Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asante sana bossWewe ni mjinga....
Acha uoga mwanaume hujibu hoja kwa hoja na sio kuvimbisha mashavu[emoji28]Unajaribu kutuchokonoa. Utapata unachotaka hata kama haukijui.
Kwani ukigeukwa na wananchi wako ndio unashindwa kujiua? Kuna uhusiano gani kati ya kutojiua na kutokuungwa mkono na wananchi?Situation za Gaddafi na Saddam haziwezi kulinganishwa na Mkwawa wao wote waligeukwa na wananchi wao wenyewe na hakuna aliyekamatwa na mzungu
Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
Mkwawa alishindwa vita vs German akaona hataweza vumilia humiliation mbele ya watu wake akaamua kujitoa uhai!hawa wengine waligoma kusoma alama za nyakatiKwani ukigeukwa na wananchi wako ndio unashindwa kujiua? Kuna uhusiano gani kati ya kutojiua na kutokuungwa mkono na wananchi?
Sawa mkuu
Hili lengo limeandikwa wapi katika historia na mimi nisome?Kwa sababu lengo la Wajerumani ilikuwa kumkamata akiwa hai na kumdhalilisha.
Hahahahaaaa eti walishindwa kusoma alama za nyakati karne hii ya 21 ya sayansi na teknolojia.Mkwawa alishindwa vita vs German akaona hataweza vumilia humiliation mbele ya watu wake akaamua kujitoa uhai!hawa wengine waligoma kusoma alama za nyakati
Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
Asante sana boss...Una ufahamu mdogo sana
Infantry soldier kama kibaraka vile. Hata hatumuelewi. Linapokuja story chanya za waafrika anaponda hadi anataka kufiapo. Sijawahi ona wachina au wazungu wanaponda story zao. Tena wanadiliki hata kudanganya story ili waonekane wanaweza. Lakini muda ume wa prove wrong. Hadi sasa mwafrika ndo bado anaonekana anafanya vizuri physically and mentally. Hii utaiona kwenye sports na area nyingi tu. Ila kwa sababu wanao control dunia ni wahabeshi. Basi favour yote inaelekea kwao. Kuna blacks wengi wanafanya the best ila wanafunikwa.Una ufahamu mdogo sana..usiku mwema ASKARI
Kibaraka wa nani mkuu?...Infantry soldier kama kibaraka vile.
Jibu hapo ni ndio. Unaweza kufahamu pia kww urahisi tu; vita ya iraq usa imepiganwa wakati teknolojia ikiwa wazi kabsa, pili, ni vita ambayo haijazidi miaka 3. Vita ya mkwawa vs ujerumani imepiganwa kwa takribani miaka 8; wajerumani walikuwa na teknolojia kubwa zaidi kuliko mkwawa, unàweza kurejea tu chanzo cha jina Tosamaganga inatosha kujua ufinyu wa teknolojia ya mkwawa vs ujerumani.Mbona Saddam Hussein hakujiua? Ina maana himaya ya wahehe ya miaka hiyo ya zamani ilikuwa na siri nzito kuzidi Iraq ya mwaka 2003?...
Yaleyale ya OKonko..kujinyonga baada ya watu wake kusema si kila cha mzungu ni kibaya.Habari za wakati huu ndugu zangu wa humu JamiiForums.
Kulikuwa na uhalali gani wa Chief Mkwawa kutambulika kama "shujaa"? Kamwe hakuna askari anayeweza kuitwa shujaa kwa kuogopa adui kisha kujiua mwenyewe.
Mbona Muamar Gadaffi wa Libya na Saddam Hussein wa Iraq hawakujiua kabla ya kukamatwa na wazungu? Mkwawa alikuwa shujaa ama askari muoga?
UOGA SIO SIFA NJEMA YA MWANAUME MPIGANAJI
=====
Uoga ni tabia ambayo hofu nyingi humzuia mtu kupambana na hatari au kukabiliana na adui. Uoga unaonyesha uwezo wa mtu kukosa tabia ya ujasiri wakati wa changamoto. Katika kanuni za kijeshi za nchi nyingi hapa duniani, uoga katika vita ni sawa sawa na uhalifu.
Vitendo vya uoga, kwa muda mrefu tangia vita ya kwanza ya dunia, vimeadhibiwa na sheria za kijeshi, ambazo inafafanua vema makosa yanayohesabika kama uoga, ikiwa pamoja na kumkimbia adui au kujisalimisha kwa adui pasipo kupata amri kutoka kwa wakubwa. Wale ambao walikamatwa walikuwa, mara kwa mara, wakipelekwa mahakamani na adhabu ya vitendo kama hivyo kwa kawaida huwa ni kali sana.
Siku zote ulimwengu umewaheshimu majasiri na kuwalaani waoga. Kuwa jasiri ni muhimu kwa mwanamume kama vile kuwa msafi kwa mwanamke, na muoga kati ya wanaume ana sifa mbaya kama kahaba kati ya wanawake.
