Kulihusisha tukio la mauaji Kinondoni na vyama vya siasa ni kukosa busara za kisiasa

Kulihusisha tukio la mauaji Kinondoni na vyama vya siasa ni kukosa busara za kisiasa

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2020
Posts
3,315
Reaction score
5,058
Huku sio kuchafuana au kupakana matope bali ni kukosa busara za kisiasa. Maana huwezi kusema kuwa ni Chadema yetu au Ccm yao itachafuka kwa upuuzi wa kutunga mitandaoni.

Hili ni tukio baya la kuterrorise maisha ya watu kama lingekuwa motivated na chama cha siasa asingekwenda mtuhumiwa mmoja pekee. Tungeona makundi ya wafuasi wa vyama vya siasa.

Tuache majungu ya kisiasa yasiyokuwa na tija kwa taifa letu.
 
Tukio la jana ni ugomvi wa kifamilia, CCM baina ya CCM (UVCCM vs POLISISISEMU).

Raia tuliokua tumejificha chini ya seat za ile daladala ndio maana hatukupata maafa yoyote. Jamaa lingeamua kuzimwaga kwenye tank la mafuta ya ile daladala lingetukaanga kama shenene.​

JamiiForums447496613.jpg
 
Wewe mleta mada kama kweli huna nia ya kuingiza siasa kwenye tukio hili kwa nini uzi wako haujaupeleka Jukwaa la Habari Mchanganyiko? Kajiti kakukupaka 'haja' unajisaidia ukiwa umekakanyaga!
 
Tukio la jana ni ugomvi wa kifamilia, CCM baina ya CCM (UVCCM vs POLISISISEMU).

Raia tuliokua tumejificha chini ya seat za ile daladala ndio maana hatukupata maafa yoyote. Jamaa lingeamua kuzimwaga kwenye tank la mafuta ya ile daladala lingetukaanga kama shenene.View attachment 1908854
Kwa uzoefu wetu CCM ni wezi! Sasa katika kufanya ujambazi wao UVCCM na Polisiccm wamedhurumiana wakaishia kutwangana risasi!
 
Huku sio kuchafuana au kupakana matope bali ni kukosa busara za kisiasa. Maana huwezi kusema kuwa ni Chadema yetu au Ccm yao itachafuka kwa upuuzi wa kutunga mitandaoni. Hili ni tukio baya la kuterrorise maisha ya watu kama lingekuwa motivated na chama cha siasa asingekwenda mtuhumiwa mmoja pekee. Tungeona makundi ya wafuasi wa vyama vya siasa. Tuache majungu ya kisiasa yasiyokuwa na tija kwa taifa letu.
Kwa kuwa imewagusa ccm ndio maana mnasema lisihusishwe na vyama vya siasa. Mmesahau kuwa nyie ndio mlianza kwa polisi wenu kuja na picha za bunduki zilizofungwa na bendera ya chadema, visu vyenye rangi ya CUF?
 
Ni Watanzania wangapi walio hudhuria shule na masomo aliyo soma Hamza huko Misri? Hamna shule nyingine zenye masomo hayo huko duniani? Wangapi ambao wako tayari wanasubiria muda ukifika wafanye kama alivyo fanya mwenzao?
 
CCM na mambo ya kitoto, ya kijinga na ya kikatili hawawezekani. Fikiria walikuwa wameshatengeneza kadi ya Chadema na kuanza kudai mtuhumiwa ni Chadema na kumpa jina la gaidi!...
Aisee, kumbe ndivyo mambo yalivyo?

I said it, kwamba, tukio hili lina motivations za kisiasa.

Mlengwa ni CHADEMA.

Wameshaona kabisa kuwa wamekosea kui - design kesi ya ugaidi wa Mbowe ili ku - incriminate CHADEMA na kisha wapate uhalali na sababu za kuifuta.

Sasa wamekuja na tukio hili la kutengeneza ili kujaribu kurekebisha makosa yao na kuipa uhai kesi hii.

Bahati njema ni kuwa, Mungu muumba yuko upande wa umma/CHADEMA...
 
Kada la Lumumba likiwa kazini kutetea chama chake! Nina uhakika, kama huyu Hamza angekuwa CDM basi ungeshiriki hapa kuinanga CDM na hata kumuhusisha Hamza na Mbowe!
 
daaaa tukio la jana hakika halikuwa zuri kwa sura ya kimataifa kwani limetokea kwenye geti la ubalozi wa Ufaransa..ni kama kuna jambo fulani haliko sawa, wajuzi wa intilijensia walifuatilie haraka nchi ipate majibu, chanzo chake,sababu zake, na hitimisho.
 
Back
Top Bottom