Kulikoni upatikanaji wa dawa katika hospitali za umma?

Kulikoni upatikanaji wa dawa katika hospitali za umma?

Hivi hata ungekuwa wewe , ushatukanwa miaka 6 , na tena bila kuongezwa hata sentano kipande ungepata wapi morali wa kazi ?
 
Pale Muhimbili kule kwenye wagonjwa wa akili,dawa zote zilikuwa wanapewa bure,alipoingia Jiwe akafuta ule utaratibu,ikawa sasa dawa za kulipia,harafu ilikuwa ghafra...jinsi wagonjwa walivyokuwa wanalalamika simanzi tupu.
 
Pale Muhimbili kule kwenye wagonjwa wa akili,dawa zote zilikuwa wanapewa bure,alipoingia Jiwe akafuta ule utaratibu,ikawa sasa dawa za kulipia,harafu ilikuwa ghafra...jinsi wagonjwa walivyokuwa wanalalamika simanzi tupu.
Duuuhh, hadi kichaa alipie dawa. Kazi ipo
 
Serikali inakosea kuajiri watumishi wa uma wa pamanent.
Ilitakiwa iwaajiri kwa mikataba maarum km jeshi la police ili iwe rahis ku- fire.
 
Ni hivi majuzi, katika ukumbi wa MAELEZO, tumetangaziwa kuwa Serikali ya Rais Samia imetoa TZS 57 Billion katika robo ya kwanza ya mwaka 2022/23 kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba katika hospitali na vituo vya afya vya Umma. Kwa hakika hicho ni kiasi kikubwa na cha kutosha ili kuhakikisha upatikanaji wa dawa za kutosha.

Hata hivyo, hali ya upatikanaji wa dawa katika Hospitali na vituo vya afya vya umma inazidi kuwa mbaya. Hali hii inatokana na utendaji mbovu(Poor Perfornance) ya Uongozi wa MSD kuliko hata kipindi cha uongozi wa Afande General Mhidze au wakati wa Laurean Bwanakunu.

Hospitali na vituo vya afya vya umma ndio tegemeo kubwa la watanzania masikini ambao hawawezi kumudu gharama za tiba katika vituo binafsi na utendaji mbovu wa MSD ndo unachangia hali mbaya ya upatikanaji wa dawa katika vituo vya afya vya umma, kwa kuanzia nitagusia maeneo machache yafuatayo ambayo aidha kwa makusudi au kwa sababu ya uwezo mdogo wa Mkurugenzi Mkuu Mr Tukai Mavere, Rais Samia anahujumiwa kama ifuatavyo:

1. KUCHELEWA KWA MAAMUZI HAPO MSD KUTOKANA NA KUKOSEKANA KWA SAFU YA UONGOZI
Maamuzi muhimu hapa MSD yanafanywa na mtu Mmoja(ONE MAN SHOW) Mkurugenzi Mkuu Mr. Tukai Mavere hivyo kuchelewesha maamuzi muhimu ambayo yanapelekea ucheleweshaji wa decisions ikiwemo kusainiwa kwa mikataba ya manunuzi ya dawa.

Mr. Mavere tangu aingie ofisini amekuwa kiguu na njia yupo safarini huku akitembea na ofisi bila kukaimisha mtu yeyote, kwa sababu anazozijua yeye pengine kutoamini safu ya uongozi imayokaimu nafasi mbalimbali za ukurugenzi.

Hiyo ni kinyume na sheria na kanuni za utumishi wa umma ambapo kiongozi hatakiwi ku-personalize ofisi za umma pengine hii inatokana na ukweli kwamba Mkurugenzi Mkuu Mr. Mavere ametokea kwenye ka-NGO ka watu wachache na hana uzoefu na Corporate au Public Management, lkn anapaswa kujifunza.

KIBAYA ZAIDI, NAFASI ZA WAKURUGENZI ZIMETANGAZWA KUPITIA MCHAKATO WA SEKRETARIAT YA UTUMISHI WA UMMA(PSRS) tangu July-2022 lakini hadi leo hakuna kinachoendelea. Kuna Tetesi kuwa Mr. Mavere anafanya juhudi ku-frustrate mchakato huo ili alete washikaji zake kupitia dirrisha dogo baada ya kuona vigezo vya PSRS vinawatema. PSRS ni Taasisi inayoheshimika ya umma hivyo inatakiwa kukamilisha mchakato huo kwa wakati bila kubugudhiwa.

