Sehemu ya 2.
MAWASILIANO YAZIDI KUSHAMILI
Kiukweli nilijikuta nazoeana sana na Waridi, kila mmoja alijua ratiba za mwenzake na ilikuwa kila siku lazima tuzungumza usiku hadi usiku wa manane...ama alfajiri kabisa. sana sana tulikuwa tunapiga story za mapenzi, tu usiku kucha. tuliwasiliana kwa muda wa miezi mitatu hivi na ushee. kipindi hicho sikuwa na kazi ila nilikuwa mwanafunzi kwenye chuo kimoja hivi. waridi yeye alikuwa anafanya kazi huko Geita kwenye moja ya migodi mikubwa.
siku moja nikamtania kuwa natamani sana kumuona. ni kama Waridi alikuwa anangoja nimuanze. akaniambia kuwa nikiwa teyari nimwambie. doh.
wiki hiyo ilikuwa wiki ya mitihani pale chuoni hivyo wiki ijayo siku na ratiba iliyobana. kwenye mazungumzo yangu na Waridi nikagusia kuwa wiki ijayo nipo huru sina ratiba yoyote. Waridi alifurahi sana. akaniambia kuwa nijiandae. atanitumia nauli ikiwezekana niende Geita, kiukweli mimi ni mtu ninaye penda sana safari lakini nilikuwa na mashaka sana na safari ile ukizingatia jinsi nilivyo fahamiana na Waridi nikawa napatwa na ukakasi sana. lakini sikuwa na jinsi, siku ilivyo wadia Waridi alinitumia pesa nyingi kama nauli. siku amini kwani sikuwahi kumiliki pesa nyingi kiasi kile, kwa muda huo pesa nyingi kama hizo nilizishika nilipo kuwa nalipa ada...lakini siku ile nilikuwa na kitita cha pesa, sikuwa na pochi {hii ni hadi leo wala sikumbuki kama niliwahi kumiliki pochi haaahaaahaa}
SAFARI YA GEITA INAANZA
usiku wa safai huwa mfupi sana na ndicho kilicho nitokea mimi siku ile kwani, nilipitiwa na usingizi mzito sana nimekuja kushituka ilikuwa saa 10 na dakika 45 alfajiri na kwa mujibu wa Waridi gari nzuri ya kwanza ilikuwa inaondoka saa 11 kamili za alfajiri. hivyo ilikuwa imesalia robo saa tu gari ya kwanza ianze safari, lakini kwa upande wangu ndio kwanza nilikuwa nashituka kutoka kitandani, nikaenda kuoga. hadi namaliza ilishatimia saa 11 alfajiri. doh Waridi alinipigia simu kujua nilipo alikasirika kwani alijua kuwa kwa muda huo nilitakiwa niwe stendi ndani ya basi. lakini alihisi tu nilikuwa nyumbani na alijua pengine nimemuingiza mjini kuwa amenitumia nauli na sikuwa na nia ya kwenda. ila kiukweli bado nilikuwa najadiliana na serikali yangu ya ubongo juu ya safari ile. kuna upande ulikuwa unaniambia niende na kuna sauti nyingine ilikuwa inaniambia nisiende. kukawa kuna kelele tu kwenye ubongo wangu....
hatimae niliamua niende {uamuzi mgumu huu na nilijiona shujaa sana} kwa kuwa pesa nilikuwa nayo ya kutosha nilichukua piki piki kutoka Tabata hadi stendi ya mabasi ya mikoani {Ubungo} nilivyofika kwa msaada wa wapiga debe nilipata gari ya mwisho ambayo ilikuwa inaondoka saa 11 na dakika 30 alfajiri. basi liliitwa LUSHANGA {kwa wakazi wa huko mtakuwa mnalijua nina imani hadi leo kampuni hii bado ipo}.
safari ilikuwa nzuri, tuliiacha Ubungo, tukapita Kimara, Kibaha, tukaingia Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, tukaingia Kahama...tukapinda njia iendayo Geita ki ukweli lile basi lilikuwa baya sijapata kuona na lilikuwa linavuja. yani ilikuwa shida tupu. njia nzima nilikuwa nawasiliana na Waridi akitaka kujua nilipofika...
ilipofika saa 7 na dakika 45 za usiku tulifika kwenye kijiji/mji maarufu unaoitwa Katoro.
mimi nilikaa siti ya mwisho kabisa dirishani, mbele yangu siti ya upande wa kushoto walikaa mwanaume na mwanamke. vitendo walivyokuwa wanavifanya vilikuwa vinahamasisha sana na hiki kili nifanya nijue kuwa safarini watu hulana matunda kimasihala sana. hali ilionyesha kuwa wawili wale walikuwa awafahamiani ata kidogo. lakini kwa kigezo cha kukaa siti moja. wakawa wamefahamiana. giza lilipo ingia.
