Kuleni Tikitimaji (Water Melon) kwa tahadhari

Kuleni Tikitimaji (Water Melon) kwa tahadhari

Mimi nna tatizo la tumbo kuunguruma.. na nadhani ni geai kuwa nyingi tumboni. Nawezaje kulitatua tatizo langu ?... nitumie dawa gani au vyakula gani nitumie na vipi nisitumie. Na je,nini madhara ya tatizo hilo ?. Msaada tafadhali mkuu kavulata
 
Last edited by a moderator:

Pole jonnie. Kimbilia hospitali ya karibu kulishitakia tatizo lako, maana tumbo kunguruma na kujaa gesi kuna maana nyingi. Miongoni mwa sababu zinazoweza kusababisha hali kama hii ni pamoja na utumbo kuziba (obstruction), hernia, na kuwa na tatizo la kumeng'enya vyakula. Tumbo linaweza kuzibwa na uwepo wa minyoo (ascaris, tegu) mingi tumboni, henia au constipation. Gundua kwanza chanzo cha tatizo kabla ya kufikiria njia za kutibu. Pima choo kikubwa ili ujue kama una minyoo, pima tumbo kwa gastroscopy/ultrasound/barium meal ili ujue kama una vidonga vya tumbo au tatizo lingine kama uvimbe tumboni/utumboni. Vyakula vinavyoongoza kwa kusababisha kuwa na gesi nyingi ni aina ya mikunde na viazi.
 
Matumbo yetu, viungo vyetu na miili yetu huwa tunavisononeshwa kupita kiasi kwa mambo yafuatayo:
1. Kula nyama kila mara kila siku
2. Kuchanganya nyama na ugali/wali, n.k pamoja
3. Kula nyama ya nguruwe (hasa fresh roast)
4. Kula nyama ambayo haijaiva
5. Tumbo kukosa chakula kabisa kwa muda mrefu
6. Kupika sana vyakula (mboga za majani)
7. Kunywa pombe nyingi
8. Kula sukari nyingi
9. Kula chumvi nyingi
10. Watu wazima kunywa maziwa
11. Kumeza madawa bila utaratibu unaokubalika
12. Kula matunda na chakula hapohapo
13. Kula na kunywa maji wakati huohuo
14. Kula ugali na kwenda kulala hapopo
15. Kukoboa vyakula (nafaka) kupita kiasi
16. Kula mafuta mengi (siagi, fat, cooking oil)
17. Kuvuta sigara
18. Kula uchafu (mavi, kemicals na sumu nyingine)
19. Kula nyama zenye kamba ndefu sana (ng'ombe, mbuzi, nyati, etc.)
20. Kula bila kufanya mazoezi wala kutoa jasho
21. Kunywa maji/vinywaji baridi sana
22. Kula chakula kingi bila sababu ya msingi
23. Kula artificial foods (soda, juices)
 
everlenk niwie radhi kwa kuchelewa kukujibu kuhusu chai ya maziwa, sijui kama upo kwenye uzi.

Maziwa Maziwa Maziwa!

Maziwa yana protein ya wanyama ambayo kutokana na mchakato wa umeng'enyaji tumboni tumesema unakinzana kwa kiasi kikubwa na mchakato wa umeng'enyaji wa carbohydrates tumboni pia, hivyo haifai kuchanganya tumboni kwako sukari, chapati/vitumbua/bagia/mkate/tambi (CHO) na maziwa (kwenye chai). Hivyo tunashauriwa maziwa yanywewe kama maziwa kwa wakati wake bila kuongezwa sukari wala akina chapati.

LAKINI pia: maziwa yana Calcium nyingi sana na sukari aina ya lactose nyingi. Kwa asili na kwa maumbile ya Mwenyezi Mungu maziwa ni kwa watoto wachanyanga wa binadamu na wanyama wengine wanaonyonyesha (mamalia). Watoto wachanga wanayo miundombinu madhubuti inayowezesha mtoto kunywa/kunyonya, kumeng'enya, kusaga na kufyonza mwilini protein, sukari (lactose) na mazagazaga yote yaliyomo kwenye maziwa kwa urahisi. Miundombinu hii muhimu kwa usagaji wa maziwa inatoweka polepole kadri umri wa mtu unavyoongezeka. Hivyo, Watu na wanyama wakubwa hawapaswi kunywa maziwa hata kidogo maana miili yao imeshapoteza enzymes muhimu (renin) kwa usagaji maziwa tumboni, hatuwezi kuitumia protein iliyoko kwenye maziwa kama walivyo watoto wachanga. Mfano, kati ya watu wazima 10 watakaokunywa maziwa fresh au chai ya maziwa 6 kati yao huwa wataharisha, tumbo kujaa gesi, kunguruma na kuuma (lactose intolerance) muda mfupi baada ya kunywa maziwa kwasababu ya kukosa mmeng'enyo muhimu unaohitajika kumeng'enya sukari (lactose) iliyomo kwenye maziwa.

