Kulikoni upatikanaji wa dawa katika hospitali za umma?

Miaka kadhaa iliyopita changamoto ilikuwa serikali haijapeleka fedha stahiki MSD. Serikali ilikuwa na deni kubwa sana ambalo - ilitakiwa kulilipa ili MSD iweze kuwa na fedha za kutosheleza uhitaji/maoteo ya vituo vya tiba

pamoja na deni, kulikuwa na ucheleweshaji wa kutume fedha kutoka serikali kwenda MSD

Mavere ana kazi kubwa sana, utokapo sekta binafsi kwenda serikali, yabidi uwajengee hamasa unaowaongoza ili waendane na kasi yako unayoiwaza, endapo hawatafwatana na wewe (team work) lazima mfumo ukwame.
 
Mbona mtangulizi wake hakihujumiwa?
 
Si kuna viongozi wa MSD wapya wametuliwa hata mwezi ofisini hawajamaliza, hapana bana - yawezekana dawa zenyewe haziko tu.
 
mavere kapewa msd ambayo haina pesa,msd hawajalipwa madeni yake sawia na serikali, bado ina madeni makubwa mzigo mkubwa, hata hicho kiwanda pesa ya kuendesha hazipo, hazina wakichukue kiwanda. serikali waewe serious waache siasa za kufukuzafukuza msd, bodi ya msd na waziri ummy wekeni wazi mzigo wa msd ili ile taasisi ipewe fedha za kujiendesha
 
uongozi wa MSD, laana ya Eric Mapunda itawasumbua sana.
 

Rudi kwenye details za Mleta Mada usimtetee Mr Mavere hata kwenye mambo yaliyoko wazi,Je kushindwa kupanga safu ya Uongozi kwa kukamilisha RECRUITMENT YA DIRECTORS nayo inatokana na ukosefu wa pesa? katangaza mwenyewe and it is on record pale MAELEZO kuwa MSD imepewe TZS Billion 57 za kununulia dawa,Je hiyo TZS 57 itanunuaje dawa bila mikataba(Procurement Contracts) kusainiwa kwa wakati,wakati mwenyewe Mavere ni kiguu na njia na ofisi anatembea nayo,pathetic
 
uongozi wa MSD, laana ya Eric Mapunda itawasumbua sana.
hakuna cha laana wala nini, bodi mpya wawe wazi msd hali yake mbaya, mzigo wa madeni wa miaka mingi walipwe wapewe mtaji wa kujiendesha kihalisia
 

Wewe na Mtoa mada mtakuwa mmekosa nafasi. Hasira unazileta JamiiForums.
Narudia tena MSD inakwama kwa majungu. Badala ya kufanya kazi mnaleta majungu mitandaoni. Kwenye kila Uongozi kuna watu kama nyie mnakuja kuleta majungu na haya mambo yanaanzia ngazi za juu.
MSD ni taasisi hopeless na sio sehemu sahihi ya kukuza utaalam, ni majungu na tamaa ya vyeo, mkikosa mnakuja mitandaoni. Ishu ya Rushwa kuna vyombo husika.kama kweli anakula rushwa pelekeni tuhuma pccb, rushwa ipo mpaka magogoni , wewe unashangaa msd , rushwa ipo mpaka TAKUKURU, Wewe unashangaa msd . Fanya kazi acheni umbea watu wa msd. Matatizo yenu hayatoweza kwisha. Kwa miaka 3 mmeshabadili ma dg wengi , na kila kiongozi anakuja timu yake anayoiamini. Mbona hiz mambo hatusikii huko Ewura, TCRA ,
Hata mwaka bado mmeshaanza kumnanga kiongozi wenu. msd ni kama wana wa Israel, wanavitimbi na hila kila kukicha na kazi hawafanyi. Kazi yenu ni majungu na umbea na cheo fulan kapewa nani . CEO wabaini hawa watu haraka na uwapeleke nje ya miji wakafanye kazi. Hawa ni watu wako wa ndani na ni sabotage ya chini chini
 