walijifunika shuka moja. na kibaridi kile dah. tulipofika pale Katoro dereva aligoma kabisa kuendelea na safari. jicho langu lilikuwa kwa wale wapenzi wapya ambao walikuwa wameanza kushikana shikana mule mule ndani ya gari. yule mwanamke alikuwa mnene aliye jaaliwa shepu na mbinuko ulionona...yani alikuwa na tako la haja. ghafra nikawasikia wakisema kuwa, atuwezi kulala humu hivyo walikubaliana kuwa wanaenda kulala kwenye nyumba ya wageni ambayo ipo karibu na gari lilipo pakiwa. hadi muda ule nilikuwa bado sijaamua kuwa nilale kwenye gari mule mule ama na mimi niende kwenye nyumba za wageni. kwakua ilikuwa inaelekea saa 8 na ushee za usiku niliamua nilale mule mule kwenye gari kwani siti ya mwisho watu wote nilio kaa nao walishuka nadhani wote walienda kulala kwenye nyumba za wageni.
HATIMAYE KUNA PAMBAZUKA.
waliosema giza totoro ndio ishara ya mapambazuko awakukosea hata kidogo, giza lilikuwa kali lakini lilisindikizwa kwa milio ya ndege fulani ivi ambao wakilia hao tu wazee wakale walikuwa wanajua muda si mrefu kunapambazuka. Geita kuna baridi sana hasa msimu ule. nadhani ulikuwa msimu wa baridi. nilikuwa natetemeka sana ukizingatia sikuwa na jaketi. abiria walirudi kwa minajili ya kuendelea nasafari kweli safari ilianza. chaajabu na nilicho kilaani sana ni ufupi wa safari. kutoka pale katoro hadi Geita kumbe hapakuwa mbali kabisa. ni mwendo wa dakika kadhaa tu pengine ata robo saa nijingi sana.
simu niliyokuwa natumia, ilizimika charge na ndio ilikuwa kiunganishi kikubwa sana, kwa mwenyeji wangu. nambaya zaidi sikuwa na namba za Waridi kichwani, niliuvunja ukimya nikaamua kumwambia shida yangu abiria mwenzangu nilie kaa nae siti moja
nikaongea "n
dugu yangu naomba tukifika geita uniazime simu yako,simu yangu imezimika charge " yule abiri alikubali na safari iliendelea.
tullifika Geita,tukashuka garini,lakini bahati haikuwa yangu kwani yule abiria alishuka bila kuniazima simu na mbaya zaidi alijifanya kama hanifahamu niliuzunika japo si sana, lakini kimoyo moyo nikajisemea pengine huyu alizani kuwa nitakuwa mwizi. dah. lakini kwa mbali niliona kitu kidogo cha polisi kilichopo pale stendi ya mabasi ya geita {huwa nikikutana na vituo vya polisi najiona nina amani sana na nina kuwa huru sana sijui kwanini ila tokea nilipokuwa mdogo sikuwa nawaogopa Polisi na nilikuwa nawapenda sana maaskari haswa wakiwa na vyeo nyota}
nilienda pale kituo cha polisi, nikajieleza kuwa mimi ni mgeni hivyo naomba msaada wa kupatiwa charge ili niwasiliane na mwenyeji wangu aje kunipokea. askari mmoja wa kike baada ya kujilizisha kuwa kwenye mazungumzo yangu siku na ata chembe ya udanganyifu alinipa betrii yake ya simu nikaiweka kwenye simu yangu. nilipo washa tu simu. Waridi nae alipiga.
USO KWA USO NA WARIDI
Waridi aliniambia kuwa hakulala usiku kucha kwani sikuwa napatikana kwenye simu yangu, hivyo alijawa sana na wasi wasi. nilimuondoa hofu kisha akaniambia niende nikapande daladala nikisha pata daladala nimpe dereva simu amuelekeze anapotakiwa kunipeleka. yule askari wakike alijikuta ananiamini. hivyo aliniachia betrii yake ya simu niondoke nayo kisha alibaki na yakwangu tukaahidiana kuwa nihakikishe baadaye nampelekea betrii yake.. nilitoka nje ya ile stendi nikifuata barabara ilipo. nilikaa stendi bila mafanikio ya kuona dala dala yoyote ikisimama pale nilipo simama. ilipita nusu saa nikaamua kumpigia simu Waridi "nikamwambia daladala zenyewe huku za shida sana yani hakuna ata dala dala moja ilio nipita" Waridi alicheka sana kisha akaniambia "inamaana kweli huzioni daladala....?"nikamwambia "hakuna daladala kabisa" Waridi akaniambia "je hakuna baiskeli zenye viti nyuma hapo ulipo" nilipo geuka kushoto na kulia niliona baiskeli za aina hiyo nyingi tu...! Waridi akaniambia hizo ndizo Daladala zenyewe.mfuate dereva wa baiskeli kisha unipigie nimpe malekezo......itaendeleaaaaaa