Kulikuwa na umuhimu gani kwa Chama changu CHADEMA kutengeneza ofisi Mikocheni kwa Bilioni 2 ?

criticism kwa Chadema ni kubwa kuliko kwa watawala waliotengeneza Chimwaga kwa kodi zenu?
Kama mtu alikuwa katika upangaji na akafanikiwa kujenga nyumba yake mwenyewe nadhani anastahili kupongezwa. Gharama za nyumba aachiwe mwenyewe. Maana akijenga yenye thamani ndogo atasemwa na akijenga yenye thamani kubwa napo atasemwa.

Cha msingi mtu amepata kwake basi!!!!!!!
 
Wakiwa na ofisi kinondoni mbovu mbovu mnawasema na ku refer kila mara kuwa hawana ofisi ya hadhi yao, wakijenga/kununua ofisi ya hadhi masaki mnawasema, HIVI KWENU JEMA NI LIPI NYIE ASEE??
 
Ni pesa za wananchi
 
Mmeanza tena. Daah...! Binadamu bwana hasa Watanzania hatuna lililo sawa. Ile ofisi ya mwanzo kutwa mlikuwa mnaiponda Chadema kwa ile ofisi ya ufipa. Wamejenga ofisi nzuri,tayari yameanza tena maneno.
 
Hiyo nyumba haikujengwa na Chadema kama ofisi yao. Ni ama wameamua kupanga sehemu nyingine yenye hadhi au wameiunununua (na huenda kwa mkopo) katika kujiandaa na uchaguzi ujao. Neno acquire halimaanishi built.
 
Kama ofisi ni ya chama nawapongeza sana, maana kile kibanda cha ufipa hapana kwa kweli, ofisi hata choo ni aibu kilikuwa cha ovyo sijawahi ona, niliwaza zile ruzuku zote zilikuwa zinaenda wapi sipati jibu

Bora ACT walivyokuja na kuwanyoosha hatimae wakatia akili kwamba kuwa na ofisi inayoeleweka ni jambo la msingi sababu wao wenyewe wanakaa kwenye mabangaloo vipi ufanyie kazi pagaleni??

Fikiria anakuja mgeni kutoka chama rafiki na unamkaribishia hotelini Johari au Kempinski ama Serena na anondoka hajafika kwenye makao makuu ya chama chako kisa aibu halafu unajinasibu ni chama kikuu cha upinzani??

Hongereni sana kwa hatua hii hata mngesema bilioni 5 ningewaunga mkono maana upigaji ni kawaida yenu lakini kwa hili mnastahili pongezi bila kujali thamani, ila hapo mwanzoni kukaza fuvu mlifanya ujinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…