Hao watu uliowataja kama wanavigezo kwanin wasipewe hizo nafasi? Hapo ndio unaonesha ulizitaka Wewe
 

Halafu Sekretariati ya ajira ni independent entity, CEO wa taasisi fulan hana uwezo wa kuingililia majukumu ya taasis nyingine . Wewe labda umekosa cheo
 
Jibu hoja za mleta mada,JF siyo sehemu ya mipasho.l
Ndugu punguza jazba kunywa maji kwanza kama una kiu,hapa JF hoja hujibiwa kwa hoja na siyo kuleta mipasho.Nakukumbusha kuwa mnamo tarehe 17th April,2022 ,ukiwa chawa wa mavere ulikuja na uzi wenye title 'Rais Samia amegeuza upepo wa MSD kwa kumteua Mavere Tukai' siye tulikuonya kuwa acha uchawa na usimpe kichwa kwa sifa za kijinga lkn hukutuelewa lakini leo facts zinawekwa mezani unakuja na mipasho baada ya kupanick.Kwa taarifa yako,JF ndo forum sahihi kwa whistle blowers kama sisi wenye nia ya dhati ya kufichua makando kando mbalimbali. Labda nikukumbushe hoja za mleta mada ambazo unatakiwa kuzijibu kwa facts/evidence na siyo kuleta mipasho na mere bare words.Hoja ni kama zifuatazo:
  1. Je Mkurugenzi wa MSD Mr.Mavere hakutangazia Taifa pale MAELEZO kuwa serikali ya SAMIA imeipatia MSD pesa yote ya robo ya kwanza 2022/23 kiasi cha TZS 57 Billion kwa ajili ya manunuzi ya dawa?
  2. Je hakuna uhaba mkubwa wa dawa katika hospitali na vituo vya Afya vya Umma?
  3. Je MSD kwa sasa ina safu ya uongozi(Menejimenti team) au inaendeshwa na mtu Mmoja(One Man Show) mkurugenzi Mkuu Mr.Mavere ambaye muda mwingi yupo safarini huku akitembea na ofisi bila kufanya juhudi za dhati kuhakikisha zoezi la RECRUITMENT OF MSD DIRECTORS linakamilika ili kutii agizo la Waziri Ummy ambae alitoa deadline ya 30th September,2022 MSD iwe imepata safu mpya ya uongozi,Je deadline hiyo ya Ummy kaileta mleta mada au ni ya kweli?Je huoni kuwa kutokuwa na safu kamili ya uongozi inachelewesha maamuzi haswaa ya manunuzi na usambazaji wa dawa na vifaa tiba? Je kudharau agizo la Waziri Ummy hiyo siyo Insubordination kwa waziri huyo?
  4. Je Mchakato wa manunuzi ya vitendanishi ambao ulipigwa chini na mamlaka ya rufaa ya zabuni za umma(PAA-Public Procurement Appeals Authority) haukutokana na kukosa weledi kwa Mavere na kushauriwa vibaya na Mr.Mkama Mbuguma mtu aliyemteua ilihali akijua hana competency,kama anaona anafaa kwanini amemuondoa baada ya kuangukia Pua huko PAA?
  5. Je kitendo cha Mr.Mavere Kumteua Mr.Michael Bajile -Ag.Manager wa Maoteo(Quantification Manager) kuwa mwenyekiti wa MSD Tender Board,ili aka-approve manunuzi ambaya katengeneza requistion mwenyewe kama user.Je huoni hiyo inaleta mgongano wa masilahi(Conflict of interest) na ndo chanzo cha rushwa?
 
