Uchaguzi 2020 Kulikuwa na ulazima gani kununua ndege za kibiashara kwa cash kuliko kununua matrekta na kuyagawa kila kijiji ili kulitupa jembe la mkono?

Uchaguzi 2020 Kulikuwa na ulazima gani kununua ndege za kibiashara kwa cash kuliko kununua matrekta na kuyagawa kila kijiji ili kulitupa jembe la mkono?

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Binafsi nimewahi kupanda ndege mara moja tu ukubwani na utotoni sidhani kama nimewahi kupanda. Nililipa 120k tu kwenda Mbeya na kurudi kwa Fast Jet 2015 kabla midege yetu haijapata sifa hizi.

Sasa hizi ndege zimeleta faida kwa kundi lipi kama tangu awali kabla ya ujio wa haya ma bombardier na Airbus za Magufuli huduma bora na rahisi zilikuwepo?

- Je, nauli zimeshuka kwa Watanzania?

-Je,pato linaloingia kupitia hizi ndege ni kubwa kuweza kuboresha sekta ya kilimo au afya?

*Tunaomba hesabu ya mapato na matumizi yatokanayo na hizi ndege.

Magufuli ungenunua trekta kila kijiji, na wananchi wangekuwa wanachangia fedha kidogo tu kwaajili ya Mafuta, repair na ujira wa operator wa tractor ungetukuzwa zaidi na wananchi. Umaskini ungepotea kabisa by reality hapa nchini na vijana wangerudi kijijini kulima.

Kuna mtu mmoja alisema ukijenga nyumba bila baraka ya watoto nyumba hiyo haitakuwa na baraka. Sasa naanza kumwelewa yule mtu .
 
Anapandisha bei za kupanda ndege bila kupandisha mishahara, hapohapo ananyanyasa wafanyabiashara kwa kodi lukuki, sijui alitegemea nani azipande hizo ndege mpaka zilete faida. Hakukuwa na ulazima wa kununua ndege nyingi kwa cash. Meko anatumia vibaya kodi zetu hapaswi kupewa tena kazi.
 
Anapandisha bei za ndege bila kupandisha mishahara, hapohapo ananyanyasa wafanyabiashara kwa kodi lukuki, sijui alitegemea nani azipande hizo ndege. Hakukuwa na ulazima wa kununua cash. Meko anatumia vibaya kodi zetu hapaswi kupewa tena kazi.
Sema tu tupo Afrika, ingekuwa US. huenda angeshitakiwa mtu hapa kwa matumizi mabaya ya fedha za umma.
 
Kulikuwa na ulazima wa kufufua ATCL, kwa sababu ya local connection. Kuna ndege ya Dar Kigoma Tabora ambayo inachukua wastani wa masaa matatu hadi manne. Ruti hii kwa bus ni siku moja na nusu.

Swali la kujiuliza je ATCL ilifufuliwa aje?

Tanzania tupo njia panda kati ya Ubepari na Ujamaa. Hatujui tushike wapi. Mfumo wa ubepari unawapa uhuru wananchi kuchagua bidhaa wanayotaka mfano utachagua kati ya Coastal/Precision/Fastjet au ATC. Tatizo la ubepari linafanya wamiliki wa hizo kampuni kuwa na utajiri mkubwa ambao wanaweza kuutumia kupata wanayotaka kwenye mfumo wa Siasa.

Mfumo wa Ujamaa huwa unaondoa ushindani na mali kumilikiwa na chombo kimoja ambacho ni Serikali. Ujamaa pia hufanya Wananchi kumtegea Kiongozi mmoja mkubwa. Mfano Mao, Kim Jung Un, n.k
 
Binafsi nimewahi kupanda ndege mara moja tu ukubwani, na utotoni sidhani kama nimewahi kupanda. Nililipa 120k tu kwenda Mbeya na kurudi kwa Fast Jet 2015 kabla midege yetu haijapata sifa hizi..
Si mnasema serikali isifanye biashara ambazo Mimi na wewe tunaweza fanya?
Pili mngt yake ya kukodisha na control ingekuwaje??

3.serikali in encourage watu wajiunge in groups ili walime mashamba makubwa na pia wawe na mitaji mikubwa na pia waweze kukopesheka

Sasa wewe una eka 2 au kumi , tractor utakuwa una li under utilise.
 
Sema tu tupo Afrika, ingekuwa US. huenda angeshitakiwa mtu hapa kwa matumizi mabaya ya fedha za umma.
Kama ikatokea chama cha upinzani ikachukua nchi katiba mpya ni jambo la kwanza, pia kuwaondolea kinga viongozi waliofanya ujinga ili wawajibishwe kwa makosa yao.

Kubadirisha sheria kandamizi na kupunguza mrundikano wa kodi kwa wafanyabiashara. Sera za ACT- Wazalendo na CHADEMA ni sera bora na zimepangiliwa kwa kuakisi maisha halisi ya mtanzania na hali ya dunia kiujumla ilivyo kiuchumi.
 
Binafsi nimewahi kupanda ndege mara moja tu ukubwani, na utotoni sidhani kama nimewahi kupanda. Nililipa 120k tu kwenda Mbeya na kurudi kwa Fast Jet 2015 kabla midege yetu haijapata sifa hizi...
Unajua nyuma ya pazaia fastjet ilikuwa na mizengwe gani mpaka ikawa inatoa huduma za bei rahisi? Kwa nini waliondok na ndege zao kukamatwa huku wakiwa na madeni kibao?

Hizi ndege zilizonunuliwa na serikali faida yake utaiona hasa zitapokuwa zinaleta watalii ambao wataliletea taifa pato kubwa tu. Umekariri upuuzi kudhania faida ya hizi ndege ni mpaka wananchi wazipande kwa bei rahisi.
 
Eti kila Kijiji kipewe trekta akili Huna Kuna vijiji Ni wafugaji sio wakulima na Kuna vijiji hawalimi hulima mazao ya kudumu Kama mikorosho ,Chai ,kahawa nk

Kuna vijiji viko maeneo ya milima yenye
Kuna vijiji Ni vya wavuvi hayo matrekta watalima kwenye maji? Chadema hamna akili

Eti kila Kijiji!!!!
 
Back
Top Bottom