Kujiua huitwa ni uoga kwa sababu inahitaji ujasiri wa hali ya juu sana ili uweze kuishi katika dunia iliyojaa kila aina ya changamoto, inahitaji mtu kuwa na mtazamo sahihi juu ya maisha na utulivu mkubwa wa akili. Pamoja na shinikizo na shida zote, vuta nikuvute za maisha ambavyo tunakabiliwa navyo, baadhi ya waoga huamua kuwa na mawazo hasi na kushindwa kupambana tena na badala yake kuchagua kufa.
KWA UFUPI SANA KUHUSU KIFO CHA CHIEF MKWAWA
=====
Kichwa cha mtemi kinasemekana kilikatwa na Wajerumani na kutumwa Berlin kilipohifadhiwa katika makumbusho, awali Berlin na baadaye Bremen. Waingereza waliochukua utawala wa koloni mwaka 1918 baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia walitaka kuonekana kama mabwana wema.
Mkuu wa serikali ya kikoloni ya Tanganyika alipendekeza kurudisha fuvu kwa sababu Wahehe walishirikiana na Waingereza wakati wa vita. Hivyo kuna kipengele 246 katika mkataba wa Versailles kinachosema: "Katika muda wa miezi 6 baada ya kuthebitishwa kwa mkataba huu. Ujerumani itakabidhi fuvu ya Sultani Mkwawa iliyohamishwa kutoka Afrika ya Mashariki ya Kijerumani na kupelekwa Ujerumani kwa serikali ya Mfalme wa Uingereza.
Wajerumani walikataa habari za fuvu hii na Waingereza waliamua ya kwamba ilishindikana kuikuta. Lakini baada ya vita kuu ya pili ambako Ujerumani penyewe ilivamiwa na wanajeshi wa Uingereza gavana Twining wa Tanganyika alikumbuka habari za fuvu akatembelea Ujerumani na kutazama mafuvu ya makumbusho ya Bremen.
Katika mkusanyiko wa fuvu 2000 zilikuwa 84 zenye namba zilizoonyesha zilitoka kiasili katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Hapa alizipanga kufuatana na ukubwa na kutazama zile zilizokuwa na vipimo vya karibu na ndugu za Mkwawa aliowahi kupima kabla ya safari yake. Hapa aliteua fuvu yenye shimo kwa sababu taarifa ya kale ilisema Mkwawa alijiua kwa kujipigia risasi kichwani.
Kulikuwa na uhalali gani kwa askari aliyejiua kutambulika kama "shujaa"?
ANGALIZO: Mimi Infantry Soldier sio askari jeshi wala mtumishi wa ofisi yoyote ya serikali bali ni raia mwema ninayeipenda sana Tanzania. Hili jina nilijpa tu kutokana na changamoto kadhaa nzito nilizowahi kuzipitia katika maisha yangu.
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Ndio mkuu, sio kila cha mzungu ni kibaya ndio maana tunatumia internet yao.Yaleyale ya OKonko..kujinyonga baada ya watu wake kusema si kila cha mzungu ni kibaya.
Suala la kujitoa roho halina uhusiano wowote na hii justification yako mkuu. Kujiua ni uamuzi wa mtu unaohitaji risasi moja au mbili tu kukatisha uhai bila kujali usasa ama uzamani wa teknolojia.Jibu hapo ni ndio. Unaweza kufahamu pia kww urahisi tu; vita ya iraq usa imepiganwa wakati teknolojia ikiwa wazi kabsa, pili, ni vita ambayo haijazidi miaka 3. Vita ya mkwawa vs ujerumani imepiganwa kwa takribani miaka 8; wajerumani walikuwa na teknolojia kubwa zaidi kuliko mkwawa, unàweza kurejea tu chanzo cha jina Tosamaganga inatosha kujua ufinyu wa teknolojia ya mkwawa vs ujerumani.
Sio kila jambo ni la kusifia mkuu. Challenges lazima ziwepoInfantry soldier kama kibaraka vile. Hata hatumuelewi. Linapokuja story chanya za waafrika anaponda hadi anataka kufiapo. Sijawahi ona wachina au wazungu wanaponda story zao. Tena wanadiliki hata kudanganya story ili waonekane wanaweza. Lakini muda ume wa prove wrong. Hadi sasa mwafrika ndo bado anaonekana anafanya vizuri physically and mentally. Hii utaiona kwenye sports na area nyingi tu. Ila kwa sababu wanao control dunia ni wahabeshi. Basi favour yote inaelekea kwao. Kuna blacks wengi wanafanya the best ila wanafunikwa.
