Usikate tamaa kabla ya kupata majibu.........
By SaidAlly :
............Asante kwa maujuzi tumekusikia na tutaifuatilia!
Nadhani Yesu alitoa snacks tu ili watulize njaa Ingawa waliishia kushiba na kusaza. Na mikate ya kipindi hicho inaweza kuwa tofautiMkuu unaweza kutohoa maana ya neno "kitoweo"
Kama yesu aligawa samaki (high protein) na mikate (carbohydrate) ambaye (kwa waamini) anahusika na uumbaji unataka kusema mnamzidi knowledge huyu mpakwa mafuta????!
Jipange upya kwenye eneo hili uje upya manake nyama ni kitoweo cha ugali. Hii ni toka zamani.
Nadhani Yesu alitoa snacks tu ili watulize njaa Ingawa waliishia kushiba na kusaza. Na mikate ya kipindi hicho inaweza kuwa tofauti
Ukasome kidogo biblia kitabu cha Yohana 21:5
Haielezei mkate ulitengenezwa na nini.
Hoja ya kutokula vyakula vyenye protins na CHO psmoja eti kwa kuwa protins zenameng'enywa kwenye acidic env na CHO kwenye alkaline env haijazingatia ukweli kwamba wanga (CHO) inameng'enywa mdomono na ptyaline enzyme na proteins tumboni. Unachotakiwa kufanya ni kutafuna mara 23 kabla hujameza kila tonge la wanga.
Sisi kazi yetu ni kukushauri usivute sigara, usinye pombe sana, vaa kondomu mara zote, punguza kitambi, usile chumvi nyingi ni hatari kwako, lakini mwamuzi wa kufuata au kuacha ni wako na ni mali yako, mungu akipenda tutaonana wodini na mortuary mungu atakapokuwa amekupenda zaidi kwa kansa ya tezi dume au stroke!Kuna tabia kwa umri wangu huu kuziacha ni ngumu. Asante kwa somo BTW
Asante sana kavulata kwa somo zuri ila ninyi madaktari mnatuchanganya sana na shauri mnazotupatia, vipi basi katika mlo wangu nikaweka starch kidogo,protein kdogo na greens nyingi,mfano nikaweka ugali kiasi cha robo au nusu ngumi,samaki 1 na saladi bakuli nzima limejaa.
Na hapo kwenye matunda umeshauri tusichanganye lakini ninyi madaktar mnatushauri tule matunda mchanganyiko na ndiyo maana sasahivi wamama weng wamejiajiri kwenye hiyo biashara hasa yale yalomenywa na kupakiwa kwenye kontena na kufungwa na karatas aina ya nylon,vipi hapa unatushauri vipi?
vipi sasa tusile kabisa matunda mchanganyiko? Naamaanisha nimechagua kula ya baridi tu lakini mchanganyiko ni sawa?au makali tu lakini mchanganyiko ni sawa?
Vipi na juisi mchanganyiko unatushauri nini?
Malengo yako ya kula starch ni kuliomba tumbo lako likisage chakula hilo na hatimaye kikupatie glucose ambayo itavyonzwa kwenda kwenye damu kupitia kwenye ini kisha kusambazwa mwilini kikaunguzwe huko kwenye mitochondria kinapokutana na oxygen ili upate nguvu zinazohitajika mwilini kwa kazi mbalimbali kama vile kutembea, kuona, kusikia, moyo kudunda, kuhema, n.k, n.k. kwahiyo mchakato huo wote unahitaji kuwepo kwa mimeng'enyo inayozalishwa kuanzia ngazi ya mdomo (kwenye mate) hadi tumboni. Hivyo kama ukila starch kidogo sana kiasi hicho inaweza kukupa ahuweni kidogo kwasababu starch yako ambayo ni kidogo itaanza kumeng'enywa kuanzia mdomoni na ptyaline na amylase za kwenye mate kwa kiwango kikubwa wakati protein yako itaanza kumeng;enywa kuanzia level ya tumbo, na mboga za majani zitasaidia kuzikingia kifua enzymes zilizotoka mdomoni ziendelee kuimeng'enya starch yako (ambayo sio nyingi) hadi tumboni kabla tumbo halijachachuka sana kutokana na uwepo wa protein tumboni. Hvyo ni heri ule kama unavyosema vina afadhali.
Kuhusu mchanganyiko wa matunda, watu wengi wanachanganya matunda kwasababu ya kupata radha na flevor na sio kwasababu ya afya ya mwili, wewe usifanye hivyo, nunua matunda yako kisha muda ukifika kula matango tu, baada ya muda (saa 1 hivi) kula machungwa yako, baada ya muda kula tikitimaji lako ndiyo afya hiyo.
Angalia hata wanyama wanavyokula, simba anakula nyama tu, lakini akizidiwa anaweza kula majani lakini hawezi kuvamia shamba la mkulima na kula mahindi kama tumbili, ng'ombe atakula majani tu hawezi kula nyama lakini unaonaje afya zao huko porini?
Sie ni wazee wa vice versa, asubuhi chai vitumbua viwili, mchana na usiku ndipo tunapiga milima ya nguvu haswa kumbe kile cha asubuhi ndio kilitakiwa kiwe cha usikuAsante. Ila nadhani mpaka hapa nilipo fikia huo ndio utaratibu wa maisha na wazee wangu waliishi hivyo ... sasa nadhani hizi sumu za kula ugali nyama au wali nyama nimezizoea
Mkuu unaweza kutohoa maana ya neno "kitoweo"
Kama yesu aligawa samaki (high protein) na mikate (carbohydrate) ambaye (kwa waamini) anahusika na uumbaji unataka kusema mnamzidi knowledge huyu mpakwa mafuta????!
Jipange upya kwenye eneo hili uje upya manake nyama ni kitoweo cha ugali. Hii ni toka zamani.