msomi uchwara
JF-Expert Member
- Oct 17, 2017
- 4,796
- 9,165
Chaka jipya hilo la kupigia pesa,,,kumiliki timu ni ghali sana, ni heri wangeenda kuidhamini yanga au simba wakae kwenye jezi basi
Bandari haikuwahi kununua timu ilikua ina-fanya recruitment ya wachezaji wenye vipaji kutoka sehemu tofauti tofauti kisha inaunda timu na ilikua na timu nyingi sana football, volleyball, netball, basketball, nk zote hizo sio za kununua walikua wanachukua vijana wenye vipaji kutoka mashuleni kwenye mashindano ya umiseta, umitashumta, maeneo ya mitaa vijana wanapocheza cha ndimu, mchangani, nk kote huko inapita inachukua wachezaji tofauti tofauti ndio ikaunda hizo timu ambazo zilishiriki mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi, baadae timu hizo zilipokufa wachezaji hao wakageuzwa kua wafanyakazi wa Bandari katika vitengo tofauti tofauti, timu za Bandari tangu zife hazijawahi kurudi tena, kwa hio kulinganisha TRA kununua timu kwamba Bandari iliwahi kununua timu Bandari haikuwahi kununua timu ilikua inatengeneza wachezaji na kuchukua vijana wenye vipaji maeneo tofauti kisha inaundwa timuBandari ilishawahi kumiliki timu
Heshima yako mkuu 🫡Bandari haikuwahi kununua timu ilikua ina-fanya recruitment ya wachezaji wenye vipaji kutoka sehemu tofauti tofauti kisha inaunda timu na ilikua na timu nyingi sana football, volleyball, netball, basketball, nk zote hizo sio za kununua walikua wanachukua vijana wenye vipaji kutoka mashuleni kwenye mashindano ya umiseta, umitashumta, maeneo ya mitaa vijana wanapocheza cha ndimu, mchangani, nk kote huko inapita inachukua wachezaji tofauti tofauti ndio ikaunda hizo timu ambazo zilishiriki mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi, baadae timu hizo zilipokufa wachezaji hao wakageuzwa kua wafanyakazi wa Bandari katika vitengo tofauti tofauti, timu za Bandari tangu zife hazijawahi kurudi tena, kwa hio kulinganisha TRA kununua timu kwamba Bandari iliwahi kununua timu Bandari haikuwahi kununua timu ilikua inatengeneza wachezaji na kuchukua vijana wenye vipaji maeneo tofauti kisha inaundwa timu
Hiyo ni ccm .utawaambia nini ndugu yangu. Machozi ya samaki ndani ya majiMamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeibua mjadala mkali baada ya kutangaza rasmi umiliki wa timu ya soka ya Tabora United na kuibadilisha jina kuwa TRA United Sports Club. Kwa maneno yao wamedai kuwa hatua hii, inalenga kuhamasisha ulipaji wa kodi wa hiari na kuimarisha uwajibikaji wa kijamii. Kwa 99.9% kauli hii imepokelewa kwa mshangao mkubwa sana miongoni mwa wananchi.
View attachment 3476674
Kwa mujibu wa taarifa ya TRA, timu hiyo sasa itakuwa “mali ya walipakodi na Watanzania wote.” Hata hivyo, kauli hii imeonekana kuwa kinyume na uhalisia, kwani kodi zinazokusanywa na TRA zinapaswa kuelekezwa moja kwa moja katika kuboresha maisha ya wananchi kwa kuwapatia huduma bora za afya, elimu, maji safi, barabara na miradi ya maendeleo siyo kwenye manunuzi ya timu za michezo.
Soma Pia: Rasmi sasa Tabora United imekuwa TRA United SC
View attachment 3476675
Katika mwaka wa fedha 2024/2025, TRA imekusanya jumla ya Shilingi Trilioni 32.26, sawa na ufanisi wa asilimia 103 ya makadirio yao. Ni fedha kubwa ambayo kila Mtanzania anatarajia kuona ikiwekezwa katika kutatua changamoto za msingi zinazowakabili maskini wa Tanzania.
View attachment 3476682
Mashuleni bado kunakosekana madarasa yenye ubora, hospitali hazina dawa za msingi, miundombinu ya maji na barabara vijijini ni duni, huku wakulima na wafanyabiashara wadogo wakihangaika na changamoto za mitaji na masoko.
View attachment 3476680
Katika mazingira haya, wengi tunaona matumizi ya fedha za kodi kwa ajili ya timu ya soka si tu kitendo cha ajabu, bali ni dhihaka na dharau kubwa kwa watanzania.
View attachment 3476673
Swali kubwa linalobaki ni: ni nani aliyewashauri TRA kwamba kununua timu ya soka ni kipaumbele cha kitaifa? Je, ni wazo lililotoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Je, ni wazo la Waziri wa Fedha? Au ni mawazo binafsi ya watendaji waandamizi wa TRA kama Ephraim Mdee (Mkurugenzi wa Tafiti na Mipango), Richard Kayombo (Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano)?.
View attachment 3476672
Ikiwa wazo hili limepitishwa na Bodi ya Wakurugenzi, wajumbe wake akiwemo Yusuph Mwenda, Dr. Mariam Nchimbi, Emmanuel Tutuba na Elijah Mwandumbya, basi kimsingi wamepuuza na kupindisha kabisa dhima ya TRA ya kuhakikisha rasilimali za walipakodi zinatumiwa kwa tija.
