Kula yako ipoje? huwa unakula unachokiona au mpaka ujiandae kiakili

Kula yako ipoje? huwa unakula unachokiona au mpaka ujiandae kiakili

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
25,030
Reaction score
61,298
Kwa mfano kwa Sisi wapenda pombe huwa kula yetu ni ya Kiasi tunamfuata Janabi, sasa Mimi binafsi ukiniamsha asubuhi ukanishtukiza eti kula supu ya kuku hii hapa aisee huwa siwezi.

Mimi napenda niamke asubuhi nianze kujiandaa na kutafakari nini Leo samaki au utumbo ndizo au majani ya maboga au Leo Nina hamu na tembere nilitafute niandaliwe ndo niwe na hamu ya kula tena napenda kula nisiwe peke yangu niwe na wadau ndo nitatembeza ugali vizuri.
 
Mimi sijui kuchagua, na nyongo yangu haina kukataa kitu, hata niwe nimelewa ugali, sijui wali napiga tu. Na hakuna kurudisha chenji.

Na sihitaji kundi la watu ndio niweze kula hata man alone napiga tu.

Sijui makande,sijui pilau napiga tu,
Nikilewa labda uji tu ndio siwezi kunywa. 😁
 
hang over inatesa sana aisee mim nikiamka na hangover naanza na maji yenye limao baada ya hapo natafuta supu kwanza ila kula mimi siwezi kuamua nile nini labda mtu anichagulie. naweza kwenda hadi mgahawani nikiwa sijui nitakula nini
 
Back
Top Bottom