Kulingana na ushahidi wa kesi ndogo ndani ya kesi kubwa uliotolewa, Je unadhani maelezo ya Adamoo aliyoandikisha polisi yatapokelewa kama ushahidi..?

Kulingana na ushahidi wa kesi ndogo ndani ya kesi kubwa uliotolewa, Je unadhani maelezo ya Adamoo aliyoandikisha polisi yatapokelewa kama ushahidi..?

Kwa upande wangu baada ya ufuatiliaji wa mwenendo mzima wa shauri hili dogo,Ninaona upande wa utetezi utatoboa.
 
Tukuulize wewe unaehudhuria mahakamani kama ulivyokwisha jinasibu.

Au kama wewe ni jaji basi toa hukumu tu usisumbue watu vichwa.

Ila kama kweli unahudhuria mahakamani rejea pale shahidi alipoonyesha makovu miguuni,mikononi na kichwani huku wakiomba asioneshe yaliyofichwa maungoni.

Asubuhi njema
Ushahidi una mikanganyiko
1. Ushahidi unaonesha waliteswa.
Japo shahidi ameonesha makovu ila ajabu amesema yapo mapya na ya zamani mahakama itachagua.

2. Shahidi ameonesha tena kwa kuhojiwa na wakili wa serkali kuwa alisaini pasipo mateso yapo baadae alisema kwenye Re examination kuwa alitishwa na Kingai, na kitendo cha kuwa na pingu ni mateso.

3. Hatari zaidi ni pale shahidi amedai akili yake haiko sawa kwa ajili ya Battle confusion, na wakili wa serkali kuiita kama mental disoder,iliyosabibishwa na utumiaji wa madawa ya kulevya kupita kiasi. Hivyo kuwa wakati akili yake haikumbuki mambo kisawasawa.
Yote kwa Yote HAKI ITENDEKE
 
Huo moto wa katiba unasubiri hadi kesi iishe? Isipoisha karibuni basi moto wa katiba nao haupo?? Upinzani wa TZ ni majanga matupu, ni ubatili na kujilisha upepo. Kesi itaisha na hakutakuwa na moto wa katiba wala bibi ya moto wa katiba, hakuna mpinzani mwenye guts za kuanzisha moto wowote hapa TZ, tuna wapinzani wa kuropoka na kupiga makelele nyuma ya keyboard!! Kama kulikuwa kuna jambo la wapinzani kuwasha huo moto unaosema basi ilibidi wauwashe mwenyekiti wao aachiwe, nini kimetokea?? Kwa sasa wanaogopa hata kuvaa Tshirt zao nyekundu mahakamani...
Unataka wapigane na kichaa mwenye rungu wakiwa mikono tupu?
Hii kesi ndani ya kesi inawaumbueni!
Labda 'mtashinda' kwa kuvuruga kesi tu. Lakini mbele ya jamii mmeshashindwa na mtalegea zaidi.
 
Sijui kwa nini judge asisimamishe hii kesi maana Mpaka sasa tayari amekwisha sikia mengi ya kumfanya aamue...ya nini kuendelea kuwahoji mashahidi wengine waliobaki ili hali waliobaki wote watakuja kusema au ku collaborate yote ya ushahidi wa utetezi? Sioni kama kuna haja ya kuendelea maana amekwisha sikia mengi tayari Mpaka sasa na anaweza kutoa maamuzi kwa yale yote aliyoyasikia...

serikali wamefunga ushahidi tayari... au labda ni kuwaruhusu waendelee ili mawakili waendelee kula fedha za umma tu kama akina kingai na Mahita?

Au labda ni kuwaruhusu cdm waendelee tu kusema halafu judge aseme ushahidi unapokelewa halafu kesi kubwa ya Msingi inaendelea na tayari mashahidi wa chadema wanakuwa wameisha na hakuna jipya?

Je kamanda Sirro ataitwa katika hii kesi ndogo au ni katika kesi kubwa tu? Nasikia huwa anatuma wawakilishi tu - MaRPC wamuwakilishe, sijui hii itakuwaje Sirro akitaka hivyo?

