Kulikuwa na uhalali gani kwa Chief Mkwawa kutambulika kama 'Shujaa?

Habari za wakati huu ndugu zangu wa humu JamiiForums.

Kulikuwa na uhalali gani wa Chief Mkwawa kutambulika kama "shujaa"? Kamwe hakuna askari anayeweza kuitwa shujaa kwa kuogopa adui kisha kujiua mwenyewe.

Mbona Muamar Gadaffi wa Libya na Saddam Hussein wa Iraq hawakujiua kabla ya kukamatwa na wazungu? Mkwawa alikuwa shujaa ama askari muoga?

UOGA SIO SIFA NJEMA YA MWANAUME MPIGANAJI
=====
Uoga ni tabia ambayo hofu nyingi humzuia mtu kupambana na hatari au kukabiliana na adui. Uoga unaonyesha uwezo wa mtu kukosa tabia ya ujasiri wakati wa changamoto. Katika kanuni za kijeshi za nchi nyingi hapa duniani, uoga katika vita ni sawa sawa na uhalifu.

Vitendo vya uoga, kwa muda mrefu tangia vita ya kwanza ya dunia, vimeadhibiwa na sheria za kijeshi, ambazo inafafanua vema makosa yanayohesabika kama uoga, ikiwa pamoja na kumkimbia adui au kujisalimisha kwa adui pasipo kupata amri kutoka kwa wakubwa. Wale ambao walikamatwa walikuwa, mara kwa mara, wakipelekwa mahakamani na adhabu ya vitendo kama hivyo kwa kawaida huwa ni kali sana.

Siku zote ulimwengu umewaheshimu majasiri na kuwalaani waoga. Kuwa jasiri ni muhimu kwa mwanamume kama vile kuwa msafi kwa mwanamke, na muoga kati ya wanaume ana sifa mbaya kama kahaba kati ya wanawake.

Kujiua huitwa ni uoga kwa sababu inahitaji ujasiri wa hali ya juu sana ili uweze kuishi katika dunia iliyojaa kila aina ya changamoto, inahitaji mtu kuwa na mtazamo sahihi juu ya maisha na utulivu mkubwa wa akili. Pamoja na shinikizo na shida zote, vuta nikuvute za maisha ambavyo tunakabiliwa navyo, baadhi ya waoga huamua kuwa na mawazo hasi na kushindwa kupambana tena na badala yake kuchagua kufa.

KWA UFUPI SANA KUHUSU KIFO CHA CHIEF MKWAWA
=====
Kichwa cha mtemi kinasemekana kilikatwa na Wajerumani na kutumwa Berlin kilipohifadhiwa katika makumbusho, awali Berlin na baadaye Bremen. Waingereza waliochukua utawala wa koloni mwaka 1918 baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia walitaka kuonekana kama mabwana wema.

Mkuu wa serikali ya kikoloni ya Tanganyika alipendekeza kurudisha fuvu kwa sababu Wahehe walishirikiana na Waingereza wakati wa vita. Hivyo kuna kipengele 246 katika mkataba wa Versailles kinachosema: "Katika muda wa miezi 6 baada ya kuthebitishwa kwa mkataba huu. Ujerumani itakabidhi fuvu ya Sultani Mkwawa iliyohamishwa kutoka Afrika ya Mashariki ya Kijerumani na kupelekwa Ujerumani kwa serikali ya Mfalme wa Uingereza.

Wajerumani walikataa habari za fuvu hii na Waingereza waliamua ya kwamba ilishindikana kuikuta. Lakini baada ya vita kuu ya pili ambako Ujerumani penyewe ilivamiwa na wanajeshi wa Uingereza gavana Twining wa Tanganyika alikumbuka habari za fuvu akatembelea Ujerumani na kutazama mafuvu ya makumbusho ya Bremen.

Katika mkusanyiko wa fuvu 2000 zilikuwa 84 zenye namba zilizoonyesha zilitoka kiasili katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Hapa alizipanga kufuatana na ukubwa na kutazama zile zilizokuwa na vipimo vya karibu na ndugu za Mkwawa aliowahi kupima kabla ya safari yake. Hapa aliteua fuvu yenye shimo kwa sababu taarifa ya kale ilisema Mkwawa alijiua kwa kujipigia risasi kichwani.

Kulikuwa na uhalali gani kwa askari aliyejiua kutambulika kama "shujaa"?

ANGALIZO: Mimi Infantry Soldier sio askari jeshi wala mtumishi wa ofisi yoyote ya serikali bali ni raia mwema ninayeipenda sana Tanzania. Hili jina nilijpa tu kutokana na changamoto kadhaa nzito nilizowahi kuzipitia katika maisha yangu.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Saddam was an exception, yule jamaa anahukumiwa kifo akaanza kuongea uzalendo hapo hapo, alipewa nafasi ya kujitetea mahakamani asiuwawa alijibu hivi
"Saddam Hussein ni mkubwa mno kutetewa na Binadamu yeyote, hata Saddam Hussein mwenyewe hana hadhi ya kumtetea Saddam Hussein bali Mungu tu ndiye mwenye hadhi ya kumtetea saddam Hussein" Hivyo usimfananishe Saddam na mtu yeyote maana yule mzee alikuwa mgumuwa mno, imagine unaletewa taarifa wanao wawili na mjikuu wameuwawa wewe unauliza "je walipambana ?" unajibiw ndio alafu unajibu "basi wamekufa kishukaa"
turudi kwa mkwawa sasa, Mkwawa namuona ni shujaa maana kuliko ateswe na maadui zake akaona bora ajiue tu, alikuwa shujaaa kwa maana hakutaka kuwapigia magoti wazungu na hata yeye alipowateka wazungu aliwaua so aliona l
abda kuuliw na adui wake ni uzembe
 
Habari za wakati huu ndugu zangu wa humu JamiiForums.

Kulikuwa na uhalali gani wa Chief Mkwawa kutambulika kama "shujaa"? Kamwe hakuna askari anayeweza kuitwa shujaa kwa kuogopa adui kisha kujiua mwenyewe.

Mbona Muamar Gadaffi wa Libya na Saddam Hussein wa Iraq hawakujiua kabla ya kukamatwa na wazungu? Mkwawa alikuwa shujaa ama askari muoga?

UOGA SIO SIFA NJEMA YA MWANAUME MPIGANAJI
=====
Uoga ni tabia ambayo hofu nyingi humzuia mtu kupambana na hatari au kukabiliana na adui. Uoga unaonyesha uwezo wa mtu kukosa tabia ya ujasiri wakati wa changamoto. Katika kanuni za kijeshi za nchi nyingi hapa duniani, uoga katika vita ni sawa sawa na uhalifu.

Vitendo vya uoga, kwa muda mrefu tangia vita ya kwanza ya dunia, vimeadhibiwa na sheria za kijeshi, ambazo inafafanua vema makosa yanayohesabika kama uoga, ikiwa pamoja na kumkimbia adui au kujisalimisha kwa adui pasipo kupata amri kutoka kwa wakubwa. Wale ambao walikamatwa walikuwa, mara kwa mara, wakipelekwa mahakamani na adhabu ya vitendo kama hivyo kwa kawaida huwa ni kali sana.

Siku zote ulimwengu umewaheshimu majasiri na kuwalaani waoga. Kuwa jasiri ni muhimu kwa mwanamume kama vile kuwa msafi kwa mwanamke, na muoga kati ya wanaume ana sifa mbaya kama kahaba kati ya wanawake.

Kujiua huitwa ni uoga kwa sababu inahitaji ujasiri wa hali ya juu sana ili uweze kuishi katika dunia iliyojaa kila aina ya changamoto, inahitaji mtu kuwa na mtazamo sahihi juu ya maisha na utulivu mkubwa wa akili. Pamoja na shinikizo na shida zote, vuta nikuvute za maisha ambavyo tunakabiliwa navyo, baadhi ya waoga huamua kuwa na mawazo hasi na kushindwa kupambana tena na badala yake kuchagua kufa.

KWA UFUPI SANA KUHUSU KIFO CHA CHIEF MKWAWA
=====
Kichwa cha mtemi kinasemekana kilikatwa na Wajerumani na kutumwa Berlin kilipohifadhiwa katika makumbusho, awali Berlin na baadaye Bremen. Waingereza waliochukua utawala wa koloni mwaka 1918 baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia walitaka kuonekana kama mabwana wema.

Mkuu wa serikali ya kikoloni ya Tanganyika alipendekeza kurudisha fuvu kwa sababu Wahehe walishirikiana na Waingereza wakati wa vita. Hivyo kuna kipengele 246 katika mkataba wa Versailles kinachosema: "Katika muda wa miezi 6 baada ya kuthebitishwa kwa mkataba huu. Ujerumani itakabidhi fuvu ya Sultani Mkwawa iliyohamishwa kutoka Afrika ya Mashariki ya Kijerumani na kupelekwa Ujerumani kwa serikali ya Mfalme wa Uingereza.

Wajerumani walikataa habari za fuvu hii na Waingereza waliamua ya kwamba ilishindikana kuikuta. Lakini baada ya vita kuu ya pili ambako Ujerumani penyewe ilivamiwa na wanajeshi wa Uingereza gavana Twining wa Tanganyika alikumbuka habari za fuvu akatembelea Ujerumani na kutazama mafuvu ya makumbusho ya Bremen.

Katika mkusanyiko wa fuvu 2000 zilikuwa 84 zenye namba zilizoonyesha zilitoka kiasili katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Hapa alizipanga kufuatana na ukubwa na kutazama zile zilizokuwa na vipimo vya karibu na ndugu za Mkwawa aliowahi kupima kabla ya safari yake. Hapa aliteua fuvu yenye shimo kwa sababu taarifa ya kale ilisema Mkwawa alijiua kwa kujipigia risasi kichwani.

Kulikuwa na uhalali gani kwa askari aliyejiua kutambulika kama "shujaa"?

ANGALIZO: Mimi Infantry Soldier sio askari jeshi wala mtumishi wa ofisi yoyote ya serikali bali ni raia mwema ninayeipenda sana Tanzania. Hili jina nilijpa tu kutokana na changamoto kadhaa nzito nilizowahi kuzipitia katika maisha yangu.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Una uhakika gani kuwa Chifu Mkwawa alijiua kwa kujipiga risasi??.
 
Huyu hakuwa shujaa kabisa
Kwanza alikuwa anafanya biashara ya watumwa anauza waafrika wenzie ili apate risasi,shanga,nguo,mvinyo
Halafu sio kwamba alipigana na wahehe tu ila makabila mengine madogo ya pembeni yaliunganisha nguvu wakapigana na mjerumani.

Tatu ujio wa wangoni ulileta effect nyingi sana mbaya na nzuri ikiwemo ku adopt mbinu zao za
Kivita kwahivyo mkwawa baada ya kuchapwa na wangoni aka copy military technic zao ikiwemo cow horn na short spear. Long shield.

Kingine alikuwa anapata ufadhili kutoka kwa waarabu koko waliokuwa wanafanya bado bishara ya utumwa kimya kimya na wajerumani walikuwa kama wanazibia.
Mmojawapo ni abushiri na bwana heri hawa walikuwa sponsors wa mkwawa.

Pia mauwaji ya delegates wa mkwawa yalichangia kuibua Vita .nae akamuua kamanda wa kijerumani katili kuliko wote Emily von zellywiski
Infantry Soldier
 
Mpaka sasa bado ulimwengu haujui nini kilimkuta Adolph Hitler. Miongoni mwa majeshi ya washirika yalioungana katika kuung'oa utawala wa Nazi, kuna wanaodhani Marekani ilimficha kama ambavyo wanadai Osama amefichwa
Hitler alijiua na abaada ya hapo wasaidizi wake wakachoma moto mwili wake, hii nimeisoma bbc news mwezi uliyopita.
Ngoja niitafute nikuwekee link.
 
Ni maneno ya nani hayo mkuu? Inawezekana alifichwa na Uingereza ila wakasingizia kuwa alijiua.
 
Hapana, Hitler alijiua kwa kujipiga risasi kwenye handaki lake. Ila kabla hajajiua alimuagiza dereva wake amfuatia Lita 200 za petrol, Ila dereva huyo alipata Lita 180 ambazo aliambiwa aziweke nje ya handaki hilo. Na mpaka mda huwo Hitler hakumwambia kazi ya mafuta hayo.
Ingawaje baada ya Hitler kujipiga risasi wasaidizi wake na walinzi wake walijiongeza wakaamua kuuchoma mwili wa Hitler kwa petrol hiyo ila haukuungua wote, hivyo wakauzika, na ndipo warusi walipo wafikia na kufukua mwili huyo na kuondoka nao
 
Back
Top Bottom