Uchaguzi 2020 Kukubalika kwa Rais Magufuli/CCM: Kishindo cha asilimia 99.9% ni mawingu tu ya dalili, mvua ni 2020, ni lele tu, ngoma ni 2020!

Uncle Paskali kama kawaida yako, kukuelewa maandiko yako siku hizi inahitaji kusoma kwa hatua,
Asante sana nimekuelewa uzuri,
Kifupi hizi ni rasharasha tu, “kama Faulo zilizochezwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa basi 2020 tutegemee maradufu”
 
Iangalieni nchi kwa macho mawili - makengeza yakizidi tutapoteza uelekeo wa kitaifa

Kila mmoja apiganie kuimarishwa kwa mfumo thabiti wa kidemokrasia
 
Kwa wale ambao sio maarufu huwa wanaambiwa wakachukue buku saba au wanaulizwa mbona wamesahau kuweka namba za simu.

Kwa wewe mkongwe jukwaani utaambiwa mbona cheo chako kipya kinachelewa. Ili mradi tu waukwepe ujumbe wa mada husika.
 
Umeona eeeh yaani sio Pascal tunaemjua,sasa hivi amekua puppet mpaka anachekesha,njaa itamuua!kwakweli kuliko kuwa hivyo ni bora ajifunze kunyamaza!
Mkuu mimi pia ni mdau wa makala zake mayala, hajabadilika sema kabadili namna ya uandishi badala ya kwenda direct anatumia lugha ya kifasihi ambayo inafanya kila msomaji atafsiri alivyoelewa yeye jambo linalomweka yeye salama zaidi mbele ya mamlaka hii dhalimu.
 
2007 Kenya yaliyotokea yalisababishwa na walio madarakani kudhani wananchi in wajinga sana.
Nimemshangaa Kabudi anaenda kuwafundisha Kenya kuacha ukabila huku nyumbani kuna uchama.
Ukabila uzuri wake kuwezi kumuua ndugu yako, lakini uchama unaweza kutumwa kumuua mumeo au mkeo itikadi zikihitafiana
 
Huu uzi kwa makamisaa kama sisi ni dongo kubwa sana.
Alafu mayalla umewasilisha unataka kuwaachia watu msala kwa coment zao
 
MZEE MEKO: Mayalla maanayake ni NJAA😂😂😂
 
Pascal kudos for smart writing and putting things in great political perspective. You have been well understood by all those who can decipher your coded message.
 
Mkuu Chakaza umeamua kutia chumvi, ukabila ni mbaya sana nadhani unaifahamu historia ya kweli ya Rwanda mwaka 1994 mwezi wa nne.
Nadhani unaifahamu historia za Sudan Kusini na hata wauliza Nigeria ambao wanayo nchi yenye utaifa dhaifu.
 
Imbecile
 
Nakubaliana na wewe kuwa mchezo uliofanyika katika uchaguzi wa Serikali za mitaa 2019 ndio utakaochezwa 2020 kwenye Uchaguzi Mkuu! Sana sana watabadili mbinu ya mchezo ili wasishtukiwe.
Kwa sasa CCM haina imani na Wapiga Kura kabisa!
 
Mkuu Chakaza umeamua kutia chumvi, ukabila ni mbaya sana nadhani unaifahamu historia ya kweli ya Rwanda mwaka 1994 mwezi wa nne.
Nadhani unaifahamu historia za Sudan Kusini na hata wauliza Nigeria ambao wanayo nchi yenye utaifa dhaifu.
Uchama mbaya ninaozungumzia ni kama ule ulitokea Pemba, ccm hawezi pakiwa ndani ya jahazi la m CUF Hata kama anawahishwa hospitali. Pia mCUF hawezi kuongezewa damu na mCCM hata kama ni kuokoa maisha yake.
Sasa hilo hatukua nalo kabisa Tanzania (bara) ila baada ya Magufuli limeanza kushika kasi na yeye ndio kinara wa kulipa nguvu.
 
Kuna kazi kubwa kafanya JPM, kuitoa CCM kutoka kuzomewa mpaka inakuja kuonekana inanyanyapaa vyama vingine.

Matokeo yake anaonekana anavionea vyama vingine, anatekeleza ilani kadri anavyoweza mengineyo ni upungufu wa kibinadamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…