Kulikuwa na uhalali gani kwa Chief Mkwawa kutambulika kama 'Shujaa?

Hii ni kwa vijana ambao maziwa ya mama yao hayajawaisha mdomoni,,,

Yaani wananuka maziwa mdomoni.
Iko hivi:
Kwenye mbinu za medani, askari akiona yuko hatarini kukamatwa,,,
Na akijua akikamatwa atatoa siri kwa mateso atakayopata
Mbinu ya medani inamtaka

3 atoroke
2 awe na uwezo wa kuhimili mateso
1 Ajiue.
Wengi huchagua mbinu no 1
 
Kama hakuwa shujaa mbn wajerumani walikata kichwa na kuondoka nacho??

Huoni kuwa ule ushujaa wake wa kuwasumbua na kuwaua wazungu, ndio ulikuwa ushujaa wake na ujasiri pia. Maana hata kujiua ni ushujaa wa kutokukiogopa kifo
Kujiua ni uoga wa maisha mkuu na waoga kamwe hawatauona ufalme wa Mungu. Mzalendo hajiua hata siku moja.
 
So wajerumani waliamua kuweka kichwa cha mtu muoga??
Unajua nini maana ya neno TROPHY? Maana yake ni kwamba, "something used as a symbol of success from hunting or war"

For Example: The animal heads on the wall were trophies of his hunting trips.

Soma kamusi hii hapa>>> trophy
 
Hitler nae alikuwa muoga??
Mpaka sasa bado ulimwengu haujui nini kilimkuta Adolph Hitler. Miongoni mwa majeshi ya washirika yalioungana katika kuung'oa utawala wa Nazi, kuna wanaodhani Marekani ilimficha kama ambavyo wanadai Osama amefichwa
 
[emoji28][emoji28] so fuvu la mkwawa kumba ni "trophy" kwann hawakuchukua na mafuvu mengine ya askari waliokufa??
Kwanini video ya kuuwawa kwa Saddam na Gadaffi zimesambaa mitandaoni na sio za askari wengine wa Iraq na Libya? Jibu ni rahisi sana, wao ndio "Commanders In Chief" ikiwa na maana kwamba nchi haiwezi kuingia vitani pasipo wao kuidhinisha.
 
Mkuu, hata kama sisi sio askari acha kutudanganya. Kutoroka ni option au ni jambo ambalo kila anayezidiwa na adui yake anapenda kulifanya?

Mapambayo yakizidi na unaona hauna namna, hapo kutoroka ni lazima na sio option kama ambavyo unataka kutuaminisha hapa mkuu.

Kujiua au kutojiua ndio options lakini kutoroka "is a REFLEX" na inakuja "automatically"
 
Wakati mwingine ni ule uthubutu tu unafanya mtu aitwe shujaa maana wengi hata kuthubutu ni shida.
 
kwanza umeanza kwa kuharibu kudhani israel inaumaalumu wowote ,na sijui imetokeaje kwenye thread za kishujaa,anyway madini hayo yakuletewa,swala la kujiua useme siri nalielewa na mkwawa ni shujaa maana alipambana na wajerumani miaka minne (najua hujui) polini wakiwa wanamzidi technology mbali ,kukamatwa kwake yeye wangekutumia kuwavunja nguvu wahehe ya kimapinduzi maana wangeamua hata kuuburuza mwili wake kila mahali ili kuwakatisha moyo wahehe.
aidha wahehe waliendelea kuwa shida kuwatawala na hata wajerumani kadhaa waliandika kuwa watu wenye kiburi ,wavivu na hasira ,hata mashambani mwao wajerumani waliajiri wakinga na wabena sio wahehe .
 
Mkuu, sasa kama waliweza kuukata kichwa, kwani wangeshindwa kuuburuza kwa maana ulikuwa katika himaya yao tayari. Kwahiyo tuseme Wajerumani hawakuamua tu kufanya hivyo lakini haina uhusiano wowote wa yeye (Mkwawa) kujiua? Au sio mkuu?...
 
Sijategemea wewe kuuliza hilo swali Mkuu, kwani si ulifunzwa kuhusu 'suicide pill'?
 
Hujawahi kusikia msema "kwa shujaa uenda kilio" wewe?[emoji35]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…