Kuliko Bilion 34 kujenga soko Kariakoo bora soko lihamishwe

Naungana na wewe mkuu ,uko sahihi
 
Umesema vitu vya maana sana aseee..tatizo la nchi hii linajulikana sikuzote..ni viongozi wa ccm.

#MaendeleoHayanaChama
 
Una chuki na wamachinga eh!!?

Nchi ni yetu sote, nenda Hong Kong kawaulize wanapumlia wapi halafu uliza maendeleo yao then njoo na porojo zako.
Wale wamefanya hivyo kwa sababu hawana ardhi ya kutosha. Nchi yetu ina ardhi kubwa sana unataka tuige kuishi kwa kusongana? Use your common sense. Hivi kweli ule msongamano wa Hong Kong, watu wanapanda lift kwa foleni ndefu ndiyo unaona ni maendeleo? Waafrika tuna shida gani?
 
Yani tena siyo kigamboni tu, vitongoji vyote vilivyo pembezoni mwa jiji vingejengewa masoko makubwa kama hayo ili kuondoa msongamano katikati ya jiji hao wamachinga wasambazwe huko pembezoni mwa jiji.
Hii iko sawa sana, kipindi cha nyuma nilisikia kulikuwa na mpango wa kujenga soko kubwa la Kinyerezi, naona huo mradi umekufa kabisa.
 
Serikali wafanye mpango wa kujenga masoko makubwa nje ya mji ilinkuounguza msongamano katikati ya jiji.
Maeneo kama Mbagala, Tegetw au Bunju, Kinyerezi, Mbezi Luis.

Nadhani itasaidia hata wafanyabiashara wanaorundikana mjini, watu wengi wanaoenda karikakoo wanaishi nje ya mji.
 
Tuna mchumi namba moja kule jikoni. Anajua kila kitu kinachowafaa watanzania.

Hayakuwa makosa kushauri watu wahame kama hawataki maamuzi fulani.

Kama mazuri vile!!!
 
Una chuki na wamachinga eh!!?

Nchi ni yetu sote, nenda Hong Kong kawaulize wanapumlia wapi halafu uliza maendeleo yao then njoo na porojo zako.
Acheni ujinga lile soko lina muda gani pale mpaka sasa kuna maendeleo gani hadi mfananishe na watu wenye akili

Sent from my CPH2179 using JamiiForums mobile app
 
Wangechukua hiyo 34 wajenge masoko matatu makubwaaaa mapya nje ya mji.
1. Njia ya Bagamoyo (Bunju au mbele zaidi)
2. Njia ya Morogoro (Kibaha au mbele zaidi)
3. Njia ya kuelekea kusini. (Mbagala kwa mbele mbele huko)

Halafu wanakuwa wamejipanga na wanakuwa na ardhi kubwa kama eka 5000 hivi
 
Kabisa yani.
 
Una chuki na wamachinga eh!!?

Nchi ni yetu sote, nenda Hong Kong kawaulize wanapumlia wapi halafu uliza maendeleo yao then njoo na porojo zako.
Hujaelewa logic ya bandiko... Nikuulize swali hiyo pesa ukiamua kujenga masoko matatu ya pembeni huko (kila soko bilioni 11) maana jiji la Dar limepanuka mnoo na ni upuuzi kutaka eti watu milioni karibia nne wawe wanakuja shopping Kariakoo. Sasa je ukijenga masoko matatu ya uhakika huko pembeni utakuwa umewasaidia wamachinga wangapi kulinganisha na soko moja la Kariakoo?? Hii nchi ni kama hakuna city planners at all, pale Dodoma au Morogoro yaani unatumia karibia bilioni 20 kujenga soko moja really??? Badala ya pesa hiyo hiyo kujenga masoko matatu au manne kwenye maeneo ya watu ili watu wapate huduma jirani wewe unalazimisha mtu aende 10km kununua nyanya au vitunguu au shati ya shule ya mtoto.
 
Wewe hongkong hujaona kuna misitu? Wamachinga siyo lazima walundikane sehemu moja k'koo mji umekuwa kuna vitongoji vingi sana vya kuwasambaza hata tegeta, mbezi, kinyerezi, mbagala kuna wamachinga kwani lazima kariakoo?
Exactly eti badala ya kuwa na masoko mazuri hata matano huko waliko watu wewe unataka mtu atoke Tegeta, Tabata, Mbagala eti aje Kariakoo eboo!!
 
Nadhani kitengo husika kipo halimashauri. Maana si wanahusika na mazingira pia?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…