Hatukatai. Waafrika tuliteleza katika point fulani ya maisha kwa sababu ya roho nzuri za kukaribisha wageni na kuwaheshimu. Sasa tumejifunza kitu kimoja kwamba kumbe roho mbaya inahesabiwa kua akili kwenye dunia ya sasa.
Infantry Soldier! Salute mkuu.Habari za wakati huu ndugu zangu wa humu JamiiForums.
Kulikuwa na uhalali gani wa Chief Mkwawa kutambulika kama "shujaa"? Kamwe hakuna askari anayeweza kuitwa shujaa kwa kuogopa adui kisha kujiua mwenyewe.
Mbona Muamar Gadaffi wa Libya na Saddam Hussein wa Iraq hawakujiua kabla ya kukamatwa na wazungu? Mkwawa alikuwa shujaa ama askari muoga?
UOGA SIO SIFA NJEMA YA MWANAUME MPIGANAJI
=====
Uoga ni tabia ambayo hofu nyingi humzuia mtu kupambana na hatari au kukabiliana na adui. Uoga unaonyesha uwezo wa mtu kukosa tabia ya ujasiri wakati wa changamoto. Katika kanuni za kijeshi za nchi nyingi hapa duniani, uoga katika vita ni sawa sawa na uhalifu.
Vitendo vya uoga, kwa muda mrefu tangia vita ya kwanza ya dunia, vimeadhibiwa na sheria za kijeshi, ambazo inafafanua vema makosa yanayohesabika kama uoga, ikiwa pamoja na kumkimbia adui au kujisalimisha kwa adui pasipo kupata amri kutoka kwa wakubwa. Wale ambao walikamatwa walikuwa, mara kwa mara, wakipelekwa mahakamani na adhabu ya vitendo kama hivyo kwa kawaida huwa ni kali sana.
Siku zote ulimwengu umewaheshimu majasiri na kuwalaani waoga. Kuwa jasiri ni muhimu kwa mwanamume kama vile kuwa msafi kwa mwanamke, na muoga kati ya wanaume ana sifa mbaya kama kahaba kati ya wanawake.
Kujiua huitwa ni uoga kwa sababu inahitaji ujasiri wa hali ya juu sana ili uweze kuishi katika dunia iliyojaa kila aina ya changamoto, inahitaji mtu kuwa na mtazamo sahihi juu ya maisha na utulivu mkubwa wa akili. Pamoja na shinikizo na shida zote, vuta nikuvute za maisha ambavyo tunakabiliwa navyo, baadhi ya waoga huamua kuwa na mawazo hasi na kushindwa kupambana tena na badala yake kuchagua kufa.
KWA UFUPI SANA KUHUSU KIFO CHA CHIEF MKWAWA
=====
Kichwa cha mtemi kinasemekana kilikatwa na Wajerumani na kutumwa Berlin kilipohifadhiwa katika makumbusho, awali Berlin na baadaye Bremen. Waingereza waliochukua utawala wa koloni mwaka 1918 baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia walitaka kuonekana kama mabwana wema.
Mkuu wa serikali ya kikoloni ya Tanganyika alipendekeza kurudisha fuvu kwa sababu Wahehe walishirikiana na Waingereza wakati wa vita. Hivyo kuna kipengele 246 katika mkataba wa Versailles kinachosema: "Katika muda wa miezi 6 baada ya kuthebitishwa kwa mkataba huu. Ujerumani itakabidhi fuvu ya Sultani Mkwawa iliyohamishwa kutoka Afrika ya Mashariki ya Kijerumani na kupelekwa Ujerumani kwa serikali ya Mfalme wa Uingereza.
Wajerumani walikataa habari za fuvu hii na Waingereza waliamua ya kwamba ilishindikana kuikuta. Lakini baada ya vita kuu ya pili ambako Ujerumani penyewe ilivamiwa na wanajeshi wa Uingereza gavana Twining wa Tanganyika alikumbuka habari za fuvu akatembelea Ujerumani na kutazama mafuvu ya makumbusho ya Bremen.
Katika mkusanyiko wa fuvu 2000 zilikuwa 84 zenye namba zilizoonyesha zilitoka kiasili katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Hapa alizipanga kufuatana na ukubwa na kutazama zile zilizokuwa na vipimo vya karibu na ndugu za Mkwawa aliowahi kupima kabla ya safari yake. Hapa aliteua fuvu yenye shimo kwa sababu taarifa ya kale ilisema Mkwawa alijiua kwa kujipigia risasi kichwani.
Kulikuwa na uhalali gani kwa askari aliyejiua kutambulika kama "shujaa"?
ANGALIZO: Mimi Infantry Soldier sio askari jeshi wala mtumishi wa ofisi yoyote ya serikali bali ni raia mwema ninayeipenda sana Tanzania. Hili jina nilijpa tu kutokana na changamoto kadhaa nzito nilizowahi kuzipitia katika maisha yangu.
