Kula mgahawani na kupika mwenyewe kipi kinamaliza pesa kwa upande wako?

Mimi tangu niko kwa mama mpaka nimeenda kwangu sina desturi ya kununua kitafunwa asubh na nikinunua ujue nina ham nacho na sana mihogo au vitumbua vinginevyo hua napika jioni vya asubuh au kama ni weekend naamka mapema napika tu asubuhi bajeti za jero jero zinapungua
Mkuu siku zikinikaa napiga supu ya ngombe na tule tumafuta yake ya juu A.K.A LAYER ambayo inag'aa sana mpaka naifanya kioo pale kwa sababu najiona.
Ila siku zingine napata muhogo wa 500 na dagaa 500 na vhai ya 100 mchezo umeisha...
 
Kama hujanunua mkaa gunia ukanunue ule wa kupima hapo kama ges unayo kidogo nafuu sema ukiwa mwenyewe kama unaona sometimes utajitaji kujipikia unanunua vyakula unaweka ndani unavihifadhi vizur sku ukitaman msos wa mkono wako unajipikia
Hiyo nayo inakera sana yani.

Nakumbuka nilikuwa nanunua maziwa chupa ya drop kwa alfu mbili.alafu hapo hapo nakunywa siku nne ila napata gharama ya kuyaweka kwenye friji na friji yangu inakulaga umeme.

Nikaona upumbavu huu natumia unit nyingi kwa siku kwa ajili ya kuhifadhi maziwa ya buku?
Nikaachilia mbali nikawa nachukua nusu nusu kila siku na friji nikawa nawasha wife akiwepo natia mazagazaga kibao.

Mahesabu bwana
 
Ni kweli kama niko home siendi kibaruani naandaa msosi wangu wa nguvu natia kila kiungo ili nione tofauti ya kula mgahawani na kupika mwenyewe.

Siku moja nimepika mboga nikatia mbwembwe kitunguu saumu kizima nikatia kwenye mboga.
Bwana bwana bwana daaaah
 
Mahesabu muhimu
 
Iko hivi, chakula cha mtu 1 kupika ni gharama sana. 1,500 au mbili ushakula na kushiba. Ila kama getto mko zaidi ya mtu 1 ni heri kupika. Kwa sababu elfu 3 au 4 zitakazotumika hapo ni nyingi kama mngeamua kupika ingeweza kutosha 2,500 au hata elfu 2.

Sent using my Nokia Torch
 
Ahahahaahha ilikua mboga gani??? Uliila au ulimwaga
 
Ni kweli kabisa. Kwa kifupi hakuna formula kuwa kupika (X) au kula mgahawani (Y), basi tendo X ni ghali zaidi ya Y. Kuna factors nyingi za kuzingatia. Vitu kama location, unapika/kununua chakula gani na mko watu wangapi vinaweza kubadili kabisa cost. Hata amount ya chakula unachopika vile vile.
 
Sasa mi mwanaume nikande ngano?
Afu madam S ujue na mimi nipo single.

Sent using my Nokia Torch
 
Ahahahaahha ilikua mboga gani??? Uliila au ulimwaga
Mkuu ilikuwa ni mchuzi wa samaki.
Siku hiyo nilisema nataka kufanya maajabu.

Mchuzi nilikuwa ulikuwa mzuri ila sasa uki mbaja harufu yake inakuwa ya shida sana,yani una mbaja alafu unajiuliza hakuna mwingine ananisaidia humu au ndo mimi tu?

Alafu nilichanganya na tangawizi ukubwa wa dole gumba.
 
Honestly ni kubwa kwangu mm kama nipo peke yangu na kama tuko zaidi ya mmoja heri ninunue tambi nusu na robo na sukari robo nipike tule kuliko kuitumia hivo na kama nina ham hasa ya kununua kitafunwa me napenda mihogo sambusa sjui katles za jero nimeshashiba bila hiyana
Acha utani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…