Kesi yote Mpaka sasa ni ya kupoteza muda tu na kuwasumbua watuhumiwa... ikiisha tu, moto wa katiba mpya utarudi na hapo ndio utakuwa mwanzo wa vurugu kati ya JWTZ, polisi na wananchi... subiri tu... ndio hayo yanakuja kutokea, hata wakifungwa, ni hayo hayo maana JWTZ wamedharirishwa vibaya sana na hawa polisi uchwara wasio jua hata miongozo yao ya kazi...

Issue Kubwa kwa judge Kuamua ni je kutokufuata miongozo ya kazi kunaifanya hiyo kazi kuwa batili? Ni Hilo tu ndilo linalotakiwa kuamuliwa mengine yote ni Isidingo...
Jeshi limedhalilishwa vya kutosha...
Polisi wameonesha hawajali cha komandoo wala 92KJ wala nani wa jeshini. Wanawasulubu na kuwapoteza kama kawa.
Alafu; mbona trend inaonesha wakitokea mission zao Tazara inawahusu?
 
Mahita alinichekesha sana.Kibatala alimuuliza alitumia PGO katika ukamataji ule?Mahita akajibu kuwa hajawahi kutumia PGO katika ukamataji wake wowote ule.

Kibatala alichanganywa na jibu hili ikabidi amuombe jaji ruhusa ya kuishia hapo na akaenda kukaa kabisa.Baada ya ishu hii ya mahita upande wa jamhuri ilibidi wafunge upande wa mashahidi.It was a big blow.
Hahahahahh
 
Ushahidi una mikanganyiko
1. Ushahidi unaonesha waliteswa.
Japo shahidi ameonesha makovu ila ajabu amesema yapo mapya na ya zamani mahakama itachagua.

2. Shahidi ameonesha tena kwa kuhojiwa na wakili wa serkali kuwa alisaini pasipo mateso yapo baadae alisema kwenye Re examination kuwa alitishwa na Kingai, na kitendo cha kuwa na pingu ni mateso.

3. Hatari zaidi ni pale shahidi amedai akili yake haiko sawa kwa ajili ya Battle confusion, na wakili wa serkali kuiita kama mental disoder,iliyosabibishwa na utumiaji wa madawa ya kulevya kupita kiasi. Hivyo kuwa wakati akili yake haikumbuki mambo kisawasawa.
Yote kwa Yote HAKI ITENDEK
Nilichoelewa ... Shadidi alihojiwa (specifically kuhojiwa) bila mateso lakini ali sign maelezo kwa kutishwa/kuteswa .... maelezo aliyoyatoa bila kutishwa yaliandikwa na kutayarisha pasipo kushuhudia
 
Unataka wapigane na kichaa mwenye rungu wakiwa mikono tupu?
Hii kesi ndani ya kesi inawaumbueni!
Labda 'mtashinda' kwa kuvuruga kesi tu. Lakini mbele ya jamii mmeshashindwa na mtalegea zaidi.
Hahaha! Mnapenda sana ushabiki na kuamini hearsay!! Hata mimi naweza kujitokeza na nikasema NIMETESWA SANA ili kutafuta huruma ya Umma! Kuna jambo rahisi duniani kama kutunga na kusema uongo? And kuna watu waongo, wafitini na wazushi zaidi ya wanaojiita wapinzani TZ? BTW siyo wapinzani wa kweli, ni wasaka tonge tu, siku wakitupiwa hilo tonge basi na kelele zote zinaisha
 
Una utaalamu wowote wa Sheria? Kama huna basi kuwa na subira, muda ndiyo utatoa majibu, sidhani kama hapa JF utapata jibu sahihi zaidi ya mihemko ya ki CCM na CDM.
Hapana, mimi si mwanasheria kitaaluma lakini ninazo basics za sheria and more over, ni kuwa, wote tunafuatilia hatua kwa hatua mwenendo wa kesi yote mpaka hatua hii...

Ninachotaka watu waseme ni siyo kutoa hukumu bali kutoa maoni yao kulingana na walichoona kwa macho yao na kusikia wenyewe kwa masikio yao...

Nadhani hii haihitaji uwe mtaalamu wa sheria...
 
