Uchaguzi 2020 Kukubalika kwa Rais Magufuli/CCM: Kishindo cha asilimia 99.9% ni mawingu tu ya dalili, mvua ni 2020, ni lele tu, ngoma ni 2020!

Uchaguzi 2020 Kukubalika kwa Rais Magufuli/CCM: Kishindo cha asilimia 99.9% ni mawingu tu ya dalili, mvua ni 2020, ni lele tu, ngoma ni 2020!

How sure you are Paskali?Nchi kuubwa sana hii,ina wadau chini ya dunia hadi juu mbinguni.Umewashirikisha wote ukajua mawazo yao juu yake?hasa yule aliye juu mbinguni?from now till 2022 we Tanzanians have a lot to learn from somebody!Utanielewa baadae.
 
Watu wengine bana, hivi huu ulikuwa uchaguzi ama ngoma ya CCM ya mdumange..!! wanapiga wao wanacheza wao...
Watanzania hebu tuwe serious kwa mambo ya maana katika nchi, sasa kama karne hii mnashindwa hata zoezi dogo tu la kuchaguana hivi mnategemea ni lini mtafikia waliko mabeberu?

Karne ya 11 yaani mwaka 1100 ndiyo waliyafanya haya!! sasa hesabu tulivyo mbali kuwakamata.
 
Nimekuelewa mzee, inawezekana umeamua kutumia njia hii ya kumpongeza Raisi na Chama chake. Ingawa naamini ulichokiandika hukukimanisha na ulichokiimsnisha yankini hukikiandika.
 
Wanabodi,
Hongera sana CCM in advance kwa ushindi wa kishindo katika Uchaguzi Mkuu ujao wa rais, wabunge na madiwani hapo mwakani 2020.
CCM imekubalika sana,
Magufuli amekubalika sana,
Hongera sana Watanzania kuikubali CCM,
Kumkubali JPM
Viva African Democracy
Viva Tanzanian Democracy

Paskali
Wakati watu wakihangaika na kampeni, sisi watu wa predictions za ukweli, tunaendelea na kutoa pongezi za ushindi.
P
 
Hahahaaaa hahahaaaa hahahaaaa hahahaaaa
hahahaaaa hahahaaaa hahahaaaa hahahaaaa
hahahaaaa hahahaaaa hahahaaaa hahahaaaa
 
Paskali Paskali,nimekuita Mara mbili kuonyesha kuwa nakukubali na kuheshimu mawazo yako ingawa sikubaliani na hoja zako kwa asilimia zaidi ya 45.

Umetumia kipimo Kimoja kuwapata ushindi chama cha mapinduzi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu huku ukitumia uchaguzi wa serikali za mitaa kama kipimo kiuu cha kawapa ushindi wa kishindo,ingawa kwangu Mimi kipimo hicho hakitoshi na ni sawa na kipimo chenye matobo kupimia sukari, kipimo ambacho kwacho hatuwezi katu kupata mizania sawia kati ya CCM na vyama vingine ambavyo havikushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa.

Paskali, Kwangu mimi uchaguzi hule sikuelewa CCM ilishindanishwa na chama gani zaidi ya chama chenyewe,p na ushindi wa CCM nimeuchukulia Kama michezo wa masumbwi ambapo bondia mmoja kapanda ulingoni na kujipiga mwenyewe ngumi za tumbo alafu referee amtangaze kwa kujipiga Kwa knockout !!? Litakuwa jambo la kushangaza sana na mimi nauona ushindi wa CCM kwa mtazamo huo ambavyo bondia huyo awezi kuwekwa kwenye kaliba moja na mabondia waliopigana na mabondia wengine!.

Wenye ubongo na milango yote ya fahamu tunafahamu ni kipi kilitokea na sio laisi kusahau. Tunaujua uwezo wa wagombea wa CCM dhidi ya wagombea wa vyama vingine ,Kama sio machinery walizonazo zinazowasaidia kuwezesha huo ushindi sidhani kama ata nusu ya utabiri wako asa kwenye nafasi za ubunge na madiwani Huku uchaguzi ukimya huru na haki bila makandokando ,sijui inaweza kuwa hivyo.
Wacha niishie hapa,muda haujawahi kudanganya tuone na kushuhudi ushindi ulioutari wa kishindo wa %72-92.

Kila la heri CCM kwa kujiandaaa kupata ushindi wa kishindo....
 
