Samia atosha tukutane2030
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 17,728
- 49,762
Leo sitaki kugusia matendo ya uzinzi yanayofanywa na wake wa watu wakiwa kwenye safari za kikazi au wakiwa kazini. Ninataka nigusie zaidi suala la uwajibikaji ambao mwanamke anapaswa kuwa nao kwa mume wake.
Msije mkasema siijui Biblia — nimesoma vyuo vya Biblia takribani vitatu, vikiwemo vikubwa viwili, na hata kile cha White Horse cha Wasabato. Nimeijua Biblia kwa kina kwanza, ndipo nikafanya uamuzi wa kuwa Mkristo niliyeokoka.
Yesu alipokuwa akifundisha, alizungumzia maisha halisi ya Mkristo na akasisitiza kwamba hapaswi kuwa na nia mbili. Kama Yesu ni Bwana, basi mtu amfuate yeye bila shaka, na nguvu zake zote aziweke kwa Yesu, akijua kwamba ndiye chombo pekee cha kumfikisha mbinguni.
Yesu alitumia mfano wa mwanamke au mtumishi kwa bwana wake/mume wake. Mwanamke anapoolewa, anatakiwa kuwa responsible kwa mume wake kwa masaa 24 kila siku, siku 7 za wiki. Hapasi kupewa majukumu mengine kutoka kwa mtu mwingine tofauti na mume wake — jambo hilo ni sawa na matusi makubwa.
Lakini leo hii tunaona hali kama hii: mke anaajiriwa, anapewa safari ya kikazi Dodoma kwa wiki moja; akirudi, mezani kuna mafaili kibao, anarudi nyumbani saa 4 usiku. Ni kituko, kituko, kituko! Lakini bado mume ana ujasiri wa kumwita huyo “mke wake” 😭😭.
Kesho yake anaambiwa, “Kesho jioni unatakiwa uwe Mtwara,” naye chap! Anaitika na kutii bila kusita. Wewe bado una ujasiri wa kumwita mke wako?
Kama uko hivyo, basi hujui maana ya neno mke.
Na pia hujui maana ya neno mume.