Ni takribani miezi 6 tu imepita viongozi walikuwa Chato kuweka mashada kwenye kaburi la Magufuli mashada mengine yangalipo na hayajakauka, ni sababu zipi zimefanya tena leo kuweka mashada kwenye kaburi lile lile, kama lengo lilikuwa kuzima mwenge kwa nini wasingeitumia siku ya leo kwa shughuli iliyowapeka na kama kulikuwa na mtu angependa kutembelea kaburi kwanini asingeenda jana au kesho kupisha hii siku muhimu ya kumbukumbu ya Nyerere?
Njia nzuri ya kukumbuka siku ya marehemu ni kusafisha kaburi lake au kulitembelea na kuwafariji wafiwa, kwa vile leo ilikuwa siku ya Nyerere ilikuwa sahihi kabisa kuzuru kaburi la Nyerere na kumfariji Mama Maria badala ya kuweka maua kwenye kaburi la Magufuli.