa shingo) akiwa hai na damu yake kutiririshwa. Linapokuja suala la Udini ndipo tunapokutana na Halal, Rabbinic, Traditional n.k. vitu ambavyo ni vya Kiimani zaidi.
Kama mnyama hajaelekezwa Kibla na mkataji shingo akawa ni Mwislamu aliyeidhinishwa; huyo mnyama japo kachinjwa na damu kutiririshwa nyama hiyo Ni Kibudu.
Kama aliyekata shingo sio mwislamu; nyama hiyo ni Kibudu
Yapo masharti mengi sana ya Kiimani i.e. Waislamu, Wayahudi, Kimila/Traditional, n.k. LAKINI katika hali ya kawaida iwe iwavyo; nyama ni nyama tuu alimradi iwe ni Fit for Human consumption.
 
Eti wakuu kwa mfano kuku kafa na na ndani ya nusu saa akachinjwa ana shido gani kuliwa?mimi sielewi mantiki ya kuku kutoliwa baada ya kufa nachojua ili mfugo aliwe lazima AFE kwanza..
Kwa nini afe? Amezeeka?
 
Hapa ndipo Uislam unapochukua point 3 ndani moyo wangu Allah ametukataza kula vibudu alishajua kwamba kuna maambukizi mbalimbali ya magonjwa yanayotokana na vibudu kwa kuepuka shaka na nini kimepelekea kifo chake tukaambiwa msile vibudu kush'ney.
 
Wale kinamama wanaodamka na ndoo zao kwenda vingunguti wanaenda kuuziwa nyama za ngombe ,,,wale walofia njiani ama wale waliokuwa wajawazito,,,vile vitoto hukatwa katwa na kuuzwa ! Wewe hushangai hapa mjini kuna mama ntilie wanauza mpaka supu za jero ? Nyama unawekewa kubwa kubwa mbili,,,, ! Supu ya buku unashiba kabisa ,,! Unadhani hizo nyama ndo wananunua Buchani 10k-12k per kg ? Sio kweli wananunua zile za bei rahisi!
 
Wafugaji hatuchinji mnyama alie na afya njema, tunawala wale choka mbaya, katibiwa kwa tiba zote zimegonga mwamba basi huyo anachonjwa tu, hata akifa mwenyew bado anakua hajakwepa kuliwa ataliwa tu.
 
Eti wakuu kwa mfano kuku kafa na na ndani ya nusu saa akachinjwa ana shido gani kuliwa?mimi sielewi mantiki ya kuku kutoliwa baada ya kufa nachojua ili mfugo aliwe lazima AFE kwanza..
Kuchinja hufanywa Ili kuflash damu nje ya mwili kwa kasi,damu ndiyo hubeba vimelea vya magonjwa,kwa waislam mnyama akiwa amejeruhiwa nadhani hafai kuchinjwa, ndiyo maana huko nyuma ukifundushwa kuchinja sharti kwanza uchinje mchinjo mdogo Ili damu itoke kwa nguvu kisha unamalizia, mnyama akijifia mwenyewe hujui kimemuua nini,pengine maradhi ya kuambukiza,ndiyo maana kuna mabwana nyama machinjioni kukagua nyama ikiwa wanyama hawakuwa na maradhi
 
Back
Top Bottom