MY TAKE: Niliwahi kushauri huko nyuma kuwa zoezi la ku-overhaul MSD ilikuwa ni order ya Rais which is good as PRESIDENTIAL DECREE hivyo si vema akaachiwa Mr. Mavere peke yake ku-impliment order hiyo kwani angeishia kuleta washikaji zao kitu ambacho kinaendelea sasa hivi hapo MSD.

NASHAURI TENA SERIKALI KUPITIA CHIEF SECRETARY ISIMAMIE UPATIKANAJI WA WAKURUGENZI KWA HARAKA NA KWA UWAZI KUPITIA PSRS. Cha kushangaza, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alitoa deadline ya 30th September, 2022 MSD iwe imepata safu mpya ya uongozi, lakini Mr Mavere hajali na hiyo nadhani it amounts to insubordination ya waziri Ummy

2. KUTELEKEZWA KWA KIWANDA CHA UZALISHAJI DAWA HUKO IDOFI-NJOMBE IRINGA:
Pamoja na mapungufu ya DG aliyepita wa MSD Major General Mhidize ,bado alikuwa na maono ya kuanzisha kiwanda cha kutengeneneza dawa ili kujazia pengo la upatikanaji wa dawa kutoka nje ya nchi ambapo mlolongo wake ni mrefu sana.

Hata hivyo, uendelezaji wa kiwanda hicho kilichokuwa kimefikia hatua ya kuanza uzalishaji umekuwa frustrated na uongozi wa Mr. Mavere na Mashine zinaishia kupata kutu na hivyo huenda serikali ikaingia hasara kubwa kutokana na uwekezaji mkubwa uliokwisha fanya na serikali eneo hilo.

MY TAKE: Nashauri serikali kupitia wizara ya afya, isimamie kuhakikisha kiwanda hicho kinaanza kufanya kazi ili kupunguza ukosefu wa dawa katika Hospitali na vituo vya afya vya umma

3.TEUZI NA TRANSFERS ZISIZO NA TIJA ZINAZOFANYWA NA MR. MAVERE:
Tangu ameshika hatamu hapo MSD, Mr Mavere amekuwa akifanya teuzi na staff transfers ambazo zinazingatia ushikaji na hazina tija kwa MSD na kwa mustakabali wa upatikanaji wa dawa kwa Taifa kupitia utendaji wa MSD. Eneo korofi ni eneo lolote linalogusa manunuzi kwani inaonekana amapania kuweka washikaji ili aweze kupiga dili zake vizuri kupitia manunuzi, nitatoa mifano michache kama ifuatavyo:

(a) Alimteua Mr. Mkama Mbuguma kukaimu nafasi ya Ukurugenzi wa Manunuzi ilihali akijua ni very junior na incompetent. Hapa JF, tulishauri kuwa hapo amekosea lakini akatupuuza na tukaonekana tunapiga fitna kilicho kuja kutokea ni aibu.

Kwani alitaka kumtumia Mr. Mkama kutoa tenda ya 10 Billion kwa mtu ambaye hakushinda tenda na wala hakupitishwa na tenda bodi, kinyume na Sheria na Kanuni za Manunuzi ya Umma (Public Procurement Act and Regulations) kupitia fake and unprocedural negotiations ambapo iliishia PCCB na hatimaye Mamlaka ya rufaa za Zabuni PAA (Procuremen Appeals Authority) ikatengua maamuzi feki ya Mr. Mavere na wapambe wake.

