Faru_johny
JF-Expert Member
- Feb 8, 2014
- 343
- 304
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi nna tatizo la tumbo kuunguruma.. na nadhani ni geai kuwa nyingi tumboni. Nawezaje kulitatua tatizo langu ?... nitumie dawa gani au vyakula gani nitumie na vipi nisitumie. Na je,nini madhara ya tatizo hilo ?. Msaada tafadhali mkuu kavulata
everlenk niwie radhi kwa kuchelewa kukujibu kuhusu chai ya maziwa, sijui kama upo kwenye uzi.
Maziwa Maziwa Maziwa!
Maziwa yana protein ya wanyama ambayo kutokana na mchakato wa umeng'enyaji tumboni tumesema unakinzana kwa kiasi kikubwa na mchakato wa umeng'enyaji wa carbohydrates tumboni pia, hivyo haifai kuchanganya tumboni kwako sukari, chapati/vitumbua/bagia/mkate/tambi (CHO) na maziwa (kwenye chai). Hivyo tunashauriwa maziwa yanywewe kama maziwa kwa wakati wake bila kuongezwa sukari wala akina chapati.
LAKINI pia: maziwa yana Calcium nyingi sana na sukari aina ya lactose nyingi. Kwa asili na kwa maumbile ya Mwenyezi Mungu maziwa ni kwa watoto wachanyanga wa binadamu na wanyama wengine wanaonyonyesha (mamalia). Watoto wachanga wanayo miundombinu madhubuti inayowezesha mtoto kunywa/kunyonya, kumeng'enya, kusaga na kufyonza mwilini protein, sukari (lactose) na mazagazaga yote yaliyomo kwenye maziwa kwa urahisi. Miundombinu hii muhimu kwa usagaji wa maziwa inatoweka polepole kadri umri wa mtu unavyoongezeka. Hivyo, Watu na wanyama wakubwa hawapaswi kunywa maziwa hata kidogo maana miili yao imeshapoteza enzymes muhimu (renin) kwa usagaji maziwa tumboni, hatuwezi kuitumia protein iliyoko kwenye maziwa kama walivyo watoto wachanga. Mfano, kati ya watu wazima 10 watakaokunywa maziwa fresh au chai ya maziwa 6 kati yao huwa wataharisha, tumbo kujaa gesi, kunguruma na kuuma (lactose intolerance) muda mfupi baada ya kunywa maziwa kwasababu ya kukosa mmeng'enyo muhimu unaohitajika kumeng'enya sukari (lactose) iliyomo kwenye maziwa.
Mungu hakutengeneza maziwa kwaajili ya watu mazima ila watoto tu, ndio maana anatukomesha tunaokunywa maziwa ya watoto kwa kuharisha, kujaa gesi tumboni na vidonda vya tumbo kwa kunywa maziwa. Wako watu wazembe wanaokunywa maziwa wakizani kuwa maziwa yatawaponya vidonda vya tumbo, huu ni ujinga, usinywe maziwa hata kidogo kama unahisi kuwa una vidonda vya tumbo maana utakiona cha mtema kuni kama una ulcers halafu unakunywa maziwa.
kavulata samahani maswali yamekuwa mengi,naona umetushauri ni vizuri tunywe mtindi, je mtindi wa viwandani unafaa? mfano katika makampuni ya hapa nyumbani kama Asas,Tanga fresh,Mara milk n.k
Pia umeshauri kwa habari ya nyanya mbichi kwamba ina Oxalate,vipi tunapokuwa tunakula kachumbari na aina nyingine ya vyakula, je ni sawa au si sawa?
Mitindi ni mingi na watengenezaji tofauti na hii ni bidhaa kama zilivyo bidhaa nyingine sokoni, wewe tumia zile kanuni zinazohusiana na bidhaa za vyakula:
1. Angalia nembo ya ubora (tbs) kwenye bidhaa
2. Angalia expiry date ya bidhaa
3. Angalia kama seal ya kifungashio haijaharibika (paketi haivuji)
4. Angalia kama bidhaa imehifadhiwa kwenye mazingira yanayopendekezwa (usafi, joto)
5. Tumia uzoefu wako kupima ubora (radha, ubora, utashi)
Mimi binafsi huwa nagandisha mtindi wangu mwenyewe kwenye familia yangu. Nikizidiwa huwa natumia mtindi wa Tanga fresh kwakuwa nilibahatika kuona namna unavyotayarishwa. Maziwa haya huwa yanakususanywa kutoka kwa wakulima/wafugaji wadogo wenye ng'ombe za kienyeji kabisa waliopewa vifaa maalumu vya kukusanyia maziwa na mafunzo fulani na kufikishwa kiwandani kwenye hali ya usafi, hivyo nikavutiwa na maziwa yao, angalau nafahamu kuwa Tanga fresh ni maziwa halisi ya ng'ombe mengi yakiwa ya ng'ombe wa kienyeji kutoka kwa wakulima wa kawaida kabisa. Ila maziwa yote nadhani yanapitia mlolongo unaofahamika kwa taifa kabla hayajafika kwa mlaji.
Somo limenoga: Oxalic Acid ni nini? Kifupi hii ni aina ya acid iliyoko kww wingi kwenye mboga za majani na baadhi ya matunda. Vyakula vilivyo na oxalic acid nyingi ni kama vile mchicha, spinachi, lettuce, kitunguu saumu, maharage, karoti, soya, nyanya, n.k. oxalic acid inapokutana na madini kama vile calcium, magnesium, chuma (Iron) huko tumboni huwa vinakamatana na kutengengenza chumvi (salt) inayoitwa oxalate (calcium oxalate, magnesium oxalate, etc.). Kitendo hiki hiki haramu kinasababisha madhara ya aina 2 kwa binadamu:kavulata samahani maswali yamekuwa mengi,naona umetushauri ni vizuri tunywe mtindi, je mtindi wa viwandani unafaa? mfano katika makampuni ya hapa nyumbani kama Asas,Tanga fresh,Mara milk n.k
Pia umeshauri kwa habari ya nyanya mbichi kwamba ina Oxalate,vipi tunapokuwa tunakula kachumbari na aina nyingine ya vyakula, je ni sawa au si sawa?
kiuhalisia kwa mwananchi wa kawaida ni ngumu kufuata huu utaratibu wa mlo.
watu wenye maisha nafuu wanaweza lakini m'bongo wa kawaida ni ngumu.wengine hata ratiba constant ya chakula hawana.majangaaaa.
kavulata naomba msaada jinsi ya kupangilia mlo kwa mgonjwa wa Kifua Kikuu,nina ndugu yangu namuuguza nnimeambiwa ale zaidi vyakula vya Protein,Carbohydrates na Vitamini,vitu kama maziwa,mayai,maharage na soya visikosekane kwenye mlo wake kwa siku.
Pole sana kwa kuuguza, kanuni ni ile ile usichanganye nyama na starch pamoja, usichanganye matunda matamu na matunda machachu pamoja, usichanyanye matunda yenye acidi na matunda yasiyo na acid (alkaline) pamoja. Siku ina masaa 24 hivyo panga masaa ya kula nyama, mayai, maziwa, wali/ugali, matunda na mboga za majani kwa siku. tulisema kuwa ugali/wali/tambi/muhogo vinaweza kuliwa pamoja na mboga za majani, maharagwe, kunde, nyegere, soya, n.k. Nyama inaweza kuliwa pamoja na mboga za majani (kabichi, spinach, mchicha, kachumbali, n.k), maziwa na matunda vitafutiwe muda wake kila kimoja, maji yatafutiwe muda wake wa kunywewa.