Kulikuwa hakuna ulazima wowote wa TRA kununua Tabora United?

TRA Tanzania natumaini sisi kama walipa kodi mtatuoatia maelezo yakina kuhusu faida na hasa katika hili swala ili nasi tuwapime kwa utandaji kazi yenu
 
Aliyetoa wazo la kununua timu alitaka waitumie timu kuwashawishi watu kulipa kodi 😃
Tatizo siyo kulipa kodi je wao TRA wameweka mazingira gani rafiki ya kumshawishi mtu alipe kodi. ?
 
Mimi kama mlipa kodi ndani ya hii nchi (na hata tarehe 30 ya mwezi huu natakiwa kulipa kodi ya awamu ya 3)! Kamwe siungi mkono huu ujinga uliofanywa na TRA!

Kwanza hawajatushirikisha walipa kodi wao ili kutoa maoni yetu! Na kwa kufanya hivi, niwe tu mkweli! Ninaiombea mabaya hii timu ya Tabora United! Ikiwezekana mwishoni mwa msimu huu ishuke daraja, na kujifia kifo cha mende.


Haiwezekani sisi tulipe kodi kwa mateso, halafu hela zetu mnaenda kuzichezea kwenye mambo ya kipuuzi. Na nina uhakika mwishoni mwa mwaka mkiulizwa faida mliyoipata kwenye huu uwekezaji wenu wa kipuuzi, hamtakuwa na majibu.
 
Kuna jambo gani limeshawahi fanywa nchi hii likaungwa mkono na wote?
 
Team ya saa 100 wanachezea pesa walipa kodi.......
 
Sisi TRA tumeiga kwa ndugu zetu wa Uganda URA, URA sports club. Si unajua waswahili wanasema: kizuri kula na wenzio. Kosa letu ni lipi. Awamu hii kufa masikini ni kujitakia.

PS
Halafu tupesa vyenyewe tulivyonunulia Tabora united, Tsh 55bn ni pesa ya kuifungulia thread, kweli?
 
Serious mkuu! Yaani badala ya kwenda kuboresha miundombinu ili upate kodi zaidi, unakwenda kununua timu ili uongeze utoaji wa elimu? 1 jumlisha 1 sio 11 mkuu
 
Mgulu wa chemba 1st class economiste akujulishe wewe FFF
 
Ni kawaida

Zamani kulikuwa na timu toka taasisi za serikali au bodi za mazao, biashara n.k kama : Mecco, Sigara, Tumbaku, Pamba, Reli, RTC, Ushirika, Kurugenzi n.k

Baadaye kukawa na timu za taasisi za kiserikali kama polisi, jeshi, magereza, zimamoto...

Pia kuna timu za halimashauri, mikoa kama Mbeya City, KMC, Mji Mpwapwa n.k...

Sio jambo geni...
 
Umepata kusikia sababu za kununua Tabora United mkuu!?
 
TRA hawa waliofuta risiti ya 2.4 billion ya Abdul?
Corrupt and rotten.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…