Mungu hakutengeneza maziwa kwaajili ya watu mazima ila watoto tu, ndio maana anatukomesha tunaokunywa maziwa ya watoto kwa kuharisha, kujaa gesi tumboni na vidonda vya tumbo kwa kunywa maziwa. Wako watu wazembe wanaokunywa maziwa wakizani kuwa maziwa yatawaponya vidonda vya tumbo, huu ni ujinga, usinywe maziwa hata kidogo kama unahisi kuwa una vidonda vya tumbo maana utakiona cha mtema kuni kama una ulcers halafu unakunywa maziwa.

Asante sana kavulata ila duh! Ninavyopenda chai ya maziwa mbona kazi!!
 
Last edited by a moderator:
kavulata samahani maswali yamekuwa mengi,naona umetushauri ni vizuri tunywe mtindi, je mtindi wa viwandani unafaa? mfano katika makampuni ya hapa nyumbani kama Asas,Tanga fresh,Mara milk n.k

Pia umeshauri kwa habari ya nyanya mbichi kwamba ina Oxalate,vipi tunapokuwa tunakula kachumbari na aina nyingine ya vyakula, je ni sawa au si sawa?
 
Mitindi ni mingi na watengenezaji tofauti na hii ni bidhaa kama zilivyo bidhaa nyingine sokoni, wewe tumia zile kanuni zinazohusiana na bidhaa za vyakula:
1. Angalia nembo ya ubora (tbs) kwenye bidhaa
2. Angalia expiry date ya bidhaa
3. Angalia kama seal ya kifungashio haijaharibika (paketi haivuji)
4. Angalia kama bidhaa imehifadhiwa kwenye mazingira yanayopendekezwa (usafi, joto)
5. Tumia uzoefu wako kupima ubora (radha, ubora, utashi)

Mimi binafsi huwa nagandisha mtindi wangu mwenyewe kwenye familia yangu. Nikizidiwa huwa natumia mtindi wa Tanga fresh kwakuwa nilibahatika kuona namna unavyotayarishwa, (chain yote kutoka kwa wazalishaji hadi kufika kiwandani). Maziwa haya huwa yanakususanywa kutoka kwa wakulima/wafugaji wadogo wenye ng'ombe wa kienyeji kabisa waliopewa vifaa maalumu vya kukusanyia maziwa na mafunzo fulani na kufikishwa kiwandani kwenye hali ya usafi wa hali ya juu, hivyo nikavutiwa na maziwa yao, angalau nafahamu kuwa Tanga fresh ni maziwa halisi ya ng'ombe mengi yakiwa ya ng'ombe wa kienyeji kutoka kwa wakulima wa kawaida kabisa. Ila maziwa yote nadhani yanapitia mlolongo unaofahamika kwa taifa kabla hayajafika kwa mlaji.
 
Mitindi ni mingi na watengenezaji tofauti na hii ni bidhaa kama zilivyo bidhaa nyingine sokoni, wewe tumia zile kanuni zinazohusiana na bidhaa za vyakula:
1. Angalia nembo ya ubora (tbs) kwenye bidhaa
2. Angalia expiry date ya bidhaa
3. Angalia kama seal ya kifungashio haijaharibika (paketi haivuji)
4. Angalia kama bidhaa imehifadhiwa kwenye mazingira yanayopendekezwa (usafi, joto)
5. Tumia uzoefu wako kupima ubora (radha, ubora, utashi)

Mimi binafsi huwa nagandisha mtindi wangu mwenyewe kwenye familia yangu. Nikizidiwa huwa natumia mtindi wa Tanga fresh kwakuwa nilibahatika kuona namna unavyotayarishwa. Maziwa haya huwa yanakususanywa kutoka kwa wakulima/wafugaji wadogo wenye ng'ombe za kienyeji kabisa waliopewa vifaa maalumu vya kukusanyia maziwa na mafunzo fulani na kufikishwa kiwandani kwenye hali ya usafi, hivyo nikavutiwa na maziwa yao, angalau nafahamu kuwa Tanga fresh ni maziwa halisi ya ng'ombe mengi yakiwa ya ng'ombe wa kienyeji kutoka kwa wakulima wa kawaida kabisa. Ila maziwa yote nadhani yanapitia mlolongo unaofahamika kwa taifa kabla hayajafika kwa mlaji.

