Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,236
- 10,774
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeibua mjadala mkali baada ya kutangaza rasmi umiliki wa timu ya soka ya Tabora United na kuibadilisha jina kuwa TRA United Sports Club. Kwa maneno yao wamedai kuwa hatua hii, inalenga kuhamasisha ulipaji wa kodi wa hiari na kuimarisha uwajibikaji wa kijamii. Kwa 99.9% kauli hii imepokelewa kwa mshangao mkubwa sana miongoni mwa wananchi.
Kwa mujibu wa taarifa ya TRA, timu hiyo sasa itakuwa “mali ya walipakodi na Watanzania wote.” Hata hivyo, kauli hii imeonekana kuwa kinyume na uhalisia, kwani kodi zinazokusanywa na TRA zinapaswa kuelekezwa moja kwa moja katika kuboresha maisha ya wananchi kwa kuwapatia huduma bora za afya, elimu, maji safi, barabara na miradi ya maendeleo siyo kwenye manunuzi ya timu za michezo.
Soma Pia: Rasmi sasa Tabora United imekuwa TRA United SC
Katika mwaka wa fedha 2024/2025, TRA imekusanya jumla ya Shilingi Trilioni 32.26, sawa na ufanisi wa asilimia 103 ya makadirio yao. Ni fedha kubwa ambayo kila Mtanzania anatarajia kuona ikiwekezwa katika kutatua changamoto za msingi zinazowakabili maskini wa Tanzania.
Mashuleni bado kunakosekana madarasa yenye ubora, hospitali hazina dawa za msingi, miundombinu ya maji na barabara vijijini ni duni, huku wakulima na wafanyabiashara wadogo wakihangaika na changamoto za mitaji na masoko.
Katika mazingira haya, wengi tunaona matumizi ya fedha za kodi kwa ajili ya timu ya soka si tu kitendo cha ajabu, bali ni dhihaka na dharau kubwa kwa watanzania.
Swali kubwa linalobaki ni: ni nani aliyewashauri TRA kwamba kununua timu ya soka ni kipaumbele cha kitaifa? Je, ni wazo lililotoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Je, ni wazo la Waziri wa Fedha? Au ni mawazo binafsi ya watendaji waandamizi wa TRA kama Ephraim Mdee (Mkurugenzi wa Tafiti na Mipango), Richard Kayombo (Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano)?.
Ikiwa wazo hili limepitishwa na Bodi ya Wakurugenzi, wajumbe wake akiwemo Yusuph Mwenda, Dr. Mariam Nchimbi, Emmanuel Tutuba na Elijah Mwandumbya, basi kimsingi wamepuuza na kupindisha kabisa dhima ya TRA ya kuhakikisha rasilimali za walipakodi zinatumiwa kwa tija.
Hili ni kosa la kimaadili na kiutendaji ambalo linapaswa kuwafanya viongozi husika wawajibike mara moja. Mkurugenzi Mkuu wa TRA anapaswa kujiuzulu kwa kushindwa kuweka vipaumbele sahihi.
Pia TAKUKURU inapaswa kuingilia kati mara moja kuchunguza mchakato mzima wa manunuzi haya. Ni lazima Watanzania waambiwe ni kiasi gani cha fedha kimetumika, kilitoka wapi na ni nani alikubaliana na uamuzi huu wa hovyo.
TRA inapaswa kukumbuka kwamba kuhamasisha ulipaji wa kodi wa hiari hakuwezi kufanikishwa kwa kutupa maelfu ya mamilioni kwenye michezo ya soka. Walipakodi wanahitaji kuona kodi zao zikibadilisha maisha yao moja kwa moja.
Elimu bora, huduma za afya zinazopatikana na barabara zinazounganisha vijiji na masoko ndizo zitakazowafanya wananchi wakubali kulipa kodi kwa moyo wa hiari – siyo kushangilia timu ya mpira inayobeba jina la TRA. HUO NI UTOTO NA UJINGA WA KIWANGO CHA LAMI.
Hatua ya kununua timu ya Tabora United ni aibu kwa taifa na usaliti kwa wananchi maskini wa Tanzania. Ni wakati wa viongozi wa TRA kusimama vizimbani na kuonyesha uwajibikaji wa kweli.
Vinginevyo, itabaki kuwa mfano wa jinsi taasisi kubwa inaweza kupoteza dira na kugeuka mzigo kwa wananchi waliowakabidhi mamlaka ya ukusanyaji kodi.
KULIKUWA HAKUNA ULAZIMA WOWOTE WA TRA KUNUNUA TIMU YA TABORA UNITED.