Baada ya kuona ameangukia pua, ndo akatoka usingizi akamtoa Mr. Mkama Mbuguma kwa kuchelewa na kaleta mwingine kukaimu ukurugenzi wa manunuzi ambaye nae hana uwezo kama Mkama yupo very slow and indecisive. As a well wisher, Nakushauri tena Mr. Mavere hakikisha unapata competent Director wa Procurement kupitia njia za wazi huko PSRS kuliko unavyozunguka zunguka ku-frustrate process ya recruitment ya directors

b) Kwa hasira baada ya kuona mpango wake wa kuwapa tenda washikaji zake umeshindwa hapo (a) juu, kamuhamishia nje ya taasisi Mr. Frankie Nkone aliyekuwa Mwenyekiti wa Tender Board ili amuweke Mshikaji wake MR Michael Bajile - Kaimu Meneja wa Maoteo (Quantification) ambaye ameingizwa MSD kimichongo hivi karibuni kutoka kwenye NGO na ni junior na hata uzoefu wowote na Public Procurement.

Amefanya uteuzi huo wa mwenyekiti wa MSD Tender Board bila kujali kuwa hapo kuna mgongano wa masilahi(Conflict of Interest) kwani Mr. Michael Bajile ndio anaanzisha mchakato wa manunuzi (Quantification) halafu yeye mwenyewe anahamia upande wa pili wa Tender Board kama Mwenyekiti anaenda tena kupitisha Manunuzi hivyo ku-defeat dhana nzima ya administrative control ya internal check and balance katika utumishi wa umma.

Pamoja na Mr. Mavere kuweka pandakizi lake ili apate mteremko asipatwe tena na kadhia ya procurement iliyokumkuta majuzi ya PAA, nashauri TAKUKURU watupie macho jambo hilo kabla mambo hayajaharibika zaidi. Besides, Kuna taarifa kuwa hata Kaimu Mwanasheria wa MSD (Ag.Legal Counsel) yupo mbioni kuondolewa baada ya kuonekana yupo strict na ni mwiba mchungu kwa Mr. Mavere ambaye anataka tenda zitolewe kwa matakwa yake na genge lake.

MY TAKE: Kutokana na mifano hiyo hapo juu, Chief Secretary na Waziri Ummy na watendaji wako wa wizara ya Afya mnashauriwa ku-exercise your oversight role ili kuhakikisha MSD inarudi katika ubora wake na siyo kuzidi kutumbukia shimoni kwa sababu ya vitendo vya mtu mmoja (One Man Show acts).

To the expense of watanzania wengi ambao ni masikini na wanaotegemea MSD katika upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma za afya katika hospitali na vituo vya afya vya umma. Hiyo kazi siyo lazima ifanywe na His Excellency SAMIA SULUHU HASSAN, tumuachie yeye a-deal na matatizo makubwa ya upatikanaji wa Maji na Umeme na mengineyo, yeye alishafanya kazi yake ya kuhakikisha MSD inapata pesa kutokana na budget iliyopangiwa.

Nawasilisha
 
Sasa wewe mwenyewe umetoa sababu tena unasema Rais anahujumiwa tushike lipi?

Ukimteua mtu lazima umueleze nini unataka afanye akishindwa apishe..

Waziri wa Afya yupo na Bodi ya MSD wapo wao wamechukua hatua gani?
 
Sasa wewe mwenyewe umetoa sababu tena unasema Rais anahujumiwa tushike lipi?

Ukimteua mtu lazima umueleze nini unataka afanye akishindwa apishe..

Waziri wa Afya yupo na Bodi ya MSD wapo wao wamechukua hatua gani?
asante kwa kuunga mkono hoja ya mtoa mada,Waziri wa Afya na Bodi ya MSD wachukue hatua,otherwise is good as hujuma kwa Rais SAMIA, serikali yake imetoa TZS Billion 57 lakini watu wanashangaa tu.Wanachi hatutakiwi kukerwa na Mpira tu kama mechi ya Jana ya Yanga Vs Club African,bali tuangalie na mambo ya msingi kama haya yenye kuhusu mustakabali wa afya za watanzania
 
Ni hivi majuzi, katika ukumbi wa MAELEZO, tumetangaziwa kuwa Serikali ya Rais Samia imetoa TZS 57 Billion katika robo ya kwanza ya mwaka 2022/23 kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba katika hospitali na vituo vya afya vya Umma.Kwa hakika hicho ni kiasi kikubwa na cha kutosha ili kuhakikisha upatikanaji wa dawa za kutosha.

