Uchaguzi 2020 Kukubalika kwa Rais Magufuli/CCM: Kishindo cha asilimia 99.9% ni mawingu tu ya dalili, mvua ni 2020, ni lele tu, ngoma ni 2020!

Uncle Paskali kama kawaida yako, kukuelewa maandiko yako siku hizi inahitaji kusoma kwa hatua,
Asante sana nimekuelewa uzuri,
Kifupi hizi ni rasharasha tu, “kama Faulo zilizochezwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa basi 2020 tutegemee maradufu”
 
Iangalieni nchi kwa macho mawili - makengeza yakizidi tutapoteza uelekeo wa kitaifa

Kila mmoja apiganie kuimarishwa kwa mfumo thabiti wa kidemokrasia
 
Kwa wale ambao sio maarufu huwa wanaambiwa wakachukue buku saba au wanaulizwa mbona wamesahau kuweka namba za simu.

Kwa wewe mkongwe jukwaani utaambiwa mbona cheo chako kipya kinachelewa. Ili mradi tu waukwepe ujumbe wa mada husika.
 
Umeona eeeh yaani sio Pascal tunaemjua,sasa hivi amekua puppet mpaka anachekesha,njaa itamuua!kwakweli kuliko kuwa hivyo ni bora ajifunze kunyamaza!
Mkuu mimi pia ni mdau wa makala zake mayala, hajabadilika sema kabadili namna ya uandishi badala ya kwenda direct anatumia lugha ya kifasihi ambayo inafanya kila msomaji atafsiri alivyoelewa yeye jambo linalomweka yeye salama zaidi mbele ya mamlaka hii dhalimu.
 
Uncle Paskali kama kawaida yako, kukuelewa maandiko yako siku hizi inahitaji kusoma kwa hatua,
Asante sana nimekuelewa uzuri,
Kifupi hizi ni rasharasha tu, “kama Faulo zilizochezwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa basi 2020 tutegemee maradufu”
2007 Kenya yaliyotokea yalisababishwa na walio madarakani kudhani wananchi in wajinga sana.
Nimemshangaa Kabudi anaenda kuwafundisha Kenya kuacha ukabila huku nyumbani kuna uchama.
Ukabila uzuri wake kuwezi kumuua ndugu yako, lakini uchama unaweza kutumwa kumuua mumeo au mkeo itikadi zikihitafiana
 
Huu uzi kwa makamisaa kama sisi ni dongo kubwa sana.
Alafu mayalla umewasilisha unataka kuwaachia watu msala kwa coment zao
 
Wanabodi,

Kuna msemo wa Waswahili usemao, " Mwanzo wa ngoma ni lele" na "Dalili ya Mvua ni Mawingu". Tukubali, tukatae, huu ushindi wa kishindo cha Magufuli, cha asilimia 99.9% kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, ni mawingu tuu ya dalili za mvua, lakini mvua yenyewe ni Uchaguzi Mkuu wa 2020, na kama hizi kelele ni kelele za ngoma, then hii ni lele tuu, ngoma yenyewe ni 2020!.

Leo tena nimepata fursa ya kuendelea na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", ambapo makala ya leo inajikita kwenye swali

Je Wajua Kuwa Hiki Kishindo cha Ushindi wa CCM, Kushinda kwa Asilimia 99.9% Kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni Mwanzo Tuuz?, Kazi Yenyewe Haswa Kukamilika Uchaguzi Mkuu wa 2020?. Jee Huu Sasa ni Uthibitisho wa Rais Magufuli na CCM Kukubalika Sana na Wananchi?. Kufuatia Kukubalika Huku, Kweli Kuna Haja ya Kufanya Uchaguzi 2020?, or Lets Just Save Time, Money and Resources Kwa Kutokufanya Uchaguzi? Rais Magufuli na Watakao Teuliwa na CCM watangazwe tuu moja kwa moja?

Au kwa vile kufanya uchaguzi ni takwa la kikatiba, kisheria, kikanuni na kiutaratibu, 2020 tufanyie tuu Uchanguzi Mkuu hata kama ni igizo tuu la uchaguzi lakini as of now tayari mshindi ni CCM kwa precedence ya matokeo ya uchaguzi huu wa serikali za mitaa?.

Naomba kwanza nianze kwa kukipongeza Chama Cha Mapinduzi, CCM kwa ushindi wa kishindo cha asilimia 99.9% kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, kishindo hiki mimi nakiita ni "Kishindo cha Kasi ya Magufuli" na ni uthibitisho wa
Kukubalika kwa chama cha siasa kwa wananchi na hupimwa kwa idadi ya kura wananchi wanazokipigia chama fulani, na ushindi hutangazwa mwisho wa mashindano, anayetangazwa mshindi, ndie mshindi halali kwa mujibu wa kanuni ya "the end justifies the means", naomba sote tukubaliane CCM ndie mshindi halali regardless uchaguzi ulikuwa huru na wa haki, mshindi ni mshindi, "the winner takes it all, the loser standing small" hongera sana CCM, Hongera Rais Magufuli, Hongera Watanzania kuikubali sana CCM, kumkubali Rais Magufuli.

Uchaguzi huru na wa haki ndicho kipimo pekee cha kupima kukubalika huku, lakini pale ambapo chama kimepata ushindi wa kishindo kwa asilimia 99.9%, ila ni kwa ushindi wa mezani, watu hawakupiga kura baada ya timu pinzani kuweka mpira kwapani, hivyo aliyebaki anatangazwa mshindi halali kwa kupitia bila kupingwa kwenye uchaguzi huru na wa haki, sasa sijui kama kule kutopiga kura kuchagua nako ndiko kukubalika kwenyewe lakini maadam kwa matokeo ya mwisho mshindi ni CCM, then CCM imekubalika.