" Watu wanakuwa makini sana wanapochagua mbuzi wa Pasaka,Eid,xmas kuliko wanapopaswa kuamua na kuchagua mambo ya msingi "

" Wakati wa uchaguzi watu huwa wanaziweka akili zao stoo,baada ya uchaguzi kupita wanazirudia akili Zao stoo"


[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Wakati watu wakihangaika na kampeni, sisi watu wa predictions za ukweli, tunaendelea na kutoa pongezi za ushindi.
P
Hawa ndo sampuli ya watu waliosomeshwa kwa kodi zetu ili wasaidie nchi kwa kupaza sauti zao/zetu pale ambapo taratibu tulizojiwekea kama nchi zinakeukwa!!!
Ni masikitiko makubwa sana, hongera kwa kutoa pongezi ndugu Pasco.
 
Punguani mwingine huyu! Sijui kama hata anajua 99.9% inamaanisha nini! Huyu naye ni msomi wa sheria kutoka Jalalani University Ooops! UDSM!!!!
 
Leo ndio siku ya hii ngoma, naisubiria kwa hamu matokeo kama nitapatia, ili nijue kama viatu vya Sheikh Yahya vinanifiti...
P
 
Hiki kinachoitwa 'ushindi wa kishindo' ni punyeto ya kisiasa tu. Hakika ccm kwa kuvuruga uchaguzi huu wamekosa kupata kipimo halisi na sahihi cha kujua kiwango cha kukubalika kwake kwa wananchi. Kushangilia ushindi haramu huu ni sawa na kujilisha upepo.
Na hiki ndicho kinawafanya maccm wanababaika na kupagawa uchaguzi wa leo maana hawana uhakika na matokeo pamoja na mbinu zote za "kisayansi" kama wanavyojinadi
 
Wanabodi,

Kuna msemo wa Waswahili usemao, " Mwanzo wa ngoma ni lele" na "Dalili ya Mvua ni Mawingu". Tukubali, tukatae, huu ushindi wa kishindo cha Magufuli, cha asilimia 99.9% kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, ni mawingu tuu ya dalili za mvua, lakini mvua yenyewe ni Uchaguzi Mkuu wa 2020, na kama hizi kelele ni kelele za ngoma, then hii ni lele tuu, ngoma yenyewe ni 2020!.

Leo tena nimepata fursa ya kuendelea na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", ambapo makala ya leo inajikita kwenye swali

Je Wajua Kuwa Hiki Kishindo cha Ushindi wa CCM, Kushinda kwa Asilimia 99.9% Kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni Mwanzo Tuu?, Kazi Yenyewe Haswa Kukamilika Uchaguzi Mkuu wa 2020!. Jee Huu Sasa ni Uthibitisho wa Rais Magufuli na CCM Kukubalika Sana na Wananchi?. Kufuatia Kukubalika Huku, Kweli Kuna Haja ya Kufanya Uchaguzi 2020?, or Lets Just Save Time, Money and Resources Kwa Kutokufanya Uchaguzi?, na badala yake mgombea urais wa CCM, Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli atangazwe tuu, na Wagombea Watakao Teuliwa na chama dola CCM watangazwe tuu moja kwa moja kuwa wamepita bila kupingwa?.

Au kwa vile kufanya uchaguzi ni takwa la kikatiba, kisheria, kikanuni na kiutaratibu, 2020 tufanyie tuu Uchanguzi Mkuu hata kama ni igizo tuu la uchaguzi lakini as of now tayari mshindi ni CCM kwa precedence ya matokeo ya uchaguzi huu wa serikali za mitaa?.

Naomba kwanza nianze kwa kukipongeza Chama Cha Mapinduzi, CCM kwa ushindi wa mezani wa kishindo cha asilimia 99.9% kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, kishindo hiki mimi nakiita ni "Kishindo cha Kasi ya Magufuli" na ni uthibitisho wa kukubalika kwa chama cha siasa kwa wananchi kwa mujibu wa African Democracy na Tanzanian Democracy ambapo uchaguzi wa vyama vingi vya siasa unafanyika, halafu chama kimoja kinapata ushindi wa kishindo cha asilimia 99.9%, kisha mshindi anasherehea ushindi huo na uchaguzi huo kuhesabika ulikuwa ni uchaguzi huru na wa haki!.

Kipimo halisi cha uchaguzi wa demokrasia ya kweli na demokrasia ya haki, ushindi wa haki wa uchaguzi huru na wa haki, hupimwa kwa idadi ya kura wananchi wanazokipigia chama fulani, votes casted, na mshindi halali kupatikana kwa aliyepigiwa kura nyingi. Lakini sio ushindi huu wa mezani.

