Kuliko Bilion 34 kujenga soko Kariakoo bora soko lihamishwe

Kuliko Bilion 34 kujenga soko Kariakoo bora soko lihamishwe

Ubungo billioni 200 tulipigwa. South Africa walijenga 4 tier interchange kwa $84million, Ghana wamejenga 4tier interchange kwa $94million sis vidaraja viwili billioni mbili[emoji23]. Pale jangwani tukijenga ya kwetu kwenda faya, Magomeni, salender, karume, kinondoni studio haizidi $250 million. Ndege moja ya Dreamliner tumenunua $248 millioni tumeagiza nyingine moja $248 + $248 =$496 millioni tunabeba mizigo guangzhou sasa hv mchina mwenyewe anashangaa Dreamliner pekee la mizigo airport ni la Africa [emoji23].

Labda nikuulize wewe hapo unajiskiaje binafsi kuwa na madege mawili ya $496million au kuwa na madaraja ya yanayoungana kwenda faya, magomeni, salender, karume hadi kinondoni studio ipi itakusaidia wewe binafsi?View attachment 1999160View attachment 1999161
Naungana na wewe mkuu ,uko sahihi
 
Inaonekana watu wa mipango miji wamelala na viongozi wetu akili zimeganda. Nimeona leo kwamba soko la k'koo litajengwa upya kwa Billion 34, leo siyo mwaka 1970 jamani kwanini pesa zote zitumike kujenga soko tena eneo lenye tatizo la msongamano wa watu badala ya kulihamisha soko pembezoni mwa mji? Au wazanzibari wao kila kitu wanataka kiwe karibu na feri ili wakitoka Zanzibar wasipate usumbufu[emoji23]? Maana naskia tena kuna mradi mwingine wa soko la jangwani[emoji26][emoji26].

Mimi nazani tuachane na hili soko la kariakoo tena serikali ingetumia opportunity hii kujenga mradi wa kuwezesha kariakoo kupumua kwa kubomoa lile soko na kupanda miti eneo lile na kutengeneza city park yenye bustani na benchi za watu kupumzika. Itungwe sheria iundwe mamlaka ya City park Authority ya kusimamia mambo haya kwenye miji yetu ipendeze. Tuache fikra kwamba kila eneo lazima lijengwe mji ule hauna hata sehemu ya kupumzika, mtalii akienda k'koo leo hii hakuna hata sehemu ya kupumzika labda ale chips sehemu ambayo imejaa joto la moshi wa jiko la mkaa na hewa ya mafuta ya kukaanga.

Kwanini bado serikali inakaa na kuwaza kujenga jenga sehemu yenye msongamano hata parking za magari hakuna badala ya kujenga miradi ya kuboresha changamoto za mji kama kujenga jengo la parking pale kwenye soko japo mimi ningetamani pasijengwe chochote ipandwe miti tu pale mji upumue.

Leo tunataka kufanya makosa yaleyale ya kujenga mwendokasi jangwani kwa kujenga soko jingine pale la wamachinga badala ya kujenga daraja flyover la kutoka magomeni kwenda faya au interchange ya kutoka magomeni kwenda faya kwenda salender kwenda karume na kupanda miti mirefu ya misitu jangwani ili kusaidia joto la mji kupungua.

Ukizingatia eneo la jangwani ndiyo aneo peke kwenye mji wa dar es salaam lenye unapana wa kutosha ndani ya jiji lenye kutosha kujenga 4 tier interchange ambazo kwa Africa ziko mbili tuu, moja iko Ghana na nyingine iko South Africa.

Yani pale inasukwa interchange moja matata sana kono moja linaenda faya kono jingine linaenda magomeni, kono jingine linasambaa hadi salender , kono jingine linasambaa hadi mitaa ya ilala karume, kono jingine linakatiza hadi kinondoni studio au nyuma yake pale.

Hela tunazo invest kwenye mavitu yasiyo na kichwa (madege, ma dreamliner) tunaweza tukatoa kitu cha maana sana pale jangwani chenye kupunguza changamoto nyingi sana za mji na kutujengea heshima kubwa sana kama jiji.

N:B Yani kwa asiyeelewa umuhimu wa misitu katikati ya mji ni kwamba binadamu tunazalisha kiwango kikubwa sana cha Co2 gases kwa tunavyopumua na moshi wa magari na viwanda, pia majiko tunayopikia ya mkaa sasa jiji linakuwa na hewa chafu sana ya co2 sasa wenzetu kama hongkong wamezungusha misitu kwenye jiji lao ili kuthibiti kiwango kikubwa cha Co2 gases kwa sababu misitu inanyonya gesi za Co2 na ku release gases za Oxygen hivyo kusaidia mji kuwa Na hewa safi na kusaidia ubongo kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Kinyume chake ni sisi hapa.
View attachment 1999008
Umesema vitu vya maana sana aseee..tatizo la nchi hii linajulikana sikuzote..ni viongozi wa ccm.

#MaendeleoHayanaChama
 
Una chuki na wamachinga eh!!?

