Kulikuwa hakuna ulazima wowote wa TRA kununua Tabora United?

Chaka jipya hilo la kupigia pesa,,,kumiliki timu ni ghali sana, ni heri wangeenda kuidhamini yanga au simba wakae kwenye jezi basi
 
Bandari ilishawahi kumiliki timu
Bandari haikuwahi kununua timu ilikua ina-fanya recruitment ya wachezaji wenye vipaji kutoka sehemu tofauti tofauti kisha inaunda timu na ilikua na timu nyingi sana football, volleyball, netball, basketball, nk zote hizo sio za kununua walikua wanachukua vijana wenye vipaji kutoka mashuleni kwenye mashindano ya umiseta, umitashumta, maeneo ya mitaa vijana wanapocheza cha ndimu, mchangani, nk kote huko inapita inachukua wachezaji tofauti tofauti ndio ikaunda hizo timu ambazo zilishiriki mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi, baadae timu hizo zilipokufa wachezaji hao wakageuzwa kua wafanyakazi wa Bandari katika vitengo tofauti tofauti, timu za Bandari tangu zife hazijawahi kurudi tena, kwa hio kulinganisha TRA kununua timu kwamba Bandari iliwahi kununua timu Bandari haikuwahi kununua timu ilikua inatengeneza wachezaji na kuchukua vijana wenye vipaji maeneo tofauti kisha inaundwa timu
 
Heshima yako mkuu 🫡
 
Kungekua na tija kama hayo mamilioni kama sio mabilioni waliyonunulia hiyo timu, wangesambaza watu mitaani kueneza elimu juu ya kodi, matangazo kila kona mpaka tuyachoke, wawalipe hata wasanii wakubwa wahamasishe watu kulipa kodi, kuliko hilo la kununua timu ambapo uendeshwaji wa hiyo timu ni gharama nyingine.

Kuhudumia mijitu zaidi ya 30, mavazi, malazi, chakula, mishahara na bonus si mchezo aisee.
 
Hiyo ni ccm .utawaambia nini ndugu yangu. Machozi ya samaki ndani ya maji
 
Unafahamu
Unafahamu TRA anatimu zake kwa badhi ya michezo na hua anafanya recruitment pia,??
 
Basi tu Mkuu
 
Hiyo ni ccm .utawaambia nini ndugu yangu. Machozi ya samaki ndani ya maji
Hapana Mkuu 😔 Ipo siku tutaamka asubuhi kukutana na BOT wamenunua Kitambaa Cheupe 😔 Mzaha Mzaha ......................
 
Taasisi za umma ni vyema zijihusishe na mambo ya umma sio kila siku Kodi tu.
Uganda wana URA
Zambia wana Zanako
Tanesco ya Zambia ina Zesco
Kenya wana Bandari
Ushuru fc Kenya
Fuatilia acha kulalamika
 
Taasisi za umma ni vyema zijihusishe na mambo ya umma sio kila siku Kodi tu.
Uganda wana URA
Zambia wana Zanako
Tanesco ya Zambia ina Zesco
Kenya wana Bandari
Ushuru fc Kenya
Fuatilia acha kulalamika
Ni kweli mkuu ila ukitazama process za manunuzi na sababu sidhani kama Bodi ya Wakurugenzi wanafahamu kwa undani!
 
Ni kweli mkuu ila ukitazama process za manunuzi na sababu sidhani kama Bodi ya Wakurugenzi wanafahamu kwa undani!
Hizo process za manunuzi ni vitu Sina uhakika na ushahidi navyo
Nachosema TRA kumiliki timu ni jambo zuri kabisa na sio geni
 
TRA pesa walizotumia kununulia hiyo timu ni bora wangetumia pesa hiyo kununulia mashine zile zakutoa risiti EFD wazigawe bure kwa wafanyabishara ambao hawana ili iwe rahisi kwao kupata kodi stahili.
 
TRA pesa walizotumia kununulia hiyo timu ni bora wangetumia pesa hiyo kununulia mashine zile zakutoa risiti EFD wazigawe bure kwa wafanyabishara ambao hawana ili iwe rahisi kwao kupata kodi stahili.
Aliyetoa wazo la kununua timu alitaka waitumie timu kuwashawishi watu kulipa kodi 😃
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…