Halafu Sekretariati ya ajira ni independent entity, CEO wa taasisi fulan hana uwezo wa kuingililia majukumu ya taasis nyingine . Wewe labda umekosa cheo
Mimi sihitaji cheo MSD,jikite kwenye hoja
 
Hao watu uliowataja kama wanavigezo kwanin wasipewe hizo nafasi? Hapo ndio unaonesha ulizitaka Wewe
hawakuwa na vigezo na weledi ,ndio maana wamepelekea kumshauri vibaya akaenda kuangukia pua huko PAA.Hata kama wewe ni chawa,jitahidi kufanya analysis kidogo kabla ya kumtetea bwana yako
 
Ishu ya Rushwa kuna vyombo husika.kama kweli anakula rushwa pelekeni tuhuma pccb, rushwa ipo mpaka magogoni , wewe unashangaa msd , rushwa ipo mpaka TAKUKURU, Wewe unashangaa msd . Fanya kazi acheni umbea
Kwa jinsi ulivyo shallow na usivyo mzalendo, eti unataka watu tufumbie macho rushwa hapo MSD kwa sababu eti rushwa ipo vilevile PCCB, Magogoni etc, je unaweza kuhalalisha uovu kwa uovu mwingine? DOES TWO WRONGS MAKE ONE RIGHT? Je wewe ni kilaza kiasi Cha kutojua kuwa MSD ni Taasisi ya Umma inayoendeshwa Kwa pesa za walipakodi(Taxpayers Money) ikiwemo Mimi mwenyewe, hivyo hujui Kwa sababu hiyo watendaji wa MSD wanawajibika Kwa Umma(Public Accountability) Mr. Mavere, nakushauri achana na machawa wa aina hii watakupoteza kwa sababu they are very unethical, wanatanguliza matumbo mbele na wanafikiria kwa kutumia makalio. Bado una opportunity ya kujirekebisha na kusonga mbele iwapo utayafanyia kazi maoni mbalimbali yakiwemo ya mleta mada
 
washenzi wakikosa nafasi wanakimbilia humu, huyo aliyepost inaonekana kahamishwa toka hapo
 
uwe unafanya analysis kwa taarifa au uombe maelezo , hapo namba 1.KWELI HAO JAMAA WAMEPEWA HIZO 57B NA NILAZIMA UAMBIE UMMA, lakini ukumbuke umepewa hizo pesa, lakini unadaiwa zaidi ya bilioni 200 na wazabuni na kadhalika, na msd anaidai huyohuyo serikali zaidi ya bilion 150+ unategea akili gani hapo? is just ujanja wa kufukia mafukia mambo ambayo hayafutiki.....overhaul ineendana na kulipa madeni ya msd yote na kupatiwa mtaji wa msd kujiendesha, porojo hazifai
 
Pole,jikite kujibu hoja zote za mleta mada pamoja na nilizoainisha hapo juu.Kuna mambo mengine ya ki-utendaji hayahitaji hata hizo pesa inategemea weledi wa kiongozi na timu inayomzunguka.kwa mfano:
  • Je DG Mavere kutembea na ofisi ya umma bila kukaimisha huku aki-paralyze operations kama kuchelewesha mchakato wa manunuzi ya dawa,Je hilo nalo tatizo lina connection gani na uhaba wa pesa?
  • Je kushindwa kukamilisha mchakato wa DIRECTORS RECRUITMENT ili apate watu credible anaowa-trust kuwakaimisha ofisi,pamoja na kufanya decisions zinginezo muhimu,je hilo nalo lina connection gani na madeni au uhaba wa pesa?
  • Je kushindwa kwa Mavere ku-observe Sheria na Kanuni mbalimbali katika kutekeleza majukumu mbalimbali hadi kuletea kashfa Taasisi kama ile kashfa ya PAA au Appointments/Staff Transfrers zisizo na tija,je hayo nayo yanatokana na madeni au uhaba wa pesa?
  • Je yeye Mr.Mavere akiwa free of duress/threats alivyotangazia umma kwamba MSD imepokea TZS 57BLN za kununulia dawa na kuwa zinatosha,je hilo nalo ni shida ya mleta mada?
 
Sukuma gang kaka yenu Mwendazake kauwa uchumi sana na madhala yake tutayaona sana bado miaka 5 mbele ya hali ngumu ya maisha kua magumu sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…