Kulikuwa na uhalali gani kwa Chief Mkwawa kutambulika kama 'Shujaa?

Unajua ni kwanini Rais Samia anamshinda Tundu Lissu? Ni kwa sababu yule kiwete wa Ubelgiji hana jipya na watanzania wamechoka kelele zake
 
Acheni kuweweseka nyie Wapinzani. Rais Samia ametupeleka uchumi wa kati kwa miaka mitano tu.
 
Hivi wewe bado unaamini hizi history fake, leo kane ya 21 humgusi mgerumani hiyo miaka nguvu ya kupigana nao tulitoa wapi? History ina uwongo kibao mara sijui vita vya majimaji hawakupigana huku Town mzizima wakapigane porini kule. Hata hayo mambo sijui babu zetu walichukuliwa watumwa mimi sijawahi kusikia family yoyote ku report babu is missing. Vita vya Uganda tuliambiwa jamaa ana kichwa cha nyoka tukawa tunaamini tukaambiwa leo kachinja mtoto wake kamla tukaamini......
 
Kujiua kuna mambo mengi mkuu ( ingawa bado suala la Mkwawa kujiua is still debatable, hakuna mwenye uhakika ). Mimi nasoma sana hata habari za Waisrael (sasa Wayahudi ) na wenyewe mara kadhaa viongozi wao walipo elemewa walijiua; iko hivi; KIONGOZI ukitekwa, utateswa hadi useme SIRI yenu, na hilo ndilo ambalo adui hulitafuta, bora ufe na siri yako ili wengine walioachwa wapambane kivyao wakiendelea kuzishikiria codes zenu/zao
Nasikia hata Makomandoo vitani au kwenye operesheni zao huwa wana vidonge vya sumu kiasi kwamba akitekwa fasta anameza ili afe kutunza siri
 
Habari za wakati huu ndugu zangu wa humu JamiiForums.

Kulikuwa na uhalali gani wa Chief Mkwawa kutambulika kama "shujaa"? Kamwe hakuna askari anayeweza kuitwa shujaa kwa kuogopa adui kisha kujiua mwenyewe.

Mbona Muamar Gadaffi wa Libya na Saddam Hussein wa Iraq hawakujiua kabla ya kukamatwa na wazungu? Mkwawa alikuwa shujaa ama askari muoga?

UOGA SIO SIFA NJEMA YA MWANAUME MPIGANAJI
=====
Uoga ni tabia ambayo hofu nyingi humzuia mtu kupambana na hatari au kukabiliana na adui. Uoga unaonyesha uwezo wa mtu kukosa tabia ya ujasiri wakati wa changamoto. Katika kanuni za kijeshi za nchi nyingi hapa duniani, uoga katika vita ni sawa sawa na uhalifu.

Vitendo vya uoga, kwa muda mrefu tangia vita ya kwanza ya dunia, vimeadhibiwa na sheria za kijeshi, ambazo inafafanua vema makosa yanayohesabika kama uoga, ikiwa pamoja na kumkimbia adui au kujisalimisha kwa adui pasipo kupata amri kutoka kwa wakubwa. Wale ambao walikamatwa walikuwa, mara kwa mara, wakipelekwa mahakamani na adhabu ya vitendo kama hivyo kwa kawaida huwa ni kali sana.

Siku zote ulimwengu umewaheshimu majasiri na kuwalaani waoga. Kuwa jasiri ni muhimu kwa mwanamume kama vile kuwa msafi kwa mwanamke, na muoga kati ya wanaume ana sifa mbaya kama kahaba kati ya wanawake.

Kujiua huitwa ni uoga kwa sababu inahitaji ujasiri wa hali ya juu sana ili uweze kuishi katika dunia iliyojaa kila aina ya changamoto, inahitaji mtu kuwa na mtazamo sahihi juu ya maisha na utulivu mkubwa wa akili. Pamoja na shinikizo na shida zote, vuta nikuvute za maisha ambavyo tunakabiliwa navyo, baadhi ya waoga huamua kuwa na mawazo hasi na kushindwa kupambana tena na badala yake kuchagua kufa.

KWA UFUPI SANA KUHUSU KIFO CHA CHIEF MKWAWA
=====
Kichwa cha mtemi kinasemekana kilikatwa na Wajerumani na kutumwa Berlin kilipohifadhiwa katika makumbusho, awali Berlin na baadaye Bremen. Waingereza waliochukua utawala wa koloni mwaka 1918 baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia walitaka kuonekana kama mabwana wema.

