Kula mihogo mibichi kunasababisha uwe zezeta

Mihogo ni kweli ina sumu, na madhara yake hayaonekani hapo hapo, ni progressive yanawez chukua hata miaka kuonekana! Kukubwa usile miogo MIBICHI... Iliyopikwa iko safe
Na unga wake je?
 
Daah sijui mkuu... Ugonjwa wa akili
Ila mkuu usikubaliane kila kinacholetwa hapa, na watu wenye tabia kila wanachosikia, huja kuandika hapa.

Kwa mfano hii habari, alitakiwa aeleze chanzo cha habari yake, utafiti umefanyika wapi na wapi.

Tunapigana kwa ajili yetu na Taifa, tuache kueneza mambo yanayotuangamiza sisi na taifa kijumla, kuna watu wanaishi wakitegemea kuuza mihogo.
 
Watafiti wetu wa mabwana shamba cjui wanafanya nini, ilitakiwa wao ndo watoe elimu kuhusu ardhi gani inafaa kulima mihogo ila wanakaa ofisinj tu.

Umenena kweli kilimanjaro ardhi haifai kwa mihogo sababu mm ni muhanga wa kifo, mama yangu alienda kununua mihogo soko la mwika jioni.

Basi asubuhi alikaanga tukala vizuri na chai ila ilikuwa michungu mimi, mama na wajuku zake wawili yaani watoto wangu nikaelekea job.

Kufika jioni nikapigiwa simu watoto wanaumwa wanatoa mapovu mdomoni ilibidi awatafutie (mapolo) kinyesi cha ng'ombe chenye mchanganyiko wa mkojo hii inasaidia kama dawa pindi unapohisi mtu amemeza sumu, aliwanywesha lakini hali ikawa mbaya zaidi ilibidi wakimbizwe hospitali ya marangu kitemboni fasta wakatundikiwa dripu na madawa hiyo ndo ilikuwa pona yao.

Uzuri wa moshi kumejaa hospitali nyingi jirani kila kona ingekuwa mikoa mingine huko vijijini ungekuta nilishawapoteza wote kwa mpigo, japo bili ilikuwa kubwa ni zaidi ya 300,000/=.

Hiyo ndo shida ya hosptali za taasisi yaani usiku mmoja bili ni zaidi ya hiyo laki tatu, wanajipangia bei wanavyotaka na ukiwa na bima ukiwaonyesha hawakuhudumii utakufa unajiona.

Naomba serikali mlitazame hilo.
 
Mihogo ipo yenye sumu tena sumu hasa, kwa mikoa inayolima mihogo wanaijua, aina hii ya mihogo, huliwa ikiwa makopa, haifai kuliwa ikiwa imepikwa wala kuchomwa, huliwa ikiwa makopa tu.

Mbegu za mihogo zina majina yake, na majina yanatofaitiana kulinga mkoa, mbegu zinazofanana majina ni hizi, zinazosambazwa na watafiti.
 
Nilichogundua Wanawake wanaangaika na vikolombwezo kibao vya kujiongezea mvuto wapendwe na wanaume.

Na wanaume nao wako Bize kutafuta stamina kitandani Ili kwenda kushinda nao wanawake kwenye mizagamuo. Which is Bullshit
 
Jambo hili limenisikitisha sana. Hili suala hata kuna baadhi ya maeneo morogoro walipiga dawa DDT hapo zamani.

Zile sumu mpaka Leo hii bado ziko ardhini kuna watu wanazaliwa na ulemavu na matatizo makubwa ya kiafya. Mtoto anazaliwa leo unakuta ana kisukari. Mpaka unajiuliza inakuwaje kumbe tunakula sumu mbaya sana.

Kweli kuna haja ya serikali kutazama hili kwa jicho la tatu.
 
Mi nimekua kahama uko.. mihogo nimekula sana na sijawa zezeta... Mihogo mkomboz wa jamii nying sana... Hii tafiti ya pdf
Nilivyoelewa, kula mihogo mibichi kuna madhara, ila ikipikwa ile sumu inaondoka. Itakuwa hata ikikauka sumu inaondoka.

Naunga mkono hoja. Ukila mihogo mibichi mingi tumbo linaanza kuuma, lakini ukila maparachichi mengi tumbo haliumi ila unavimbewa tu! Tafsiri yake, kwenye mihogo mibichi kuna sumu, ila ikikauka sumu inapungua!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Labda Ni kweli mihogo huleta uzezeta.
Kilimanjaro hakuna mihogo.
Lushoto hakuna mihogo.
Mbeya hakuna mihogo.

Sasa tuje sehemu zenye mihogo ya kumwaga. Mtwara, Tabora, Handeni, Kigoma, Pwani, Lindi.Geita, Mara.
Do you get the point? Sio lazima kila kitu kisemwe.
 
Parachichi, haliwezi kuwa sawa na mihogo, parachichi lenyewe ni laini hivyo mmengenyo wake ni rahisi ndiyo maana hamna maumivu ya tumbo, mihogo ina ugumu hivyo ukila mingi wakati wa mmengenyo (Digestion). Sumu ingesikia maumivu ya kichwa.

Hebu jaribu kula kiasi kikubwa cha nyama choma ya ng'ombe, lazima tumbo utalisikia na hali fulani, alafu kula kiasi kama hicho cha nyama mbuzi choma, hali uliyoisikia tumboni ulipokula ng'ombe, hiwei isikia.

Sababu mbuzi nyama laini, kuliko ng'ombe.
 
Ni sehemu gani za huko Morogoro kwenye athari za DDT?
 
Ni sehemu gani za huko Morogoro kwenye athari za DDT?
Aisee unanipa kazi ya kukutafutia ila hili swala limefanyiw research na watu wengi sana lilikuw reported kipindi cha nyuma mpak ITV that's how I came to know. .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…