Kuleta maridhiano na amani CHADEMA, 4rs za Dr. Samia Suluhu Hassan zitumike kutuliza joto la siasa kuelekea uchaguzi wake wa ndani ngazi ya taifa

Kuleta maridhiano na amani CHADEMA, 4rs za Dr. Samia Suluhu Hassan zitumike kutuliza joto la siasa kuelekea uchaguzi wake wa ndani ngazi ya taifa

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Kwa ushahidi wa mahojiano ya viongozi waandamizi wa Chadema Taifa hususani Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti Taifa, ni wazi hekima na busara inahitajika ili kuinusuru Chadema kwenye kupasuka na kwakweli kusambaratika kabisa kwasababu za ubinafsi uliokithiri baina ya viongozi hao, uchu na tamaa ya madaraka wa kupindukia.

Falsafa ya maridhiano ya Dr. Samia Suluhu Hassan, ni hai na inahitajika haraka sana kutuliza joto la kisiasa ndani ya chadema na kuondoa hofu, mashaka na sintofahamu zinazoendelea kuelekea uchaguzi wao wa uongozi wa kitaifa.

4Rs za Dr.Samia Suluhu Hassan, ni wazi zinahitajika sana na haziepukiki chadema, ili hatimae kuiunganisha na kuwaleta pamoja wanachadema, vinginevyo migawanyiko ya wazi inayoonekana, vita ya maneno inayoendelea na uhasama miongoni mwa viongozi waandamizi na wafuasi wao, vinaweza kuudhoofisha spirit ya mapambano ya mageuzi na kuinyong'onyeza chadema na huenda kuifuta kwenye medani ya siasa na kuitoa kabisa kwenye misingi ya kuanzishwa kwake.

Maridhiano ndio haswa dawa na kitulizo pekee cha uhakika cha mawenge yanayo izonga chadema na hali ya kuweweseka kunakoambatana na wimbi la mpasuko kwa sasa 🐒

Mungu Ibarki Tanzania
 
Back
Top Bottom