Hahaha! Mnapenda sana ushabiki na kuamini hearsay!! Hata mimi naweza kujitokeza na nikasema NIMETESWA SANA ili kutafuta huruma ya Umma! Kuna jambo rahisi duniani kama kutunga na kusema uongo? And kuna watu waongo, wafitini na wazushi zaidi ya wanaojiita wapinzani TZ? BTW siyo wapinzani wa kweli, ni wasaka tonge tu, siku wakitupiwa hilo tonge basi na kelele zote zinaisha
Sasa nimekulewa kuwa kumbe wewe ndiyo tatizo maana unatoa maoni yako ukiongozwa na pressure na emotion za itikadi za kisiasa na bila shaka wewe ni mwanaCCM, au siyo..?

Kumbuka, hili suala linawahusu watu na wako mahakamani. Usitoe maoni yako kuhusu kesi na mambo ya kisheria kwa kuwa na mtazamo wa;

".....hawa si wapinzani tu, au waoinzani wenyewe si lolote wala chochote..."

Ukiwa na mtazamo huu, you will absolutely miss the bull na bila shaka utajifunga mwenyewe kujipatia ufahamu wa baadhi ya mambo kupitia jambo hili...
 
Wengi tunahudhuria mahakamani kusikiliza kesi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake watatu .

Wengine tunafuatilia mitandaoni hatua kwa hatua mwenendo wa kesi nzima....

Kwa ambao hawajui au hawakumbuki au kusahau ni kuwa, kinachoendelea sasa ni kesi ndogo ndani ya kesi kubwa (trial within a trial)...

Kinachobishaniwa ni aidha maelezo ya mshitakiwa wa 1 Adamoo na wenzake waliyoyatoa polisi yapokelewe au yasipokelewe kama kielelezo cha ushahidi upande wa mashitaka...

UPANDE WA MASHITAKA, unadai yapokelewe kwa sababu yalichukuliwa kwa utaratibu wa kawaida kwa mujibu wa sheria na PGO na watuhumiwa kusaini wenyewe kwa hiari yao...

UPANDE WA UTETEZI NA WASHITAKIWA WENYEWE, unapinga yasipokelewe kwa sababu unadai maelezo hayo yalichukuliwa kinyume cha sheria (chini ya shinikizo la mateso makubwa kwa watuhumiwa) kama njia ya kuwalazimisha kukubali na kusaini maelezo ambayo hawajui yameandikwa na nani...!!

Hii ndiyo sababu upande wa mashitaka waliwekewa "OBJECTION" na washitakiwa (utetezi) katika hili na kuzaa kesi ndogo ndani ya kesi kubwa na ndiyo inayosikilizwa sasa...

Ni katika hatua hii ya kesi hii ishu ya PGO imezuka kwa namna ya kipekee sana na watu kujua kumbe polisi wanapaswa kutekeleza wajibu wao wa kipolisi wa kila siku ikiwemo kukamata na kuhoji watuhumiwa, kuwasafirisha kutoka eneo moja kwenda jingine nk nk kwa mujibu wa PGO...!!

Kwa vyovyote vile itakavyokuwa, maamuzi yoyote ya kesi hii ndogo ndiyo yàtakayotoa uelekeo wa kesi kubwa ambayo huko mbele tutamkuta kinara anayelengwa kuangamizwa au kufungwa (mshtakiwa namba 4, yaani Mh. Freeman A. Mbowe)...

MASWALI YA KUTUONGOZA KATIKA MJADALA HUU NI HAYA;

1. Je, mpaka hatua hii kwa wote mnaofuatilia kesi hii, na kwa mtazamo wa kila mmoja based on the evidence uliokwisha kutolewa, unadhani objection ya upande wa utetezi itatoboa....?

2. Kwa maelezo ya mshtakiwa namba 1 na 2 ambao pia ndiyo mashahidi wenyewe wa kesi hii ndogo, unadhani wameweza kuishawishi mahakama kuwa ni kweli waliteswa kama njia ya kuwalazimisha kukubali maelezo waliyoyatoa polisi chini ya kiapo cha "onyo?"...

