Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Madada ndiyo walengwa wa uzi huu lakini makaka msiache kusoma na pia kutoa mawazo yenu. Mama wakwe ni wanawake na wao pia walikua vijana wakati fulani hivyo kukutana na mama kusikufanye uwe roho juu juu.
Mpaka mwenza anaamua kukufahamisha kwa mama yake, inamaana kuna vitu ameviona kwako na hataki kukupoeza. Wadada mfahamu hawa vijana tuliwabeba tumboni, kuwanyonyesha na kuwapikia. Hawa vijana wana nafasi ya pekee katika mioyo yetu na wanapopata wachumba viherehere na mashangumbe ya mjini tunaumia sana.
Mdada kwa mama mkwe kuwa katika uhalisia wako. Inawezekana umealikwa kwa chakula, kula kwa ustaarabu na baada ya kula unaweza kuomba uonyeshwe jiko liko wapi uondoe sahani mezani. Siku ya kwanza kuwa msikilizaji na umsome mama mzaa chema. Usiwe msemaji mpaka maduka yote ya vipodozi unavijua wewe.
Mnapo fake tunawajua kwakua hata sisi tulishapata muda wa kukaa na mama wakwe zetu kwa mara ya kwanza.