Kuleni Tikitimaji (Water Melon) kwa tahadhari

Kuleni Tikitimaji (Water Melon) kwa tahadhari

Hoja ya kutokula vyakula vyenye protins na CHO psmoja eti kwa kuwa protins zenameng'enywa kwenye acidic env na CHO kwenye alkaline env haijazingatia ukweli kwamba wanga (CHO) inameng'enywa mdomono na ptyaline enzyme na proteins tumboni. Unachotakiwa kufanya ni kutafuna mara 23 kabla hujameza kila tonge la wanga.
 
Kiuhalisia kwa mwananchi wa kawaida ni ngumu kufuata huu utaratibu wa mlo.
 
Cha msingi ni kupiga zoezi la kutosha. Na kufuata mpangilio vya chakula ipasavyo. Haya mambo ya masaa ni mbwembe tu. Tizi mwanzo mwisho na kuhakikisha msosi wa mpangilio over.
 
Hii mada nzuri isipokuwa sisi walalahoi tunakula tunchokipata na sio tunachokitaka...na mara nyingi milo yetu huwa ni bora kushiba na hayo mambo ya sijui madini na kujenga mwili itajulikana huko huko tumboni.....huku nikiwa nimeshiba....
Maana mtu unaweza ukala maharage mpaka ukiyaona unasikia kichefu chefu...
 
Mkuu unaweza kutohoa maana ya neno "kitoweo"
Kama yesu aligawa samaki (high protein) na mikate (carbohydrate) ambaye (kwa waamini) anahusika na uumbaji unataka kusema mnamzidi knowledge huyu mpakwa mafuta????!

Jipange upya kwenye eneo hili uje upya manake nyama ni kitoweo cha ugali. Hii ni toka zamani.
 
Kavulata... Kaharufu kale kabeberu!!!! Asante Mwanetuu somo limekaa vema
 
Mkuu unaweza kutohoa maana ya neno "kitoweo"
Kama yesu aligawa samaki (high protein) na mikate (carbohydrate) ambaye (kwa waamini) anahusika na uumbaji unataka kusema mnamzidi knowledge huyu mpakwa mafuta????!

Jipange upya kwenye eneo hili uje upya manake nyama ni kitoweo cha ugali. Hii ni toka zamani.
Nadhani Yesu alitoa snacks tu ili watulize njaa Ingawa waliishia kushiba na kusaza. Na mikate ya kipindi hicho inaweza kuwa tofauti
 
Kwa maana hiyo unatakiwa ule chakula kama ugali wa muhogo namboga yake iwe karanga nani anaeweza mlo wa ajabu kama huu.
 
Haielezei mkate ulitengenezwa na nini.

Mkuu Kwani inawezekana mkate ukatengenezwa kwa mchicha!!!!

Ni dhahiri ukitembea mguu hauendi na mkono wake, na mkate kutengenezwa kwa ngano na kutiwa chachu ama mikate ya tambiko ile isiyotiwa chachu.
 
Kuna tabia kwa umri wangu huu kuziacha ni ngumu. Asante kwa somo BTW
 
Hoja ya kutokula vyakula vyenye protins na CHO psmoja eti kwa kuwa protins zenameng'enywa kwenye acidic env na CHO kwenye alkaline env haijazingatia ukweli kwamba wanga (CHO) inameng'enywa mdomono na ptyaline enzyme na proteins tumboni. Unachotakiwa kufanya ni kutafuna mara 23 kabla hujameza kila tonge la wanga.

Unatisha mkuu, kwahiyo utawashauri wagonjwa wako wahesabu wakati wa kula ili watafune mara 23 kabla ya kumeza? umesoma chuo gani?.

Ni sehemu ndogo sana ya carbohydrate (tena starch tu) inayoweza kuwa digested mdomoni na ptyaline iliyoko kwenye mate lakini zoezi zima la kudigest CHO linatokea tumboni kwa msaada wa amylase na ptyaline kidogo.

Unachoshauri wateja wako wafanye ni kiini macho, huwa hatuhesabu umetafuna mara ngapi kabla ya kumeza. Hata hivyo lengo la kutafuna ni kuzalisha saliva nyingi yenye ptyaline na amylase nyingi pamoja na NaCO3/KCO3 (alkaline) ili kuongeza (neutralize) pH ya tumboni inayofaa kwa kumeng'enya CHO, tendo hili litatatizwa na kula nyama kwa wakati huohuo kwakuwa nyama itakwenda kushusha pH kwa kuzalisha HCl (hydrochloric acid) tumboni ili pepsinogen ziweze kusaga nyama. Ndiyo maana kama mtu mwenye vidonda vya tumbo atakula nyama atakiona cha mtema kuni kwa sababu uchachu utazidi tumboni mara ++++ kwa sababu ya kula nyama. Kaka watch out na ushauri wako kwa wagonjwa wako.
 
Kuna tabia kwa umri wangu huu kuziacha ni ngumu. Asante kwa somo BTW
Sisi kazi yetu ni kukushauri usivute sigara, usinye pombe sana, vaa kondomu mara zote, punguza kitambi, usile chumvi nyingi ni hatari kwako, lakini mwamuzi wa kufuata au kuacha ni wako na ni mali yako, mungu akipenda tutaonana wodini na mortuary mungu atakapokuwa amekupenda zaidi kwa kansa ya tezi dume au stroke!
 
Asante sana kavulata kwa somo zuri ila ninyi madaktari mnatuchanganya sana na shauri mnazotupatia, vipi basi katika mlo wangu nikaweka starch kidogo,protein kdogo na greens nyingi,mfano nikaweka ugali kiasi cha robo au nusu ngumi,samaki 1 na saladi bakuli nzima limejaa.

Na hapo kwenye matunda umeshauri tusichanganye lakini ninyi madaktar mnatushauri tule matunda mchanganyiko na ndiyo maana sasahivi wamama weng wamejiajiri kwenye hiyo biashara hasa yale yalomenywa na kupakiwa kwenye kontena na kufungwa na karatas aina ya nylon,vipi hapa unatushauri vipi?

vipi sasa tusile kabisa matunda mchanganyiko? Naamaanisha nimechagua kula ya baridi tu lakini mchanganyiko ni sawa?au makali tu lakini mchanganyiko ni sawa?

Vipi na juisi mchanganyiko unatushauri nini?
 
Last edited by a moderator:

Malengo yako ya kula starch ni kuliomba tumbo lako likisage chakula hilo na hatimaye kikupatie glucose ambayo itavyonzwa kwenda kwenye damu kupitia kwenye ini kisha kusambazwa mwilini kikaunguzwe huko kwenye mitochondria kinapokutana na oxygen ili upate nguvu zinazohitajika mwilini kwa kazi mbalimbali kama vile kutembea, kuona, kusikia, moyo kudunda, kuhema, n.k, n.k. kwahiyo mchakato huo wote unahitaji kuwepo kwa mimeng'enyo inayozalishwa kuanzia ngazi ya mdomo (kwenye mate) hadi tumboni. Hivyo kama ukila starch kidogo sana kiasi hicho inaweza kukupa ahuweni kidogo kwasababu starch yako ambayo ni kidogo itaanza kumeng'enywa kuanzia mdomoni na ptyaline na amylase za kwenye mate kwa kiwango kikubwa wakati protein yako itaanza kumeng;enywa kuanzia level ya tumbo, na mboga za majani zitasaidia kuzikingia kifua enzymes zilizotoka mdomoni ziendelee kuimeng'enya starch yako (ambayo sio nyingi) hadi tumboni kabla tumbo halijachachuka sana kutokana na uwepo wa protein tumboni. Hvyo ni heri ule kama unavyosema vina afadhali.

Kuhusu mchanganyiko wa matunda, watu wengi wanachanganya matunda kwasababu ya kupata radha na flevor na sio kwasababu ya afya ya mwili, wewe usifanye hivyo, nunua matunda yako kisha muda ukifika kula matango tu, baada ya muda (saa 1 hivi) kula machungwa yako, baada ya muda kula tikitimaji lako ndiyo afya hiyo.

Angalia hata wanyama wanavyokula, simba anakula nyama tu, lakini akizidiwa anaweza kula majani lakini hawezi kuvamia shamba la mkulima na kula mahindi kama tumbili, ng'ombe atakula majani tu hawezi kula nyama lakini unaonaje afya zao huko porini? Ndege (kuku, bata, njiwa, n.k), na nguruwe (omnivorous) ndiyo waliobarikiwa na Mungu kuwa na matumbo yanayoweza kusaga aina mbalimbali za vyakula (carbohydrates, proteins, matunda, majani, n.k) bila shida nyingi. Lakini kwa tabia hii ya nguruwe kuweza kula na kusaga vyakula vya aina mbalimbali ndiyo maana tunasema nyama ya nguruwe haifai kwa chakula cha binadamu kwakuwa ina sumu nyingi saaana, lazima iliwe kwa tahadhari kubwa, usile utumbo, ini, damu, figo, nk la sivyo tutaonana wodini na mortuary kama mungu atakupenda zaidi kwa kupenda sana kulanyama za nguruwe.
 
Malengo yako ya kula starch ni kuliomba tumbo lako likisage chakula hilo na hatimaye kikupatie glucose ambayo itavyonzwa kwenda kwenye damu kupitia kwenye ini kisha kusambazwa mwilini kikaunguzwe huko kwenye mitochondria kinapokutana na oxygen ili upate nguvu zinazohitajika mwilini kwa kazi mbalimbali kama vile kutembea, kuona, kusikia, moyo kudunda, kuhema, n.k, n.k. kwahiyo mchakato huo wote unahitaji kuwepo kwa mimeng'enyo inayozalishwa kuanzia ngazi ya mdomo (kwenye mate) hadi tumboni. Hivyo kama ukila starch kidogo sana kiasi hicho inaweza kukupa ahuweni kidogo kwasababu starch yako ambayo ni kidogo itaanza kumeng'enywa kuanzia mdomoni na ptyaline na amylase za kwenye mate kwa kiwango kikubwa wakati protein yako itaanza kumeng;enywa kuanzia level ya tumbo, na mboga za majani zitasaidia kuzikingia kifua enzymes zilizotoka mdomoni ziendelee kuimeng'enya starch yako (ambayo sio nyingi) hadi tumboni kabla tumbo halijachachuka sana kutokana na uwepo wa protein tumboni. Hvyo ni heri ule kama unavyosema vina afadhali.

Kuhusu mchanganyiko wa matunda, watu wengi wanachanganya matunda kwasababu ya kupata radha na flevor na sio kwasababu ya afya ya mwili, wewe usifanye hivyo, nunua matunda yako kisha muda ukifika kula matango tu, baada ya muda (saa 1 hivi) kula machungwa yako, baada ya muda kula tikitimaji lako ndiyo afya hiyo.

Angalia hata wanyama wanavyokula, simba anakula nyama tu, lakini akizidiwa anaweza kula majani lakini hawezi kuvamia shamba la mkulima na kula mahindi kama tumbili, ng'ombe atakula majani tu hawezi kula nyama lakini unaonaje afya zao huko porini?

Nimekuelewa daktari,asante kwa ushauri.
 
Asante. Ila nadhani mpaka hapa nilipo fikia huo ndio utaratibu wa maisha na wazee wangu waliishi hivyo ... sasa nadhani hizi sumu za kula ugali nyama au wali nyama nimezizoea
Sie ni wazee wa vice versa, asubuhi chai vitumbua viwili, mchana na usiku ndipo tunapiga milima ya nguvu haswa kumbe kile cha asubuhi ndio kilitakiwa kiwe cha usiku
 
Mkuu unaweza kutohoa maana ya neno "kitoweo"
Kama yesu aligawa samaki (high protein) na mikate (carbohydrate) ambaye (kwa waamini) anahusika na uumbaji unataka kusema mnamzidi knowledge huyu mpakwa mafuta????!

Jipange upya kwenye eneo hili uje upya manake nyama ni kitoweo cha ugali. Hii ni toka zamani.

jogi hapo umegusa kona nyingine ambayo inatumia moyo badala ya ubongo wa binadamu. Kwa tabia hiyo ya kuchanganya nyama na mkate ndiyo maana hata wao hatujawakuta wamekufa pia ingawa wao walikuwa na kazi nyingi sana za mazoezi, kupigana kwa rungu na mikuki, kutembea na kubeba mizigo mizito magegani na vichwani, kusaga nafaka kwa kutumia jiwe la mkono n.k kuliko sisi wa leo (sharobaro). Kumbuka kuwa kama walivyo wanyama wengine wote, Mungu aliumba watu bila kutupa moto wa kupikia vyakula kwakuwa anafahamu kuwa kupika chakula kunapunguza ubora wake. Mpango wa Mungu ulikuwa sisi (binadamu) tuishi kwa kula matunda, mizizi (mihogo, viazi), nafaka, mboga, kuokota mayai, asali na kunywa maziwa (kwa watoto tu) tu bila ya kupika kama wanavyofanya wadogo zetu akina nyani, tumbili, kima, soko, n.k. Hakuna ushahidi unaonyesha kuwa katika bustani ya Eden ambako Adam na Eva waliishi kulikuwa kuna moto na walikuwa wanapika vyakula wala kula nyama.

Ona hata meno yako ni tofauti na ya wanyama walioumbwa kwa makusudi ya kula nyama (carnivorous) tu, kwa utundu wetu tukaharibu vitu vingi ikiwemo kuvipika vyakula na kula nyama, chumvi, kukamua mafuta ya kuyala kwa wingi, sukari, kukoboa nafaka na kukaanga chips. Huu ni ujinga unaoambatana na kiburi kwa Mungu eti kuwa Mungu katupa sisi akili nyingi kuliko viumbe wengine, falsafa ambayo leo hii inatuangamiza kwa magonjwa, ajali (mabomu, majengo, moto, magari, ndege, migodi kuporomoka, umeme, meli kuzama,), kuoana wanaume kwa wanaume, kubaka watoto wadogo, kuharibu mazingira yetu na ya viumbe wengine huku tukiwaacha ndege wakibarikiwa mabawa ya kurukia, nyuki wakibarikiwa kwa kutengeneza asali na uwezo wa kuwauma watu hadi kufa, mchwa wakitengeneza milima na ndege wakiimba angani kwa furaha na bila hofu yoyote.

Ndiyo maana nimekwambia kuwa kona yako hii ni ngumu sana kuijadili hapa maana inahitaji imani zaidi kuliko akili.
 
Back
Top Bottom