Mkuu unaweza kutohoa maana ya neno "kitoweo"
Kama yesu aligawa samaki (high protein) na mikate (carbohydrate) ambaye (kwa waamini) anahusika na uumbaji unataka kusema mnamzidi knowledge huyu mpakwa mafuta????!
Jipange upya kwenye eneo hili uje upya manake nyama ni kitoweo cha ugali. Hii ni toka zamani.
jogi hapo umegusa kona nyingine ambayo inatumia moyo badala ya ubongo wa binadamu. Kwa tabia hiyo ya kuchanganya nyama na mkate ndiyo maana hata wao hatujawakuta wamekufa pia ingawa wao walikuwa na kazi nyingi sana za mazoezi, kupigana kwa rungu na mikuki, kutembea na kubeba mizigo mizito magegani na vichwani, kusaga nafaka kwa kutumia jiwe la mkono n.k kuliko sisi wa leo (sharobaro). Kumbuka kuwa kama walivyo wanyama wengine wote, Mungu aliumba watu bila kutupa moto wa kupikia vyakula kwakuwa anafahamu kuwa kupika chakula kunapunguza ubora wake. Mpango wa Mungu ulikuwa sisi (binadamu) tuishi kwa kula matunda, mizizi (mihogo, viazi), nafaka, mboga, kuokota mayai, asali na kunywa maziwa (kwa watoto tu) tu bila ya kupika kama wanavyofanya wadogo zetu akina nyani, tumbili, kima, soko, n.k. Hakuna ushahidi unaonyesha kuwa katika bustani ya Eden ambako Adam na Eva waliishi kulikuwa kuna moto na walikuwa wanapika vyakula wala kula nyama.
Ona hata meno yako ni tofauti na ya wanyama walioumbwa kwa makusudi ya kula nyama (carnivorous) tu, kwa utundu wetu tukaharibu vitu vingi ikiwemo kuvipika vyakula na kula nyama, chumvi, kukamua mafuta ya kuyala kwa wingi, sukari, kukoboa nafaka na kukaanga chips. Huu ni ujinga unaoambatana na kiburi kwa Mungu eti kuwa Mungu katupa sisi akili nyingi kuliko viumbe wengine, falsafa ambayo leo hii inatuangamiza kwa magonjwa, ajali (mabomu, majengo, moto, magari, ndege, migodi kuporomoka, umeme, meli kuzama,), kuoana wanaume kwa wanaume, kubaka watoto wadogo, kuharibu mazingira yetu na ya viumbe wengine huku tukiwaacha ndege wakibarikiwa mabawa ya kurukia, nyuki wakibarikiwa kwa kutengeneza asali na uwezo wa kuwauma watu hadi kufa, mchwa wakitengeneza milima na ndege wakiimba angani kwa furaha na bila hofu yoyote.
Ndiyo maana nimekwambia kuwa kona yako hii ni ngumu sana kuijadili hapa maana inahitaji imani zaidi kuliko akili.