Hata hivyo, hali ya upatikanaji wa dawa katika Hospitali na vituo vya afya vya umma inazidi kuwa mbaya. Hali hii inatokana na utendaji mbovu(Poor Perfornance) ya Uongozi wa MSD kuliko hata kipindi cha uongozi wa Afande General Mhidze au wakati wa Laurean Bwanakunu. Hospitali na vituo vya afya vya umma ndo tegemeo kubwa la watanzania masikini ambao hawawezi kumudu gharama za tiba katika vituo binafsi na utendaji mbovu wa MSD ndo unachangia hali mbaya ya upatikanaji wa dawa katika vituo vya afya vya umma, kwa kuanzia nitagusia maeneo machache yafuatayo ambayo aidha kwa makusudi au kwa sababu ya uwezo mdogo wa Mkurugenzi Mkuu Mr Tukai Mavere, Rais Samia anahujumiwa kama ifuatavyo:

1. KUCHELEWA KWA MAAMUZI HAPO MSD KUTOKANA NA KUKOSEKANA KWA SAFU YA UONGOZI
Maamuzi muhimu hapa MSD yanafanywa na mtu Mmoja(ONE MAN SHOW) Mkurugenzi Mkuu Mr.Tukai Mavere hivyo kuchelewesha maamuzi muhimu ambayo yanapelekea ucheleweshaji wa decisions ikiwemo kusainiwa kwa mikataba ya manunuzi ya dawa. Mr.Mavere tangu aingie ofisini amekuwa kiguu na njia yupo safarini huku akitembea na ofisi bila kukaimisha mtu yeyote, kwa sababu anazozijua yeye pengine kutoamini safu ya uongozi imayokaimu nafasi mbalimbali za ukurugenzi. Hiyo ni kinyume na sheria na kanuni za utumishi wa umma ambapo kiongozi hatakiwi ku-personalize ofisi za umma pengine hii inatokana na ukweli kwamba Mkurugenzi Mkuu Mr. Mavere ametokea kwenye ka-NGO ka watu wachache na hana uzoefu na Corporate au Public Management, lkn anapaswa kujifunza.

KIBAYA ZAIDI, NAFASI ZA WAKURUGENZI ZIMETANGAZWA KUPITIA MCHAKATO WA SEKRETARIAT YA UTUMISHI WA UMMA(PSRS) tangu July-2022 lakini hadi leo hakuna kinachoendelea.Kuna Tetesi kuwa Mr.Mavere anafanya juhudi ku-frustrate mchakato huo ili alete washikaji zake kupitia dirrisha dogo baada ya kuona vigezo vya PSRS vinawatema.PSRS ni Taasisi inayoheshimika ya umma hivyo inatakiwa kukamilisha mchakato huo kwa wakati bila kubugudhiwa .

MY TAKE: Niliwahi kushauri huko nyuma kuwa zoezi la ku-overhaul MSD ilikuwa ni order ya Rais which is good as PRESIDENTIAL DECREE hivyo si vema akaachiwa Mr.Mavere peke yake ku-impliment order hiyo kwani angeishia kuleta washikaji zao kitu ambacho kinaendelea sasa hivi hapo MSD. NASHAURI TENA SERIKALI KUPITIA CHIEF SECRETARY ISIMAMIE UPATIKANAJI WA WAKURUGENZI KWA HARAKA NA KWA UWAZI KUPITIA PSRS. Cha kushangaza, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alitoa deadline ya 30th September, 2022 MSD iwe imepata safu mpya ya uongozi,lakini Mr Mavere hajali na hiyo nadhani it amounts to insubordination ya waziri Ummy