Asante sana kavulata kwa ufafanuzi yakinifu barikiwa sana,ila umesahau swali lingine la nyanya......
 
Last edited by a moderator:
kavulata samahani maswali yamekuwa mengi,naona umetushauri ni vizuri tunywe mtindi, je mtindi wa viwandani unafaa? mfano katika makampuni ya hapa nyumbani kama Asas,Tanga fresh,Mara milk n.k

Pia umeshauri kwa habari ya nyanya mbichi kwamba ina Oxalate,vipi tunapokuwa tunakula kachumbari na aina nyingine ya vyakula, je ni sawa au si sawa?
Somo limenoga: Oxalic Acid ni nini? Kifupi hii ni aina ya acid iliyoko kww wingi kwenye mboga za majani na baadhi ya matunda. Vyakula vilivyo na oxalic acid nyingi ni kama vile mchicha, spinachi, lettuce, kitunguu saumu, maharage, karoti, soya, nyanya, n.k. oxalic acid inapokutana na madini kama vile calcium, magnesium, chuma (Iron) huko tumboni huwa vinakamatana na kutengengenza chumvi (salt) inayoitwa oxalate (calcium oxalate, magnesium oxalate, etc.). Kitendo hiki hiki haramu kinasababisha madhara ya aina 2 kwa binadamu:
1.) Madini hayo hayataweza kufyonzwa mwilini kwa wingi hivyo, kuupunguzia mwili madini hayo muhimu kwake. Ndiyo maana hata siku hizi hatuwashauri wagonjwa wenye upungufu wa damu (Iron deficiency anemia) wale mchicha ili kuongeza damu kwasababu mchicha una madini ya chuma lakini miili yetu haina uwezo wa kuyachukuwa madini hayo kutoka kwenye mchicha kwasababu ya oxalate.

2. Oxalates hizi zinasababisha mawe (stones) madogo kwenye mafigo (kidney stones). Ndiyo maana tunashauri kuwa watu wenye matatizo ya mafigo wapunguze kula greens na matunda yenye oxalic acid nyingi.

Ndiyo maana tunashauri kuwa oxalic acid usiikutanishe na vyakula vyenye madini mengi ya chuma, calcium, magnesium, etc kwasababu inaweza kukorofisha ufyonzaji wake mwilini na pia kukusababishia mawe kwenye mafigo, gout, n.k. Hii haimaanishi kuwa oxalic acid haina faida mwilini, lahasha! oxalic acid kwenye vyakula inaweza kuzuia maradhi ya kansa kama vile tezi tume, n.k. na vyakula vingi vinavyounguza sumu mwilini (anti-oxidants) huwa vina oxalic acid nyingi, hivyo hatuwezi kukwepa kula vyakula vyenye oxalic acid, cha muhimu ni elimu ya namna ya kula vyakula hivyo. Mfano, usiunge mboga za majani kwa kutumia maziwa.
 
Mkuu kavulata, umenena vyema kwa ku support motion hii hebu watu wasome vitabu hivi, vitawajenga katika hoja husika

Big up Uvugizi! Maswali mengi yatajibiwa kwa kusoma hapa. Pia wanaweza kuangalia hii chart kwa maelezo zaidi

VdMecl8yqd0JZKC2QQEs0Fykll4xs58yqd8yqd8yqd80kz52JlP ZRP ZRP ZRY n mAoue9tI3aAAAAABJRU5ErkJggg==
 
kiuhalisia kwa mwananchi wa kawaida ni ngumu kufuata huu utaratibu wa mlo.

watu wenye maisha nafuu wanaweza lakini m'bongo wa kawaida ni ngumu.wengine hata ratiba constant ya chakula hawana.majangaaaa.
 
watu wenye maisha nafuu wanaweza lakini m'bongo wa kawaida ni ngumu.wengine hata ratiba constant ya chakula hawana.majangaaaa.