Inaendelea...
MZEE MEKO: Mayalla maanayake ni NJAA😂😂😂
 
Pascal kudos for smart writing and putting things in great political perspective. You have been well understood by all those who can decipher your coded message.
 
2007 Kenya yaliyotokea yalisababishwa na walio madarakani kudhani wananchi in wajinga sana.
Nimemshangaa Kabudi anaenda kuwafundisha Kenya kuacha ukabila huku nyumbani kuna uchama.
Ukabila uzuri wake kuwezi kumuua ndugu yako, lakini uchama unaweza kutumwa kumuua mumeo au mkeo itikadi zikihitafiana
Mkuu Chakaza umeamua kutia chumvi, ukabila ni mbaya sana nadhani unaifahamu historia ya kweli ya Rwanda mwaka 1994 mwezi wa nne.
Nadhani unaifahamu historia za Sudan Kusini na hata wauliza Nigeria ambao wanayo nchi yenye utaifa dhaifu.
 
Wanabodi,

Kuna msemo wa Waswahili usemao, " Mwanzo wa ngoma ni lele" na "Dalili ya Mvua ni Mawingu". Tukubali, tukatae, huu ushindi wa kishindo cha Magufuli, cha asilimia 99.9% kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, ni mawingu tuu ya dalili za mvua, lakini mvua yenyewe ni Uchaguzi Mkuu wa 2020, na kama hizi kelele ni kelele za ngoma, then hii ni lele tuu, ngoma yenyewe ni 2020!.

Leo tena nimepata fursa ya kuendelea na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", ambapo makala ya leo inajikita kwenye swali

Je Wajua Kuwa Hiki Kishindo cha Ushindi wa CCM, Kushinda kwa Asilimia 99.9% Kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni Mwanzo Tuuz?, Kazi Yenyewe Haswa Kukamilika Uchaguzi Mkuu wa 2020?. Jee Huu Sasa ni Uthibitisho wa Rais Magufuli na CCM Kukubalika Sana na Wananchi?. Kufuatia Kukubalika Huku, Kweli Kuna Haja ya Kufanya Uchaguzi 2020?, or Lets Just Save Time, Money and Resources Kwa Kutokufanya Uchaguzi? Rais Magufuli na Watakao Teuliwa na CCM watangazwe tuu moja kwa moja?

Au kwa vile kufanya uchaguzi ni takwa la kikatiba, kisheria, kikanuni na kiutaratibu, 2020 tufanyie tuu Uchanguzi Mkuu hata kama ni igizo tuu la uchaguzi lakini as of now tayari mshindi ni CCM kwa precedence ya matokeo ya uchaguzi huu wa serikali za mitaa?.

Naomba kwanza nianze kwa kukipongeza Chama Cha Mapinduzi, CCM kwa ushindi wa kishindo cha asilimia 99.9% kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, kishindo hiki mimi nakiita ni "Kishindo cha Kasi ya Magufuli" na ni uthibitisho wa
Kukubalika kwa chama cha siasa kwa wananchi na hupimwa kwa idadi ya kura wananchi wanazokipigia chama fulani, na ushindi hutangazwa mwisho wa mashindano, anayetangazwa mshindi, ndie mshindi halali kwa mujibu wa kanuni ya "the end justifies the means", naomba sote tukubaliane CCM ndie mshindi halali regardless uchaguzi ulikuwa huru na wa haki, mshindi ni mshindi, "the winner takes it all, the loser standing small" hongera sana CCM, Hongera Rais Magufuli, Hongera Watanzania kuikubali sana CCM, kumkubali Rais Magufuli.

Uchaguzi huru na wa haki ndicho kipimo pekee cha kupima kukubalika huku, lakini pale ambapo chama kimepata ushindi wa kishindo kwa asilimia 99.9%, ila ni kwa ushindi wa mezani, watu hawakupiga kura baada ya timu pinzani kuweka mpira kwapani, hivyo aliyebaki anatangazwa mshindi halali kwa kupitia bila kupingwa kwenye uchaguzi huru na wa haki, sasa sijui kama kule kutopiga kura kuchagua nako ndiko kukubalika kwenyewe lakini maadam kwa matokeo ya mwisho mshindi ni CCM, then CCM imekubalika.

Inaendelea...
Imbecile
 
Nakubaliana na wewe kuwa mchezo uliofanyika katika uchaguzi wa Serikali za mitaa 2019 ndio utakaochezwa 2020 kwenye Uchaguzi Mkuu! Sana sana watabadili mbinu ya mchezo ili wasishtukiwe.
Kwa sasa CCM haina imani na Wapiga Kura kabisa!
 
Mkuu Chakaza umeamua kutia chumvi, ukabila ni mbaya sana nadhani unaifahamu historia ya kweli ya Rwanda mwaka 1994 mwezi wa nne.
Nadhani unaifahamu historia za Sudan Kusini na hata wauliza Nigeria ambao wanayo nchi yenye utaifa dhaifu.
Uchama mbaya ninaozungumzia ni kama ule ulitokea Pemba, ccm hawezi pakiwa ndani ya jahazi la m CUF Hata kama anawahishwa hospitali. Pia mCUF hawezi kuongezewa damu na mCCM hata kama ni kuokoa maisha yake.
Sasa hilo hatukua nalo kabisa Tanzania (bara) ila baada ya Magufuli limeanza kushika kasi na yeye ndio kinara wa kulipa nguvu.
 
Kuna kazi kubwa kafanya JPM, kuitoa CCM kutoka kuzomewa mpaka inakuja kuonekana inanyanyapaa vyama vingine.

Matokeo yake anaonekana anavionea vyama vingine, anatekeleza ilani kadri anavyoweza mengineyo ni upungufu wa kibinadamu.
 
Back
Top Bottom