Mkuu wa serikali ya kikoloni ya Tanganyika alipendekeza kurudisha fuvu kwa sababu Wahehe walishirikiana na Waingereza wakati wa vita. Hivyo kuna kipengele 246 katika mkataba wa Versailles kinachosema: "Katika muda wa miezi 6 baada ya kuthebitishwa kwa mkataba huu. Ujerumani itakabidhi fuvu ya Sultani Mkwawa iliyohamishwa kutoka Afrika ya Mashariki ya Kijerumani na kupelekwa Ujerumani kwa serikali ya Mfalme wa Uingereza.

Wajerumani walikataa habari za fuvu hii na Waingereza waliamua ya kwamba ilishindikana kuikuta. Lakini baada ya vita kuu ya pili ambako Ujerumani penyewe ilivamiwa na wanajeshi wa Uingereza gavana Twining wa Tanganyika alikumbuka habari za fuvu akatembelea Ujerumani na kutazama mafuvu ya makumbusho ya Bremen.

Katika mkusanyiko wa fuvu 2000 zilikuwa 84 zenye namba zilizoonyesha zilitoka kiasili katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Hapa alizipanga kufuatana na ukubwa na kutazama zile zilizokuwa na vipimo vya karibu na ndugu za Mkwawa aliowahi kupima kabla ya safari yake. Hapa aliteua fuvu yenye shimo kwa sababu taarifa ya kale ilisema Mkwawa alijiua kwa kujipigia risasi kichwani.

Kulikuwa na uhalali gani kwa askari aliyejiua kutambulika kama "shujaa"?

ANGALIZO: Mimi Infantry Soldier sio askari jeshi wala mtumishi wa ofisi yoyote ya serikali bali ni raia mwema ninayeipenda sana Tanzania. Hili jina nilijpa tu kutokana na changamoto kadhaa nzito nilizowahi kuzipitia katika maisha yangu.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Katika uwanja wa vita askari yeyote anayejiua kwa nia kukwepa kukamatwa na adui Kama mateka anastahili na ana sifa zote za kuitwa shujaa kwani anakuwa ameokoa wenzake kwa maana endapo atakamatwa na adui lazima atabanwa atoe Siri zao,jinsi ya mapigano yao,mafunzo yao, walipo wenzake(ngome), kiongozi wao, mipango yao ya baadae, na aina zao za silaha hizi huwa Ni habari muhimu ambazo adui yako anazihitaji sana, hivyo kujiua kwake kuliokoa mambo mengi kwa faida ya wenzake
 
Nimesoma na mmoja wa akina Mkwawa yeye anapinga kabisa kuwa Chifu alijiua. Huyo mjukuu anadai kuwa babu yao huyo alikuwa Muislam safi anayejitambua aliyejua kuwa kujiua ni haramu katika Uislam kwahiyo asingeweza kujiua. Kwa maelezo hayo inawezekana Mkwawa aliuawa na Wajerumani.
 
Habari za wakati huu ndugu zangu wa humu JamiiForums.

Kulikuwa na uhalali gani wa Chief Mkwawa kutambulika kama "shujaa"? Kamwe hakuna askari anayeweza kuitwa shujaa kwa kuogopa adui kisha kujiua mwenyewe.

View attachment 1853078

Mbona Muamar Gadaffi wa Libya na Saddam Hussein wa Iraq hawakujiua kabla ya kukamatwa na wazungu? Mkwawa alikuwa shujaa ama askari muoga?

UOGA SIO SIFA NJEMA YA MWANAUME MPIGANAJI
=====
Uoga ni tabia ambayo hofu nyingi humzuia mtu kupambana na hatari au kukabiliana na adui. Uoga unaonyesha uwezo wa mtu kukosa tabia ya ujasiri wakati wa changamoto. Katika kanuni za kijeshi za nchi nyingi hapa duniani, uoga katika vita ni sawa sawa na uhalifu.

Vitendo vya uoga, kwa muda mrefu tangia vita ya kwanza ya dunia, vimeadhibiwa na sheria za kijeshi, ambazo inafafanua vema makosa yanayohesabika kama uoga, ikiwa pamoja na kumkimbia adui au kujisalimisha kwa adui pasipo kupata amri kutoka kwa wakubwa. Wale ambao walikamatwa walikuwa, mara kwa mara, wakipelekwa mahakamani na adhabu ya vitendo kama hivyo kwa kawaida huwa ni kali sana.