Au kinyume chake? watu wa kawaida/maskini ndo kundi la jamii wenye kiwango kidogo sana cha magonjwa ya kisukari, pressure, stroke, ugumba, figo na unene kupita kiasi. Hii inatokana na uwezo wao mdogo wa kula nyama, maziwa, mayai, soda, juisi na chips kila siku, lakini wana uwezo mkubwa wa kufanya mazoezi ya mwili kila siku (kutembea kwa miguu, kulima, kuchunga, kubeba). Chakula cha masikini mara nyingi ni ugali na matembele/mlenda/maharagwe/kunde/mashona nguo/mgagani, n.k. Watu masikini ndo kundi la watu pia wanaopata muda mwingi wa kulala usiku maana hawana umeme, tv, wala disco, hivyo wanalazimika kulala mapema, hivyo kutoa muda mwingi kwa mwili kupunzika na kujitengeneza upya. Hivi vyote ni vitu vinavyowaepusha watu wa kawaida na magonjwa ya hovyo kama unene kupita kiasi na uhanithi yanayowasumbua matajiri wetu na watu wa kipato cha kati hapa Tanzania na katika nchi zinazoendelea. Hii ni tofauti na watu wa nchi za Ulaya na Marekani ambao kwao watu masikini ndo wanaougua sana magonjwa haya ya unene kupita kiasi, stroke, kisukari, kansa, mafigo n.k kwasababu watu maskini ndo wanaoishi kwa kula fast foods (take away) kama chips/mayai, pizza, hot dogs, hambaga, nyama za nguruwe/kuku. Watu masikini kule ulaya na marekani hawana uwezo pia wa kugharamia kwenda sehemu za kufanya mazoezi (gym) na kupata matibabu na check ups, watu maskini kule hawapati muda wa kupunzika/kulala, wenngi wao wanalazimika kufanya kazi masaa 16 hadi 24 kwa siku.
 
Dalili muhimu za ulaji mzuri wa chakula kwako:

1. Unapata haja kubwa mara 2 hadi 3 kwa siku
2. Unapata haja ndogo (mkojo) angalau lita 1.5 kwa siku
3. Body Mass Index (BMI) yako (yaani uwiano kati ya Uzito na Urefu wako) haipungui 18.5 na haizidi 29.
Unaweza kupima BMI yako kwa kupima uzito wako kwenye Kilogram (Kg) na kuugawanya na urefu wako katika mita (M) za mraba (meter squared) (M x M). Mfano mtu mwenye uzito wa Kilo 80 na urefu wa sm. 150, BMI yake ni 80/1.5 x 1.5 = 80/2.25 = 35.6. Hivyo mtu huyu mwenye BMI 35.6 atakuwa na uzito na mafuta mengi mno mwilini (obesity) usiotakiwa hata kidogo kwa afya. Mtu kama huyu yuko hatarini kupata magonjwa ya moyo, sukari, mafigo, pressure, ugumba, saratani na stroke wakati wowote, ni swala la wakati tu. Hivyo hakikisha kuwa BMI yako iko kati 18.5 na 29.
 
kavulata naomba msaada jinsi ya kupangilia mlo kwa mgonjwa wa Kifua Kikuu,nina ndugu yangu namuuguza nnimeambiwa ale zaidi vyakula vya Protein,Carbohydrates na Vitamini,vitu kama maziwa,mayai,maharage na soya visikosekane kwenye mlo wake kwa siku.
 
Pole sana kwa kuuguza, kanuni ni ile ile usichanganye nyama na starch pamoja, usichanganye matunda matamu na matunda machachu pamoja, usichanyanye matunda yenye acidi na matunda yasiyo na acid (alkaline) pamoja. Siku ina masaa 24 hivyo panga masaa ya kula nyama, mayai, maziwa, wali/ugali, matunda na mboga za majani kwa siku. tulisema kuwa ugali/wali/tambi/muhogo vinaweza kuliwa pamoja na mboga za majani, maharagwe, kunde, nyegere, soya, n.k. Nyama inaweza kuliwa pamoja na mboga za majani (kabichi, spinach, mchicha, kachumbali, n.k), maziwa na matunda vitafutiwe muda wake kila kimoja, maji yatafutiwe muda wake wa kunywewa.
 
Asante sana kavulata kwa muongozo,ila kuna mambo mengine ni ngumu kumuongoza mtu mzima na ukizingatia ni mawifi naweza onekana mchoyo bure,ila nitajitahid kadri ya uwezo wangu,asante sana.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom