Kulikuwa na uhalali gani kwa Chief Mkwawa kutambulika kama 'Shujaa?

Kulikuwa na uhalali gani kwa Chief Mkwawa kutambulika kama 'Shujaa?

Hii ni kwa vijana ambao maziwa ya mama yao hayajawaisha mdomoni,,,

Yaani wananuka maziwa mdomoni.
Iko hivi:
Kwenye mbinu za medani, askari akiona yuko hatarini kukamatwa,,,
Na akijua akikamatwa atatoa siri kwa mateso atakayopata
Mbinu ya medani inamtaka

3 atoroke
2 awe na uwezo wa kuhimili mateso
1 Ajiue.
Wengi huchagua mbinu no 1
 
Kama hakuwa shujaa mbn wajerumani walikata kichwa na kuondoka nacho??

Huoni kuwa ule ushujaa wake wa kuwasumbua na kuwaua wazungu, ndio ulikuwa ushujaa wake na ujasiri pia. Maana hata kujiua ni ushujaa wa kutokukiogopa kifo
Kujiua ni uoga wa maisha mkuu na waoga kamwe hawatauona ufalme wa Mungu. Mzalendo hajiua hata siku moja.
 
So wajerumani waliamua kuweka kichwa cha mtu muoga??
Unajua nini maana ya neno TROPHY? Maana yake ni kwamba, "something used as a symbol of success from hunting or war"

For Example: The animal heads on the wall were trophies of his hunting trips.

Soma kamusi hii hapa>>> trophy
 
Hitler nae alikuwa muoga??
Mpaka sasa bado ulimwengu haujui nini kilimkuta Adolph Hitler. Miongoni mwa majeshi ya washirika yalioungana katika kuung'oa utawala wa Nazi, kuna wanaodhani Marekani ilimficha kama ambavyo wanadai Osama amefichwa
 
[emoji28][emoji28] so fuvu la mkwawa kumba ni "trophy" kwann hawakuchukua na mafuvu mengine ya askari waliokufa??
Kwanini video ya kuuwawa kwa Saddam na Gadaffi zimesambaa mitandaoni na sio za askari wengine wa Iraq na Libya? Jibu ni rahisi sana, wao ndio "Commanders In Chief" ikiwa na maana kwamba nchi haiwezi kuingia vitani pasipo wao kuidhinisha.
 
Hii ni kwa vijana ambao maziwa ya mama yao hayajawaisha mdomoni,,,

Yaani wananuka maziwa mdomoni.
Iko hivi:
Kwenye mbinu za medani, askari akiona yuko hatarini kukamatwa,,,
Na akijua akikamatwa atatoa siri kwa mateso atakayopata
Mbinu ya medani inamtaka

3 atoroke
2 awe na uwezo wa kuhimili mateso
1 Ajiue.
Wengi huchagua mbinu no 1
Mkuu, hata kama sisi sio askari acha kutudanganya. Kutoroka ni option au ni jambo ambalo kila anayezidiwa na adui yake anapenda kulifanya?

Mapambayo yakizidi na unaona hauna namna, hapo kutoroka ni lazima na sio option kama ambavyo unataka kutuaminisha hapa mkuu.

Kujiua au kutojiua ndio options lakini kutoroka "is a REFLEX" na inakuja "automatically"
 
Habari za wakati huu ndugu zangu wa humu jamiiforums.

Kulikuwa na uhalali gani wa Chief Mkwawa kutambulika kama "shujaa"? Kamwe hakuna askari anayeweza kuitwa shujaa kwa kuogopa adui kisha kujiua mwenyewe.

View attachment 1716322

Mbona Muamar Gadaffi wa Libya na Saddam Hussein wa Iraq hawakujiua kabla ya kukamatwa na wazungu? Mkwawa alikuwa shujaa ama askari muoga?

UOGA SIO SIFA NJEMA YA MWANAUME MPIGANAJI
=====
Uoga ni tabia ambayo hofu nyingi humzuia mtu kupambana na hatari au kukabiliana na adui. Uoga unaonyesha uwezo wa mtu kukosa tabia ya ujasiri wakati wa changamoto. Katika kanuni za kijeshi za nchi nyingi hapa duniani, uoga katika vita ni sawa sawa na uhalifu.

Vitendo vya uoga, kwa muda mrefu tangia vita ya kwanza ya dunia, vimeadhibiwa na sheria za kijeshi, ambazo inafafanua vema makosa yanayohesabika kama uoga, ikiwa pamoja na kumkimbia adui au kujisalimisha kwa adui pasipo kupata amri kutoka kwa wakubwa. Wale ambao walikamatwa walikuwa, mara kwa mara, wakipelekwa mahakamani na adhabu ya vitendo kama hivyo kwa kawaida huwa ni kali sana.

Siku zote ulimwengu umewaheshimu majasiri na kuwalaani waoga. Kuwa jasiri ni muhimu kwa mwanamume kama vile kuwa msafi kwa mwanamke, na muoga kati ya wanaume ana sifa mbaya kama kahaba kati ya wanawake.