3. Ili kuthibitisha kuwa mtu fulani aliteswa, ukiachilia mbali maelezo ya mdomo kuwa nilipigwa sana na kufanyiwa hivi au vile, ushahidi mkubwa huwa ni alama za makovu ya vidonda katika mwili...

Je, mashahidi walionesha alama zozote zinazoashiria tendo la kupigwa na kuteswa lilitendeka kweli....?

Alamsiki. Karibuni kwa mjadala...

Ni wazi kuwa hali hii:

Utesaji wa Dola - Agenda kubwa Uchaguzi ujao

ilimhusu sana mja wake Mola, bwana Adamoo.

Hakuna asiyeyajua hayo.

Tulipo ule mhimili uliojichimbia zaidi huingilia mingine yote kama utakavyo.

Majaji wetu ni katika wale vigogo wasiolipa kodi. Wanufaika wa zile haramu za ule mhimili mrefu.

Ni kwa sababu hizo hatuna furaha na matokeo yoyote ya hapa mahakamani kwa maana inajulikana ukiukwaji mkubwa wa sheria kwenye kupatikana kwa ushahidi huu ni dhahiri.

Hata hivyo kwa mahakama zetu tenganisha uamuzi sahihi kwa mujibu wa sheria na maamuzi ya mahakama zetu.

Bado si mahakama wala jaji wote hawawajibiki kwa uamuzi wowote watakao ona wao kuwa inafaa na kwa sababu yoyote.

Ni makwetu tu ambako huwezi kulalia mlango wazi.
 
PGO haikufuatwa wakati Police wanatekeleza kazi yao
Ushahidi umedhihirisha pasi na shaka kwamba washitakiwa waliteswa kabla ya kusign maelezo yao
Udhalilishaji mkubwa wa haki kwa washtakiwa & kuwaondolea manhood yao (utu)

Mangai hatoboi - ushahidi wake una mashaka makubwa !!
 
Naona objection ya upande wa utetezi ina nafasi kubwa ya kutoboa kwasababu;

1. Maelezo ya mshtakiwa wa kwanza na wa pili yote yamethibitisha walikamatwa bila kufuata sheria ( PGO) hawakukamatwa bali walitekwa, na zaidi ilithibitika hata polisi wetu hawavijui vizuri vifungu vya kwenye PGO.

2. Polisi walishindwa kujitambulisha kwa watuhumiwa wao ni akina nani (hawakutoa vitambulisho), na watuhumiwa wana makosa gani.

3. Njia iliyotumika kuwakamata, waliwavizia, mmoja kutoka nyuma akamkaba mtuhumiwa na mwingine mbele, ikiwemo kuwafunika usoni na vitambaa (jacket na shuka) huu haukuwa ukamataji bali ni utekaji.

4. Maelezo ya mshtakiwa wa kwanza, alipokamatwa alipigwa na vishikizo vya mkanda kwenye suruali yake vikakatika na bahati nzuri hiyo suruali ndiyo aliivaa siku ya kutoa ushahidi akiwa ameishikiza kwa kamba.

5. Maelezo ya mshtakiwa wa kwanza na wa pili kufanana kwamba polisi baada ya kumkamata mshtakiwa wa kwanza, walimuwekea madawa ya kulevya, na pistol, mshtakiwa wa pili akaona atoe vitu vyake mfukoni mapema ili kuepusha nae asijekuwekewa vitu kama mwenzake.

6. Haki za watuhumiwa wakiwa mikononi mwa polisi zilikiukwa, kwanza polisi waliwabadilishia majina yao ya asili na kuwapa ya bandia, hili lilifanyika ili ndugu wa watuhumiwa wasijue ndugu zao wako kituo gani cha polisi, pili, kunyimwa chakula kwa siku kumi, na tatu, vipigo walivyopata wakiwa mikononi mwa polisi.

Hapa tunaona mshtakiwa wa kwanza alishindwa kutembea kutokana na kipigo akawa anaburuzwa na polisi, na mshtakiwa wa pili, yeye aliamua kuruka ruka ili apunguze maumivu ya kipigo kwa kuamini kwamba, kama angeendelea kukaa muda mrefu bila kufanya mazoezi ndio maumivu ya kipigo cha polisi yangezidi kwake.

