Uchaguzi 2020 Kukubalika kwa Rais Magufuli/CCM: Kishindo cha asilimia 99.9% ni mawingu tu ya dalili, mvua ni 2020, ni lele tu, ngoma ni 2020!

How sure you are Paskali?Nchi kuubwa sana hii,ina wadau chini ya dunia hadi juu mbinguni.Umewashirikisha wote ukajua mawazo yao juu yake?hasa yule aliye juu mbinguni?from now till 2022 we Tanzanians have a lot to learn from somebody!Utanielewa baadae.
 
Watu wengine bana, hivi huu ulikuwa uchaguzi ama ngoma ya CCM ya mdumange..!! wanapiga wao wanacheza wao...
Watanzania hebu tuwe serious kwa mambo ya maana katika nchi, sasa kama karne hii mnashindwa hata zoezi dogo tu la kuchaguana hivi mnategemea ni lini mtafikia waliko mabeberu?

Karne ya 11 yaani mwaka 1100 ndiyo waliyafanya haya!! sasa hesabu tulivyo mbali kuwakamata.
 
Nimekuelewa mzee, inawezekana umeamua kutumia njia hii ya kumpongeza Raisi na Chama chake. Ingawa naamini ulichokiandika hukukimanisha na ulichokiimsnisha yankini hukikiandika.
 
Wakati watu wakihangaika na kampeni, sisi watu wa predictions za ukweli, tunaendelea na kutoa pongezi za ushindi.
P
 
Hahahaaaa hahahaaaa hahahaaaa hahahaaaa
hahahaaaa hahahaaaa hahahaaaa hahahaaaa
hahahaaaa hahahaaaa hahahaaaa hahahaaaa
 
Paskali Paskali,nimekuita Mara mbili kuonyesha kuwa nakukubali na kuheshimu mawazo yako ingawa sikubaliani na hoja zako kwa asilimia zaidi ya 45.

Umetumia kipimo Kimoja kuwapata ushindi chama cha mapinduzi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu huku ukitumia uchaguzi wa serikali za mitaa kama kipimo kiuu cha kawapa ushindi wa kishindo,ingawa kwangu Mimi kipimo hicho hakitoshi na ni sawa na kipimo chenye matobo kupimia sukari, kipimo ambacho kwacho hatuwezi katu kupata mizania sawia kati ya CCM na vyama vingine ambavyo havikushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa.

Paskali, Kwangu mimi uchaguzi hule sikuelewa CCM ilishindanishwa na chama gani zaidi ya chama chenyewe,p na ushindi wa CCM nimeuchukulia Kama michezo wa masumbwi ambapo bondia mmoja kapanda ulingoni na kujipiga mwenyewe ngumi za tumbo alafu referee amtangaze kwa kujipiga Kwa knockout !!? Litakuwa jambo la kushangaza sana na mimi nauona ushindi wa CCM kwa mtazamo huo ambavyo bondia huyo awezi kuwekwa kwenye kaliba moja na mabondia waliopigana na mabondia wengine!.

Wenye ubongo na milango yote ya fahamu tunafahamu ni kipi kilitokea na sio laisi kusahau. Tunaujua uwezo wa wagombea wa CCM dhidi ya wagombea wa vyama vingine ,Kama sio machinery walizonazo zinazowasaidia kuwezesha huo ushindi sidhani kama ata nusu ya utabiri wako asa kwenye nafasi za ubunge na madiwani Huku uchaguzi ukimya huru na haki bila makandokando ,sijui inaweza kuwa hivyo.
Wacha niishie hapa,muda haujawahi kudanganya tuone na kushuhudi ushindi ulioutari wa kishindo wa %72-92.

Kila la heri CCM kwa kujiandaaa kupata ushindi wa kishindo....
 
" Watu wanakuwa makini sana wanapochagua mbuzi wa Pasaka,Eid,xmas kuliko wanapopaswa kuamua na kuchagua mambo ya msingi "

" Wakati wa uchaguzi watu huwa wanaziweka akili zao stoo,baada ya uchaguzi kupita wanazirudia akili Zao stoo"


[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Wakati watu wakihangaika na kampeni, sisi watu wa predictions za ukweli, tunaendelea na kutoa pongezi za ushindi.
P
Hawa ndo sampuli ya watu waliosomeshwa kwa kodi zetu ili wasaidie nchi kwa kupaza sauti zao/zetu pale ambapo taratibu tulizojiwekea kama nchi zinakeukwa!!!
Ni masikitiko makubwa sana, hongera kwa kutoa pongezi ndugu Pasco.
 
Punguani mwingine huyu! Sijui kama hata anajua 99.9% inamaanisha nini! Huyu naye ni msomi wa sheria kutoka Jalalani University Ooops! UDSM!!!!
 
Leo ndio siku ya hii ngoma, naisubiria kwa hamu matokeo kama nitapatia, ili nijue kama viatu vya Sheikh Yahya vinanifiti...
P
 
Na hiki ndicho kinawafanya maccm wanababaika na kupagawa uchaguzi wa leo maana hawana uhakika na matokeo pamoja na mbinu zote za "kisayansi" kama wanavyojinadi
 
Ukabila unawasumbua wasukuma wengi sana tangu awamu hii ya 5 ianze. Wanasifu hata pale panapostahili kukosolewa.
 
Wataalamu wa hesabu wanasema numbers don't lie, mimi sjisifu ila kiukweli mimi ni mzuri sana kwenye hesabu za estimates na probability
Angalia matokeo
Dkt. Magufuli ameshinda kwa kupata kura 12,516,252 (sawa na 84.4% ya kura halali)

Tume imesema walikuwa na jumla ya watu 29,754,699 waliojiandikisha kupiga kura, na waliopiga kura walikuwa 15,091,950. Kura halali zilikuwa 14,830,195
View attachment 1616177
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…