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Mkuu, labda itoshe tu kusema ya kuwa unaifahamu vema sana historia ya Tanzania.Infantry Soldier! Salute mkuu.
Naomba nami pia nichangiepo tafadhali.
MKWAWA MKWAVINYIKA BIN MUNYIGUMBA! SHUJAA AU MUOGA?
Ushujaa haumaniishi kuwa Utaishi au Utakufa!
Shujaa ni Matendo au Hiba ya Mtu aliyefanya jambo la Ujasiri na Uzalendo kwa Watu wake au Asili yake kwa gharama ambayo hailipiki.
Tuanzie Nchini kwetu, tuna siku ya Mashujaa - Kifupi huwa tunawakumbuka Askari wetu waliokufa na waliosaidia nchi yetu kupigana na kulinda mipaka yetu dhidi ya Fashisti General Amin (Kagera War 1978 -79).
Duniani kote huwakumbuka Mashujaa wao - hasa wale waliopoteza maisha,kuuwawa au kujiua kwa ajili ya Maslahi mapana ya Nchi zao.
Makao Makuu ya Shirika la Ujasusi la CIA - Langley Upo Ukuta wa Mashujaa wanaotambulikana kwa nyota tu na majina yao hubakia siri milele na familia zao hupewa hadithi za uongo juu ya vyanzo vya vifo vya wapendwa wao , na wengine huambatana na majina hasa wale ambao walijihusisha na Overt Operations.
Nyota Huchongwa na Kuwekwa katika Ukuta huo wa Heshima kuwaenzi mashujaa. Ni Maafisa walipoteza maisha katika Mission mbalimbali kwa ajili ya Maslahi mapana ya USA, wengine waliuwawa,kujiua na pengine kutoroka na kuishia kuuwawa cha msingi ulionesha kupambana au kufurukuta na ulifanya hivyo kwa heshima ya Nchi yako au Rais/Mfalme/Taasisi.
Mkwawa Alikufa KISHUJAA, ni Shujaa wa Afrika - Hakukubali Kuchukuliwa Mateka na kama viongozi wengi tu ambao pia walipoona wanaelekea kushindwa walifanya vivyo hivyo. (They defied Surrendering) and became Martyr.
Mwingine ni Cheif ISIKE - Huyu Chief wa Wanyamwezi yeye alijilipua kwa Baruti pamoja na familia yake yote Wakafa, lakini chanzo ni pambano makali kati yake na Wadachi.
Bwana Heri na Cheif Hassan Makunganya hawa waliwapinga wajerumani na kupamabana nao lakini wao hawakujiua walikamatwa na Kunyongwa, Je Kunyongwa na Wajerumani au Kujinyonga wewe mwenyewe kipi ni Ushujaa.
Mkwawa na Isike walifanana katika hoja Moja - Walichukia hata kumuona Mzungu (mgeni) ,Kukamatwa na Mzungu ilikuwa ndio Ishara ya Uoga na Dhaliliko kubwa kwao, hivyo walijiapiza kamwe hawatakuja kukamatwa wala kunyongwa na Wadachi.
Shujaa Mwingine ni Mchg. John Chilembwe wa Malawi - yeye alijua kabisa hawezi kupigana na Wazungu hata kwa masaa 24! Lakini alihakikisha anawaonesha kuwa hawezi kufa kama kondoo lazima aoneshe kuwa na yeye ni Mwanaume - Ingawaje mwishoni aliamua kutimua mbio kuelekea Msumbiji wakamfuatilia na Kumuua.
Yupo Pia Mwenye Machemba Bin Mchakama wa Wayao - yeye aliwaandikia Barua ya Kuwatisha wajerumani kiasi kwamba hawakuamini kama ameandika akiwa anajua alichoandika - Maana alimalizia kwa kusema Kama mnanguvu za kutosha njooni mnitoe!.Aliposikia wanakuja alijaribu kupambana nao,mwisho alipoona mambo magumu akatimkia Msumbiji.
Shujaa ni Yule anayethubutu kupambana, anayeonesha amepambana haijalishi atashinda ama la! Chilembwe alikuwa na msemo wa "Strike a blow and Die"
Mwisho Samson The Great! huyu myahudi akiwa kipofu na mfungwa wa kusaga ngano Gaza,naye alipambana na adui za Israel na kuishia kufa na kuwauwa Wafilisti wengi kuliko aliowahi kuwauwa akiwa huru na anaona.
Wafia Dini wa Uganda! Walipambana na Kabaka Mwanga II na kuishia Kuchomwa kama mishikaki - lakini walitetea Imani yao hawakubadili Msimamo wao Kama Hamisi HK.
WHOEVER STRIKES A BLOW AND DIE FOR THE GREAT CAUSE, IS A HERO.
Asante.
Goodnight too bossUna ufahamu mdogo sana..usiku mwema ASKARI