- Vipigo, kauli za vitisho zilizotolewa na polisi kwa watuhumiwa, na kunyimwa chakula kwa siku kumi, vinatosha kuonesha kwamba watuhumiwa walitoa maelezo polisi wakiwa na hofu kwa ukatili waliofanyiwa na polisi/ wakiwa hawana afya njema ya akili kutokana na njaa, hivyo waliona bora watoe maelezo au wasaini maelezo waliyokuta yameshaandikwa tayari, ili kuokoa maisha yao.

Mkuu rejea case ya uhaini miaka ya 80s mashahidi wa serikali wakiwa kina Mabere Marando na kina Dr. Mahiga. Washitakiwa kina Hatty MacGhee, na kina Hans Poppe.

Kulikuwa na mawakili wa utetezi wazuri tu (first class) kama kina Murtaza Lakha na kina Muccaddam.

Ushahidi ulikuwa umepatikana kwa mateso kama hivi hivi. Ushahidi ulipokelewa na kutumika mahakamani dhidi ya watuhumiwa pamoja na mapingamizi kama hivi hivi.

Karibu Tanzania ambako bila katiba mpya mihimili mingine inawajibika kwa ule mmoja uliojichimbia zaidi.

Bila katiba mpya hatupaswi kuwa na matumaini, kushangilia au hata kusikitika kwa uamuzi wowote utakaotolewa.

Hata hapa pamoja na facts zote usishangae historia ikijirudia.
 
Naona objection ya upande wa utetezi ina nafasi kubwa ya kutoboa kwasababu;

1. Maelezo ya mshtakiwa wa kwanza na wa pili yote yamethibitisha walikamatwa bila kufuata sheria ( PGO) hawakukamatwa bali walitekwa, na zaidi ilithibitika hata polisi wetu hawavijui vizuri vifungu vya kwenye PGO.

2. Polisi walishindwa kujitambulisha kwa watuhumiwa wao ni akina nani (hawakutoa vitambulisho), na watuhumiwa wana makosa gani.

3. Njia iliyotumika kuwakamata, waliwavizia, mmoja kutoka nyuma akamkaba mtuhumiwa na mwingine mbele, ikiwemo kuwafunika usoni na vitambaa (jacket na shuka) huu haukuwa ukamataji bali ni utekaji.

4. Maelezo ya mshtakiwa wa kwanza, alipokamatwa alipigwa na vishikizo vya mkanda kwenye suruali yake vikakatika na bahati nzuri hiyo suruali ndiyo aliivaa siku ya kutoa ushahidi akiwa ameishikiza kwa kamba.

5. Maelezo ya mshtakiwa wa kwanza na wa pili kufanana kwamba polisi baada ya kumkamata mshtakiwa wa kwanza, walimuwekea madawa ya kulevya, na pistol, mshtakiwa wa pili akaona atoe vitu vyake mfukoni mapema ili kuepusha nae asijekuwekewa vitu kama mwenzake.

6. Haki za watuhumiwa wakiwa mikononi mwa polisi zilikiukwa, kwanza polisi waliwabadilishia majina yao ya asili na kuwapa ya bandia, hili lilifanyika ili ndugu wa watuhumiwa wasijue ndugu zao wako kituo gani cha polisi, pili, kunyimwa chakula kwa siku kumi, na tatu, vipigo walivyopata wakiwa mikononi mwa polisi.

Hapa tunaona mshtakiwa wa kwanza alishindwa kutembea kutokana na kipigo akawa anaburuzwa na polisi, na mshtakiwa wa pili, yeye aliamua kuruka ruka ili apunguze maumivu ya kipigo kwa kuamini kwamba, kama angeendelea kukaa muda mrefu bila kufanya mazoezi ndio maumivu ya kipigo cha polisi yangezidi kwake.