Kujiua huitwa ni uoga kwa sababu inahitaji ujasiri wa hali ya juu sana ili uweze kuishi katika dunia iliyojaa kila aina ya changamoto, inahitaji mtu kuwa na mtazamo sahihi juu ya maisha na utulivu mkubwa wa akili. Pamoja na shinikizo na shida zote, vuta nikuvute za maisha ambavyo tunakabiliwa navyo, baadhi ya waoga huamua kuwa na mawazo hasi na kushindwa kupambana tena na badala yake kuchagua kufa.

KWA UFUPI SANA KUHUSU KIFO CHA CHIEF MKWAWA
=====
Kichwa cha mtemi kinasemekana kilikatwa na Wajerumani na kutumwa Berlin kilipohifadhiwa katika makumbusho, awali Berlin na baadaye Bremen. Waingereza waliochukua utawala wa koloni mwaka 1918 baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia walitaka kuonekana kama mabwana wema.

Mkuu wa serikali ya kikoloni ya Tanganyika alipendekeza kurudisha fuvu kwa sababu Wahehe walishirikiana na Waingereza wakati wa vita. Hivyo kuna kipengele 246 katika mkataba wa Versailles kinachosema: "Katika muda wa miezi 6 baada ya kuthebitishwa kwa mkataba huu. Ujerumani itakabidhi fuvu ya Sultani Mkwawa iliyohamishwa kutoka Afrika ya Mashariki ya Kijerumani na kupelekwa Ujerumani kwa serikali ya Mfalme wa Uingereza.

Wajerumani walikataa habari za fuvu hii na Waingereza waliamua ya kwamba ilishindikana kuikuta. Lakini baada ya vita kuu ya pili ambako Ujerumani penyewe ilivamiwa na wanajeshi wa Uingereza gavana Twining wa Tanganyika alikumbuka habari za fuvu akatembelea Ujerumani na kutazama mafuvu ya makumbusho ya Bremen.

Katika mkusanyiko wa fuvu 2000 zilikuwa 84 zenye namba zilizoonyesha zilitoka kiasili katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Hapa alizipanga kufuatana na ukubwa na kutazama zile zilizokuwa na vipimo vya karibu na ndugu za Mkwawa aliowahi kupima kabla ya safari yake. Hapa aliteua fuvu yenye shimo kwa sababu taarifa ya kale ilisema Mkwawa alijiua kwa kujipigia risasi kichwani.

Kulikuwa na uhalali gani kwa askari aliyejiua kutambulika kama "shujaa"?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Wakati mwingine ni ule uthubutu tu unafanya mtu aitwe shujaa maana wengi hata kuthubutu ni shida.
 
Kujiua kuna mambo mengi mkuu ( ingawa bado suala la Mkwawa kujiua is still debatable, hakuna mwenye uhakika ). Mimi nasoma sana hata habari za Waisrael (sasa Wayahudi ) na wenyewe mara kadhaa viongozi wao walipo elemewa walijiua; iko hivi; KIONGOZI ukitekwa, utateswa hadi useme SIRI yenu, na hilo ndilo ambalo adui hulitafuta, bora ufe na siri yako ili wengine walioachwa wapambane kivyao wakiendelea kuzishikiria codes zenu/zao
kwanza umeanza kwa kuharibu kudhani israel inaumaalumu wowote ,na sijui imetokeaje kwenye thread za kishujaa,anyway madini hayo yakuletewa,swala la kujiua useme siri nalielewa na mkwawa ni shujaa maana alipambana na wajerumani miaka minne (najua hujui) polini wakiwa wanamzidi technology mbali ,kukamatwa kwake yeye wangekutumia kuwavunja nguvu wahehe ya kimapinduzi maana wangeamua hata kuuburuza mwili wake kila mahali ili kuwakatisha moyo wahehe.
aidha wahehe waliendelea kuwa shida kuwatawala na hata wajerumani kadhaa waliandika kuwa watu wenye kiburi ,wavivu na hasira ,hata mashambani mwao wajerumani waliajiri wakinga na wabena sio wahehe .
 
kwanza umeanza kwa kuharibu kudhani israel inaumaalumu wowote ,na sijui imetokeaje kwenye thread za kishujaa,anyway madini hayo yakuletewa,swala la kujiua useme siri nalielewa na mkwawa ni shujaa maana alipambana na wajerumani miaka minne (najua hujui) polini wakiwa wanamzidi technology mbali ,kukamatwa kwake yeye wangekutumia kuwavunja nguvu wahehe ya kimapinduzi maana wangeamua hata kuuburuza mwili wake
Mkuu, sasa kama waliweza kuukata kichwa, kwani wangeshindwa kuuburuza kwa maana ulikuwa katika himaya yao tayari. Kwahiyo tuseme Wajerumani hawakuamua tu kufanya hivyo lakini haina uhusiano wowote wa yeye (Mkwawa) kujiua? Au sio mkuu?...
 
Sijategemea wewe kuuliza hilo swali Mkuu, kwani si ulifunzwa kuhusu 'suicide pill'?
 
Hujawahi kusikia msema "kwa shujaa uenda kilio" wewe?[emoji35]
 
Back
Top Bottom