Lakini kwa vile kanuni zetu za uchaguzi zinaruhusu ushindi wa mezani, no vote casted due to no show, na ushindi hutangazwa mwisho wa mashindano, anayetangazwa mshindi, ndie mshindi halali kwa mujibu wa kanuni ya "the end justifies the means", naomba sote tukubaliane CCM ndie mshindi halali regardless uchaguzi ulikuwa huru na wa haki, mshindi ni mshindi, "the winner takes it all, the loser standing small" hongera sana CCM, Hongera Rais Magufuli, Hongera Watanzania kuikubali sana CCM, kumkubali Rais Magufuli.

Uchaguzi huru na wa haki ndicho kipimo pekee cha kupima kukubalika huku, lakini pale ambapo chama kimepata ushindi wa kishindo kwa asilimia 99.9%, ila ni kwa ushindi wa mezani, watu hawakupiga kura baada ya timu pinzani kuweka mpira kwapani kufuatia kufanyiwa figisu, hivyo aliyebaki anatangazwa mshindi halali kwa kupitia bila kupingwa kwenye uchaguzi huru na wa haki, sasa sijui kama kule kutopiga kura kuchagua nako ndiko kukubalika kwenyewe lakini maadam kwa matokeo ya mwisho mshindi ni CCM, then CCM imekubalika.

Sasa kama hili limefanyika kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na limepita na limekubalika kwa uchaguzi wa vyama vingi, chama kimoja kikashinda ushindi wa kishindo cha asilimia 99.9% na uchaguzi huo ukahesabika ni uchaguzi huru na wa haki na mshindi ni mshindi halali, hii ni African Democracy na Tanzanian Democracy it's only in Africa and only in Tanzania.

Sasa naombeni mimi mwezenu niwe wa kwanza kuwatangazia rasmi kuwa matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa yalikuwa ni dalili tuu ya mvua, mvua yenyewe halisi ni kwenye Uchanguzi Mkuu wa mwaka 2020, kama ushindi hui ni lele, ngoma ni uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Matokeo ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, ni CCM tena kwa ushindi wa kishindo ila kishindo cha uchaguzi Mkuu hakitakuwa cha ushindi wa asilimia 99.9% kama uchaguzi wa serikali za mitaa, kwasababu Uchanguzi Mkuu unahusisha Zanzibar, hivyo party ya ushindi wa CCM, itatibuliwa na yale majimbo mawili ya Zanzibar, ns majimbo ya kisiwa cha Pemba, hivyo kishindo kinaweza kuwa kwenye around 87-92%, ila ni ushindi wa kishindo.

Hongera sana CCM in advance kwa ushindi wa kishindo katika Uchaguzi Mkuu ujao wa rais, wabunge na madiwani hapo mwakani 2020.
CCM imekubalika sana,
Magufuli amekubalika sana,
Hongera sana Watanzania kuikubali CCM,
Kumkubali JPM
Viva African Democracy
Viva Tanzanian Democracy

Paskali
Ukabila unawasumbua wasukuma wengi sana tangu awamu hii ya 5 ianze. Wanasifu hata pale panapostahili kukosolewa.
 
Wanabodi,

Matokeo ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, ni CCM tena kwa ushindi wa kishindo ila kishindo cha uchaguzi Mkuu hakitakuwa cha ushindi wa asilimia 99.9% kama uchaguzi wa serikali za mitaa, kwasababu Uchanguzi Mkuu unahusisha Zanzibar, hivyo party ya ushindi wa CCM, itatibuliwa na yale majimbo mawili ya Zanzibar, ns majimbo ya kisiwa cha Pemba, hivyo kishindo kinaweza kuwa kwenye kati ya around 80%-90%, ila ni ushindi wa kishindo.

Paskali
Wataalamu wa hesabu wanasema numbers don't lie, mimi sjisifu ila kiukweli mimi ni mzuri sana kwenye hesabu za estimates na probability
Angalia matokeo
Dkt. Magufuli ameshinda kwa kupata kura 12,516,252 (sawa na 84.4% ya kura halali)

Tume imesema walikuwa na jumla ya watu 29,754,699 waliojiandikisha kupiga kura, na waliopiga kura walikuwa 15,091,950. Kura halali zilikuwa 14,830,195
View attachment 1616177
P
 
Back
Top Bottom