- Vipigo, kauli za vitisho zilizotolewa na polisi kwa watuhumiwa, na kunyimwa chakula kwa siku kumi, vinatosha kuonesha kwamba watuhumiwa walitoa maelekezo wakiwa na hofu kwa ukatili waliofanyiwa na polisi/ wakiwa hawana afya njema ya akili, hivyo waliona bora watoe maelezo au wasaini maelezo waliyokuta yameshaandikwa tayari, ili kuokoa maisha yao.
Vyema sana...

Observation yako iko vizuri na inaonesha unafuatilia hatua kwa hatua shauri hili...

Hata mimi ndivyo hivyo nionavyo...

More over, ushahidi wa upande Wa utetezi kwa mashahidi wao wote uko very consistent na unapatana vizuri. Na kama kuna variation, basi ni ndogo sana...

Hata shahidi wa leo nwanamke (mke wa Adamoo) amethibitisha hili kuwa kila wanachoeleza ni uhalisia na siyo vitu vya kutunga mahali kisha afundishwe kuja kusema uongo. Hili hata asiyesomea psychology anaweza kujua mara moja....

Hii ni tofauti sana na upande wa washitakiwa katika kesi hii ndogo ktk kesi kubwa yaani POLISI....

Hawa wameonesha dhahiri shahiri kuwa wanafanya shughuli zao kwa kutofuata sheria na kutumia madaraka yao vibaya kunyanyasa watu (RAIA) kwa kuwatengenezea makosa kwa malengo yao mabaya na kisha kufungua kesi za uongo. Huu ni uhujumu uchumi 100%....

Hili linathibitishwa na maelezo ya ushahidi wao kukosa consistency kutoka kwa askari huyu hata kwa yule kwa mambo ya kila siku yahusuyo taratibu za kisheria na kikanuni ktk ku - execute majukumu yao ya kipolisi...

Na kwa sababu ya kutozingatia sheria, kila kitu walichokitenda hawa polisi kuanzia ktk kuanzisha shauri hili, ukamataji wa watuhumiwa, kuwahoji, kuwa - detain, kuwapeleka mahakamani na namna walivyofanya juhudi kubwa kutaka shauri hili lisikilizwe gizani ni ishara kuwa everything is vanity (ubatili mtupu) na kwa hiyo hii inathibitisha kuwa MSINGI WA KESI HII NI UONGO na HILA ZA KUKOMOANA TU isikusukumwa na misukumo ya kisiasa nyuma yake....!

Hivi ndivyo nianavyo Mimi na kama maamuzi yatafanyika kwa mujibu wa sheria na siyo "kwa mujibu wa maelekezo toka juu", basi kesi hii imeshakwisha kufikia mwisho mpaja hatua hii...!!!
 
Wengi tunahudhuria mahakamani kusikiliza kesi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake watatu .

Wengine tunafuatilia mitandaoni hatua kwa hatua mwenendo wa kesi nzima....

Kwa ambao hawajui au hawakumbuki au kusahau ni kuwa, kinachoendelea sasa ni kesi ndogo ndani ya kesi kubwa (trial within a trial)...

Kinachobishaniwa ni aidha maelezo ya mshitakiwa wa 1 Adamoo na wenzake waliyoyatoa polisi yapokelewe au yasipokelewe kama kielelezo cha ushahidi upande wa mashitaka...

UPANDE WA MASHITAKA, unadai yapokelewe kwa sababu yalichukuliwa kwa utaratibu wa kawaida kwa mujibu wa sheria na PGO na watuhumiwa kusaini wenyewe kwa hiari yao...

UPANDE WA UTETEZI NA WASHITAKIWA WENYEWE, unapinga yasipokelewe kwa sababu unadai maelezo hayo yalichukuliwa kinyume cha sheria (chini ya shinikizo la mateso makubwa kwa watuhumiwa) kama njia ya kuwalazimisha kukubali na kusaini maelezo ambayo hawajui yameandikwa na nani...!!

Hii ndiyo sababu upande wa mashitaka waliwekewa "OBJECTION" na washitakiwa (utetezi) katika hili na kuzaa kesi ndogo ndani ya kesi kubwa na ndiyo inayosikilizwa sasa...

