Sisi TRA tumeiga kwa ndugu zetu wa Uganda URA, URA sports club. Si unajua waswahili wanasema: kizuri kula na wenzio. Kosa letu ni lipi. Awamu hii kufa masikini ni kujitakia.
PS
Halafu tupesa vyenyewe tulivyonunulia Tabora united, Tsh 55bn ni pesa ya kuifungulia thread, kweli?
Umepata kusikia sababu za kununua Tabora United mkuu!?
Hapo sawa Mkuu maana sababu ya manunuzi ya timu ndio inatia mashaka sana! Unanunuaje timu ili ikawafanye watu wapate elimu ya kodiSababu zao nimezisoma hazina mashiko...
Kitu pekee walipaswa kusema labda ni kwamba wameamua kujikita kwenye mpira wa miguu ili kuungana na juhudi za TFF na wizara ya michezo kuboresha timu za ligi kuu kwa kuanza na kumiliki timu...
Maana kama ni kodi za wananchi, timu za majeshi na zile za manispaa nazo zinaendeshwa kwa uwezo wa makusanyo ya kikodi tu...