Mkuu huu mchezo umetengenezwa hivi karibuni baada ya jamhuri kuona mwenendo wa huyu jaji wakamuwahi kabla hajasoma hukumu ndogo ya leo, kama asingepewa uteuzi naamini angekuwa na hukumu tofauti leo.
Ule uteuzi katikati ya kesi ndio ulioleta yote haya, toka mwanzo mpaka kufikia pale kusubiri hukumu ya kesi ndogo huyu jaji alikuwa anaenda vizuri kabisa, tatizo nahisi walimshtukia mwenendo wake wakaona wampoze na rushwa ya cheo.
Hukumu aliyosoma leo ni ya ajabu, ametumia maneno "kwa maoni yake" kwenye kila hoja aliyoanzisha badala ya kuangalia sheria inasema kitu gani, bado sijakata tamaa naamini haki haijifichi, siku zote huchomoza kama jua la asubuhi.
Kitendo cha Samia kutoa uteuzi kwa huyu jaji, nikiunganisha na ile interview yake BBC kwamba kuna ushahidi wa kumfunga Mbowe, napata picha halisi ya aina ya kiongozi tuliyenaye regardless ya jinsia yake na vilemba.