2. KUTELEKEZWA KWA KIWANDA CHA UZALISHAJI DAWA HUKO IDOFI-NJOMBE IRINGA:
Pamoja na mapungufu ya DG aliyepita wa MSD Major General Mhidize ,bado alikuwa na maono ya kuanzisha kiwanda cha kutengeneneza dawa ili kujazia pengo la upatikanaji wa dawa kutoka nje ya nchi ambapo mlolongo wake ni mrefu sana.Hata hivyo,uendelezaji wa kiwanda hicho kilichokuwa kimefikia hatua ya kuanza uzalishaji umekuwa frustrated na uongozi wa Mr.Mavere na Mashine zinaishia kupata kutu na hivyo huenda serikali ikaingia hasara kubwa kutokana na uwekezaji mkubwa uliokwisha fanya na serikali eneo hilo.
MY TAKE:Nashauri serikali kupitia wizara ya afya,isimamie kuhakikisha kiwanda hicho kinaanza kufanya kazi ili kupunguza ukosefu wa dawa katika Hospitali na vituo vya afya vya umma

3.TEUZI NA TRANSFERS ZISIZO NA TIJA ZINAZOFANYWA NA MR. MAVERE:
Tangu ameshika hatamu hapo MSD,Mr Mavere amekuwa akifanya teuzi na staff transfers ambazo zinazingatia ushikaji na hazina tija kwa MSD na kwa mustakabali wa upatikanaji wa dawa kwa Taifa kupitia utendaji wa MSD.Eneo korofi ni eneo lolote linalogusa manunuzi kwani inaonekana amapania kuweka washikaji ili aweze kupiga dili zake vizuri kupitia manunuzi,nitatoa mifano michache kama ifuatavyo:

(a) Alimteua Mr.Mkama Mbuguma kukaimu nafasi ya Ukurugenzi wa Manunuzi ilihali akijua ni very junior na incompetent.Hapa JF,tulishauri kuwa hapo amekosea lakini akatupuuza na tukaonekana tunapiga fitna.kilicho kuja kutokea ni aibu kwani alitaka kumtumia Mr. Mkama kutoa tenda ya 10 Billion kwa mtu ambaye hakushinda tenda na wala hakupitishwa na tenda bodi, kinyume na Sheria na Kanuni za Manunuzi ya Umma (Public Procurement Act and Regulations) kupitia fake and unprocedural negotiations ambapo iliishia PCCB na hatimaye Mamlaka ya rufaa za Zabuni (PAA(Procuremen Appeals Authority) ikatengua Maamuzi feki ya Mr.Mavere na wapambe wake. Baada ya kuona ameangukia pua, ndo akatoka usingizi akamtoa Mr.Mkama Mbuguma kwa kuchelewa na kaleta mwingine kukaimu ukurugenzi wa manunuzi ambaye nae hana uwezo kama Mkama yupo very slow and indecisive. As a well wisher,Nakushauri tena Mr. Mavere hakikisha unapata competent Director wa Procurement kupitia njia za wazi huko PSRS kuliko unavyozunguka zunguka ku-frustrate process ya recruitment ya directors

b)Kwa hasira baada ya kuona mpango wake wa kuwapa tenda washikaji zake umeshindwa hapo (a) juu,kamuhamishia nje ya taasisi Mr.Frankie Nkone aliyekuwa Mwenyekiti wa Tender Board ili amuweke Mshikaji wake MR Michael Bajile -Kaimu Meneja wa Maoteo(Quantification) ambaye ameingizwa MSD kimichongo hivi karibuni kutoka kwenye NGO na ni junior na hata uzoefu wowote na Public Procurement.Amefanya uteuzi huo wa mwenyekiti wa MSD Tender Board bila kujali kuwa hapo kuna mgongano wa masilahi(Conflict of Interest) kwani Mr.Michael Bajile ndio anaanzisha mchakato wa manunuzi(Quantification) halafu yeye mwenyewe anahamia upande wa pili wa Tender Board kama Mwenyekiti anaenda tena kupitisha Manunuzi hivyo ku-defeat dhana nzima ya administrative control ya internal check and balance katika utumishi wa umma.Pamoja na Mr. Mavere kuweka pandakizi lake ili apate mteremko asipatwe tena na kadhia ya procurement iliyokumkuta majuzi ya PAA, nashauri TAKUKURU watupie macho jambo hilo kabla mambo hayajaharibika zaidi.Besides,Kuna taarifa kuwa hata Kaimu Mwanasheria wa MSD (Ag.Legal Counsel) yupo mbioni kuondolewa baada ya kuonekana yupo strict na ni mwiba mchungu kwa Mr.Mavere ambaye anataka tenda zitolewe kwa matakwa yake na genge lake.