Nchi ni yetu sote, nenda Hong Kong kawaulize wanapumlia wapi halafu uliza maendeleo yao then njoo na porojo zako.
Wale wamefanya hivyo kwa sababu hawana ardhi ya kutosha. Nchi yetu ina ardhi kubwa sana unataka tuige kuishi kwa kusongana? Use your common sense. Hivi kweli ule msongamano wa Hong Kong, watu wanapanda lift kwa foleni ndefu ndiyo unaona ni maendeleo? Waafrika tuna shida gani?
 
Yani tena siyo kigamboni tu, vitongoji vyote vilivyo pembezoni mwa jiji vingejengewa masoko makubwa kama hayo ili kuondoa msongamano katikati ya jiji hao wamachinga wasambazwe huko pembezoni mwa jiji.
Hii iko sawa sana, kipindi cha nyuma nilisikia kulikuwa na mpango wa kujenga soko kubwa la Kinyerezi, naona huo mradi umekufa kabisa.
 
Serikali wafanye mpango wa kujenga masoko makubwa nje ya mji ilinkuounguza msongamano katikati ya jiji.
Maeneo kama Mbagala, Tegetw au Bunju, Kinyerezi, Mbezi Luis.

Nadhani itasaidia hata wafanyabiashara wanaorundikana mjini, watu wengi wanaoenda karikakoo wanaishi nje ya mji.
 
Leo tunataka kufanya makosa yaleyale ya kujenga mwendokasi jangwani kwa kujenga soko jingine pale la wamachinga badala ya kujenga daraja flyover la kutoka magomeni kwenda faya au interchange ya kutoka magomeni kwenda faya kwenda salender kwenda karume na kupanda miti mirefu ya misitu jangwani ili kusaidia jo
Tuna mchumi namba moja kule jikoni. Anajua kila kitu kinachowafaa watanzania.

Hayakuwa makosa kushauri watu wahame kama hawataki maamuzi fulani.

Kama mazuri vile!!!
 
Una chuki na wamachinga eh!!?

Nchi ni yetu sote, nenda Hong Kong kawaulize wanapumlia wapi halafu uliza maendeleo yao then njoo na porojo zako.
Acheni ujinga lile soko lina muda gani pale mpaka sasa kuna maendeleo gani hadi mfananishe na watu wenye akili

Sent from my CPH2179 using JamiiForums mobile app
 
Wangechukua hiyo 34 wajenge masoko matatu makubwaaaa mapya nje ya mji.
1. Njia ya Bagamoyo (Bunju au mbele zaidi)
2. Njia ya Morogoro (Kibaha au mbele zaidi)
3. Njia ya kuelekea kusini. (Mbagala kwa mbele mbele huko)

Halafu wanakuwa wamejipanga na wanakuwa na ardhi kubwa kama eka 5000 hivi
 
Wangechukua hiyo 34 wajenge masoko matatu makubwaaaa mapya nje ya mji.
1. Njia ya Bagamoyo (Bunju au mbele zaidi)
2. Njia ya Morogoro (Kibaha au mbele zaidi)
3. Njia ya kuelekea kusini. (Mbagala kwa mbele mbele huko)

Halafu wanakuwa wamejipanga na wanakuwa na ardhi kubwa kama eka 5000 hivi
Kabisa yani.
 
Una chuki na wamachinga eh!!?

Nchi ni yetu sote, nenda Hong Kong kawaulize wanapumlia wapi halafu uliza maendeleo yao then njoo na porojo zako.
Hujaelewa logic ya bandiko... Nikuulize swali hiyo pesa ukiamua kujenga masoko matatu ya pembeni huko (kila soko bilioni 11) maana jiji la Dar limepanuka mnoo na ni upuuzi kutaka eti watu milioni karibia nne wawe wanakuja shopping Kariakoo. Sasa je ukijenga masoko matatu ya uhakika huko pembeni utakuwa umewasaidia wamachinga wangapi kulinganisha na soko moja la Kariakoo?? Hii nchi ni kama hakuna city planners at all, pale Dodoma au Morogoro yaani unatumia karibia bilioni 20 kujenga soko moja really??? Badala ya pesa hiyo hiyo kujenga masoko matatu au manne kwenye maeneo ya watu ili watu wapate huduma jirani wewe unalazimisha mtu aende 10km kununua nyanya au vitunguu au shati ya shule ya mtoto.
 
Wewe hongkong hujaona kuna misitu? Wamachinga siyo lazima walundikane sehemu moja k'koo mji umekuwa kuna vitongoji vingi sana vya kuwasambaza hata tegeta, mbezi, kinyerezi, mbagala kuna wamachinga kwani lazima kariakoo?
Exactly eti badala ya kuwa na masoko mazuri hata matano huko waliko watu wewe unataka mtu atoke Tegeta, Tabata, Mbagala eti aje Kariakoo eboo!!
 
Umeongea vizuri kuhusu Sustainable Cities, ila nimejaribu ku google kama kuna mamlaka yoyote inayoshughulikia mambo hayo hakuna. Kwenye miji iliyoendelea kila mji una mamlaka ya kushughulikia na green cities (City Park Authorities). Uki google Mamlaka kama hizo Tanzania utakutana na Hamidu city park[emoji23].View attachment 1999030
Nadhani kitengo husika kipo halimashauri. Maana si wanahusika na mazingira pia?!
 
Back
Top Bottom