Binafsi nimewahi kupanda ndege mara moja tu ukubwani na utotoni sidhani kama nimewahi kupanda. Nililipa 120k tu kwenda Mbeya na kurudi kwa Fast Jet 2015 kabla midege yetu haijapata sifa hizi.
Sasa hizi ndege zimeleta faida kwa kundi lipi kama tangu awali kabla ya ujio wa haya ma bombardier na Airbus za Magufuli huduma bora na rahisi zilikuwepo?
- Je, nauli zimeshuka kwa Watanzania?
-Je,pato linaloingia kupitia hizi ndege ni kubwa kuweza kuboresha sekta ya kilimo au afya?
*Tunaomba hesabu ya mapato na matumizi yatokanayo na hizi ndege.
Magufuli ungenunua trekta kila kijiji, na wananchi wangekuwa wanachangia fedha kidogo tu kwaajili ya Mafuta, repair na ujira wa operator wa tractor ungetukuzwa zaidi na wananchi. Umaskini ungepotea kabisa by reality hapa nchini na vijana wangerudi kijijini kulima.
Kuna mtu mmoja alisema ukijenga nyumba bila baraka ya watoto nyumba hiyo haitakuwa na baraka. Sasa naanza kumwelewa yule mtu .