Kulalamika tumeibiwa kura za kwenye mabegi huku hamuendi Mahakamani, tuwaeleweje?

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
8,734
Reaction score
5,750
He who alleges must prove. Hii ni moja ya principle muhimu sana katika kuhakikisha haki inapatikana.

Mnalalamika zaidi ya miezi miwili kuwa uchaguzi haukuwa huru. Mlikamata kura za kwenye mabegi ambao ulikuwa ni ushahidi tosha kuwa mmeibiwa.

Mbona hamfungui kesi kupinga matokeo ya uchaguzi wa Ubunge?

Mnadai hamna imani na mahakama za Tanzania. Mbona mahakama hii ambayo hamna imani nayo ilimpa ushindi Ester Bulaya dhidi ya wana CCM waliopinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge 2015 huko Bunda?

Kwa mantiki hii,kama muda wa kupinga matokeo bado. Kwa kuwa mnao ushahidi jinsi mlivyoibiwa kwenye mabegi. Fungueni kesi kupinga matokeo ya ubunge. Maana tutapata ukwli jinsi mlivyoibiwa.
 
Kuna ushahidi wa kila aina ule haukuwa uchaguzi yalikuwa maonesho tu, sasa msilazimishe werevu waende kwenye mahakama zenu halafu muamue kesi kwa mapenzi ya bosi wenu ili mhalalishe ule upuuzi mlioufanya.

Wacha kila kitu kibaki hivyo hivyo, kila mwenye macho haambiwi tazama, ule uchaguzi umeliaibisha sana taifa letu.
 
Mbona Wassira alishindwa na Ester Bulaya mahakamani?
 
He who alleges must prove. Hii ni moja ya principle muhimu sana katika kuhakikisha haki inapatikana.....
Mahakama hii ambayo Jaji Mkuu ndio huyo mliye naye , na mahakimu wanaccm akina Simba ! itakuwa kituko sana kwa Chadema kwenda Mahakamani
 
He who alleges must prove. Hii ni moja ya principle muhimu sana katika kuhakikisha haki inapatikana....
Kura zipi zilizokamatwa kwenye mabegii?? Ile ilikua nikutafuta kuchafua taswira ya uchaguzii baaada ya kuona wanagaragazwa asubuhiii saana. Kibaya zaedi wakaigiza kuzichoma. We we ukamate nyaraka kama zile halafu ujichukulie sheria mkononi kuzichoma bilahata kufikisha kwenye vyombo husika??
 
Mahakama hii ambayo Jaji Mkuu ndio huyo mliye naye , na mahakimu wanaccm akina Simba ! itakuwa kituko sana kwa Chadema kwenda Mahakamani
Msitutoe fahamu,Bulaya na makamanda mlipokuwa mnashind kesi hazikuwa hizi mahakama?
 
Una hakika zilichomwa zote? kura zimelipakaa nchi nzima kuna haja gani kuogopa kuzichoma baadhi?

Mpaka ushahidi wa video upo, bora ufunge mdomo wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…