View attachment 3476671
Hili ni kosa la kimaadili na kiutendaji ambalo linapaswa kuwafanya viongozi husika wawajibike mara moja. Mkurugenzi Mkuu wa TRA anapaswa kujiuzulu kwa kushindwa kuweka vipaumbele sahihi.
View attachment 3476670
Pia TAKUKURU inapaswa kuingilia kati mara moja kuchunguza mchakato mzima wa manunuzi haya. Ni lazima Watanzania waambiwe ni kiasi gani cha fedha kimetumika, kilitoka wapi na ni nani alikubaliana na uamuzi huu wa hovyo.
View attachment 3476689
TRA inapaswa kukumbuka kwamba kuhamasisha ulipaji wa kodi wa hiari hakuwezi kufanikishwa kwa kutupa maelfu ya mamilioni kwenye michezo ya soka. Walipakodi wanahitaji kuona kodi zao zikibadilisha maisha yao moja kwa moja.
View attachment 3476677
Elimu bora, huduma za afya zinazopatikana na barabara zinazounganisha vijiji na masoko ndizo zitakazowafanya wananchi wakubali kulipa kodi kwa moyo wa hiari – siyo kushangilia timu ya mpira inayobeba jina la TRA. HUO NI UTOTO NA UJINGA WA KIWANGO CHA LAMI.
View attachment 3476678
Hatua ya kununua timu ya Tabora United ni aibu kwa taifa na usaliti kwa wananchi maskini wa Tanzania. Ni wakati wa viongozi wa TRA kusimama vizimbani na kuonyesha uwajibikaji wa kweli.
View attachment 3476679
Vinginevyo, itabaki kuwa mfano wa jinsi taasisi kubwa inaweza kupoteza dira na kugeuka mzigo kwa wananchi waliowakabidhi mamlaka ya ukusanyaji kodi.
KULIKUWA HAKUNA ULAZIMA WOWOTE WA TRA KUNUNUA TIMU YA TABORA UNITED.
Unafahamu TRA anatimu zake kwa badhi ya michezo na hua anafanya recruitment pia,??Bandari haikuwahi kununua timu ilikua ina-fanya recruitment ya wachezaji wenye vipaji kutoka sehemu tofauti tofauti kisha inaunda timu na ilikua na timu nyingi sana football, volleyball, netball, basketball, nk zote hizo sio za kununua walikua wanachukua vijana wenye vipaji kutoka mashuleni kwenye mashindano ya umiseta, umitashumta, maeneo ya mitaa vijana wanapocheza cha ndimu, mchangani, nk kote huko inapita inachukua wachezaji tofauti tofauti ndio ikaunda hizo timu ambazo zilishiriki mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi, baadae timu hizo zilipokufa wachezaji hao wakageuzwa kua wafanyakazi wa Bandari katika vitengo tofauti tofauti, timu za Bandari tangu zife hazijawahi kurudi tena, kwa hio kulinganisha TRA kununua timu kwamba Bandari iliwahi kununua timu Bandari haikuwahi kununua timu ilikua inatengeneza wachezaji na kuchukua vijana wenye vipaji maeneo tofauti kisha inaundwa timu
Basi tu MkuuKungekua na tija kama hayo mamilioni kama sio mabilioni waliyonunulia hiyo timu, wangesambaza watu mitaani kueneza elimu juu ya kodi, matangazo kila kona mpaka tuyachoke, wawalipe hata wasanii wakubwa wahamasishe watu kulipa kodi, kuliko hilo la kununua timu ambapo uendeshwaji wa hiyo timu ni gharama nyingine.
Kuhudumia mijitu zaidi ya 30, mavazi, malazi, chakula, mishahara na bonus si mchezo aisee.
Taasisi za umma ni vyema zijihusishe na mambo ya umma sio kila siku Kodi tu.Nani ataenda kuangalia Tabora Wewe kama walitaka matangazo yao TRA wangekaa timu hizi kubwa Simba na Yanga angalau wangeeleweka unajua gharama ya kuendesha timu hata hiyo Singida ngoja waziri wa fedha apigwe chini huone Kama kutakua kuna timu kuendesha timu sio mchezo
Ni kweli mkuu ila ukitazama process za manunuzi na sababu sidhani kama Bodi ya Wakurugenzi wanafahamu kwa undani!Taasisi za umma ni vyema zijihusishe na mambo ya umma sio kila siku Kodi tu.
Uganda wana URA
Zambia wana Zanako
Tanesco ya Zambia ina Zesco
Kenya wana Bandari
Ushuru fc Kenya
Fuatilia acha kulalamika
Hizo process za manunuzi ni vitu Sina uhakika na ushahidi navyoNi kweli mkuu ila ukitazama process za manunuzi na sababu sidhani kama Bodi ya Wakurugenzi wanafahamu kwa undani!
Aliyetoa wazo la kununua timu alitaka waitumie timu kuwashawishi watu kulipa kodi 😃TRA pesa walizotumia kununulia hiyo timu ni bora wangetumia pesa hiyo kununulia mashine zile zakutoa risiti EFD wazigawe bure kwa wafanyabishara ambao hawana ili iwe rahisi kwao kupata kodi stahili.