Siku zote ulimwengu umewaheshimu majasiri na kuwalaani waoga. Kuwa jasiri ni muhimu kwa mwanamume kama vile kuwa msafi kwa mwanamke, na muoga kati ya wanaume ana sifa mbaya kama kahaba kati ya wanawake.

Kujiua huitwa ni uoga kwa sababu inahitaji ujasiri wa hali ya juu sana ili uweze kuishi katika dunia iliyojaa kila aina ya changamoto, inahitaji mtu kuwa na mtazamo sahihi juu ya maisha na utulivu mkubwa wa akili. Pamoja na shinikizo na shida zote, vuta nikuvute za maisha ambavyo tunakabiliwa navyo, baadhi ya waoga huamua kuwa na mawazo hasi na kushindwa kupambana tena na badala yake kuchagua kufa.

KWA UFUPI SANA KUHUSU KIFO CHA CHIEF MKWAWA
=====
Kichwa cha mtemi kinasemekana kilikatwa na Wajerumani na kutumwa Berlin kilipohifadhiwa katika makumbusho, awali Berlin na baadaye Bremen. Waingereza waliochukua utawala wa koloni mwaka 1918 baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia walitaka kuonekana kama mabwana wema.

Mkuu wa serikali ya kikoloni ya Tanganyika alipendekeza kurudisha fuvu kwa sababu Wahehe walishirikiana na Waingereza wakati wa vita. Hivyo kuna kipengele 246 katika mkataba wa Versailles kinachosema: "Katika muda wa miezi 6 baada ya kuthebitishwa kwa mkataba huu. Ujerumani itakabidhi fuvu ya Sultani Mkwawa iliyohamishwa kutoka Afrika ya Mashariki ya Kijerumani na kupelekwa Ujerumani kwa serikali ya Mfalme wa Uingereza.

Wajerumani walikataa habari za fuvu hii na Waingereza waliamua ya kwamba ilishindikana kuikuta. Lakini baada ya vita kuu ya pili ambako Ujerumani penyewe ilivamiwa na wanajeshi wa Uingereza gavana Twining wa Tanganyika alikumbuka habari za fuvu akatembelea Ujerumani na kutazama mafuvu ya makumbusho ya Bremen.

Katika mkusanyiko wa fuvu 2000 zilikuwa 84 zenye namba zilizoonyesha zilitoka kiasili katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Hapa alizipanga kufuatana na ukubwa na kutazama zile zilizokuwa na vipimo vya karibu na ndugu za Mkwawa aliowahi kupima kabla ya safari yake. Hapa aliteua fuvu yenye shimo kwa sababu taarifa ya kale ilisema Mkwawa alijiua kwa kujipigia risasi kichwani.

Kulikuwa na uhalali gani kwa askari aliyejiua kutambulika kama "shujaa"?

ANGALIZO: Mimi Infantry Soldier sio askari jeshi wala mtumishi wa ofisi yoyote ya serikali bali ni raia mwema ninayeipenda sana Tanzania. Hili jina nilijpa tu kutokana na changamoto kadhaa nzito nilizowahi kuzipitia katika maisha yangu.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Ulikuwepo mstari wa mbele kwenye uwanja wa mapigano? Tukisema wewe ndiye uliyemkata kicha Brigadier Mkwawa ili uchukue nafasi yake tutakua tuko sahihi?
 
Kwa upande wangu namuona bado Mkwavinyika ni shujaa, tena muanzilishi wa 'guerilla welfare' (hapa Dkt. Savimbi na Ernesto Che Guevara watasubiri).

Mtu shupavu aliyeweza kumuua kamanda wa Kijerumani ndugu Zeleworsky si mchezo hata Wajerumani wakashangaa kwa kipigo kile ambacho hawakuwahi kukipata.

Usiangilie kifo chake angalia usumbufu alipowapa wajerumani ndio utajua kuwa Mtwa Mkwawa ni zaidi ya shujaa.
Historia nyingi huwa zinadanganya, Mkwawa alipigana na Waafrika wenzake (mamluki) waliokuwa wanaongozwa na Wajerumani. Tukielewa hili tutakuwa tumejua nanna ya kuelezea simulizi hizi.
 
Back
Top Bottom