MY TAKE: Kutokana na mifano hiyo hapo juu,Chief Secretary na Waziri Ummy na watendaji wako wa wizara ya Afya mnashauriwa ku-exercise your oversight role ili kuhakikisha MSD inarudi katika ubora wake na siyo kuzidi kutumbukia shimoni kwa sababu ya vitendo vya mtu mmoja(One Man Show acts). To the expense of watanzania wengi ambao ni masikini na wanaotegemea MSD katika upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma za afya katika hospitali na vituo vya afya vya umma. Hiyo kazi siyo lazima ifanywe na His Excellency SAMIA SULUHU HASSAN, tumuachie yeye a-deal na matatizo makubwa ya upatikanaji wa Maji na Umeme na mengineyo,yeye alishafanya kazi yake ya kuhakikisha MSD inapata pesa kutokana na budget iliyopangiwa.

Nawasilisha
Kwa uzoefu wangu nikihudumu katika idara ya AFYA DAWA HAZIJAWAHI KUTOSHA WALA KUFIKA KWA WAKATI . NIPO TAYARI KUTHIBITISHA
 
Sasa wewe mwenyewe umetoa sababu tena unasema Rais anahujumiwa tushike lipi?

Ukimteua mtu lazima umueleze nini unataka afanye akishindwa apishe..

Waziri wa Afya yupo na Bodi ya MSD wapo wao wamechukua hatua gani?
Acha upumbavu,mwambie January Makamba apishe,kachemka nishati
 
Hii nchi ujanja ujanja mwingi sana..ukute huyu mkurugenzi naye yuko under frustration kutoka kwa hao hao wanasiasa wapiga dili.

#MaendeleoHayanaChama
 
Enzi za wauguzi kuingia shift ukiwa na "mobile pharmacy" zimerudi! Unaingia kazini ukiwa na dawa, iv fluid, giving set, cannula, nk mgonjwa anaandikiwa dawa akienda dirisha la dawa hata Panadol hakuna, unamuita pembeni unamruuzia dawa na bonus ya kumuhudumia mgonjwa wake!

Hawa wenzetu wa kanda ya pwani wanakujaga na neema kwa watumishi: Mwinyi Ruksa, Kikwete, na sasa Samia.
 
Acha majungu. I presume you are one of the beneficiary of the old system
 
Acha majungu. I presume you are one of the beneficiary of the old system
Mkuu au unataka na ushaidi wa picha kabisa...inaonekana wewe unatibiwa Kairuki...
Siku hizi umeishasikia tena wamiliki wa hospital binafsi hasa za DINI wanalalamikia gharama za uendeshaji?
 
Itakuwa vizuri ukitoa evidence hiyo ya picture. Unauliza ili iweje?
 
watalalamikaje wakati vituo vya afya vya umma vimechoka na wachache wenye uwezo wanakimbilia private hospitals,kwa sababu ya vitu vichache kama incompetence ya uongozi wa MSD wa sasa unaosababisha ARTIFICIAL SHORTAGE ya madawa,wakati Serikali ya mama Samia ilishatoa pesa kibao
 
Enzi za wauguzi kuingia shift ukiwa na "mobile pharmacy" zimerudi! Unaingia kazini ukiwa na dawa, iv fluid, giving set, cannula, nk mgonjwa anaandikiwa dawa akienda dirisha la dawa hata Panadol hakuna, unamuita pembeni unamruuzia dawa na bonus ya kumuhudumia mgonjwa wake!

Hawa wenzetu wa kanda ya pwani wanakujaga na neema kwa watumishi: Mwinyi Ruksa, Kikwete, na sasa Samia.
Samia kafanya kazi yake,kama Rais kahakikisha pesa ya kutosha ya kununulia dawa imepelekwa MSD.Hizo so called 'mobile pharmacy' zinachangiwa na uzembe na kukosa weledi kwa baadhi ya watendaji ambao implied wanamuhujumu huku wakijua muda wa maandalizi ya uchaguzi mkuu wa 2025 ni sasa,hii haikubaliki
 
Back
Top Bottom