Ni katika hatua hii ya kesi hii ishu ya PGO imezuka kwa namna ya kipekee sana na watu kujua kumbe polisi wanapaswa kutekeleza wajibu wao wa kipolisi wa kila siku ikiwemo kukamata na kuhoji watuhumiwa, kuwasafirisha kutoka eneo moja kwenda jingine nk nk kwa mujibu wa PGO...!!

Kwa vyovyote vile itakavyokuwa, maamuzi yoyote ya kesi hii ndogo ndiyo yàtakayotoa uelekeo wa kesi kubwa ambayo huko mbele tutamkuta kinara anayelengwa kuangamizwa au kufungwa (mshtakiwa namba 4, yaani Mh. Freeman A. Mbowe)...

MASWALI YA KUTUONGOZA KATIKA MJADALA HUU NI HAYA;

1. Je, mpaka hatua hii kwa wote mnaofuatilia kesi hii, na kwa mtazamo wa kila mmoja based on the evidence uliokwisha kutolewa, unadhani objection ya upande wa utetezi itatoboa....?

2. Kwa maelezo ya mshtakiwa namba 1 na 2 ambao pia ndiyo mashahidi wenyewe wa kesi hii ndogo, unadhani wameweza kuishawishi mahakama kuwa ni kweli waliteswa kama njia ya kuwalazimisha kukubali maelezo waliyoyatoa polisi chini ya kiapo cha "onyo?"...

3. Ili kuthibitisha kuwa mtu fulani aliteswa, ukiachilia mbali maelezo ya mdomo kuwa nilipigwa sana na kufanyiwa hivi au vile, ushahidi mkubwa huwa ni alama za makovu ya vidonda katika mwili...

Je, mashahidi walionesha alama zozote zinazoashiria tendo la kupigwa na kuteswa lilitendeka kweli....?

Alamsiki. Karibuni kwa mjadala...
Kama maamuzi yata andikiwa Ikulu/ Lumumba basi ushahidi wa kubumba wa polisi uta pokelewa. Lakini kama Jaji ana maamuzi yake binafsi, basi hakuna ushahidi utapokelewa.. Na hakuna kesi...
 
Kuweka rekodi sahihi Adamoo ni mshtakiwa namba2 sio 1 na Lingwenya ni mshtakiwa namba 3 sio 2

Mshtakiwa namba 1 ni Bwire
 
Mkuu rejea case ya uhaini mashahidi wa serikali wakiwa kina Mabere Marando na kina Dr. Mahiga. Washitakiwa kina Hatty MacGhee, na kina Hans Poppe.

Kulikuwa na mawakili wa utetezi wazuri tu (first class) kama kina Murtaza Lakha na kina Muccaddam.

Ushahidi ulikuwa umepatikana kwa mateso kama hivi hivi. Ushahidi ulipokelewa na kutumika mahakamani dhidi ya watuhumiwa pamoja na mapingamizi kama hivi hivi.

Karibu Tanzania ambako bila katiba mpya mihimili mingine inawajibika kwa ule mmoja uliojichimbia zaidi.

Bila katiba mpya hatupaswi kuwa na matumaini, kushangilia au hata kusikitika kwa uamuzi wowote utakaotolewa.

Hata hapa pamoja na facts zote usishangae historia ikijirudia.
Ndiyo brazaj, mimi nakubaliana na wewe kabisa, kuwa hilo linaweza kutokea bila shaka....

Hata ikitokea watu hawa wakifungwa kwa kuonewa tu kwa sababu "wenye mamlaka na nguvu za kiserikali" wameamua hivyo, basi hiyo haitaondoa ukweli kuwa HAWA WATU HAWAKUWA NA HATIA...!!

Lakini kubwa ni hili, lazima tujue na kuzingatia kuwa NYAKATI na MAJIRA zimebadilika sana. Nyakati za kesi hiyo ya uhaini ni tofauti kabisa na nyakati hizi tulizopo hizi...

Nakuhakikishia jambo moja kuwa, kesi hakutakuwa na mashinikizo ya kuamua kunyume cha mwenye haki dhidi ya asiyekuwa na haki hata kama Jaji ni CCM kijani kupita majani yenyewe halisi...

Mazingira yatamlazimisha kusimama upande wa haki. Kama huamini, subiri utashuhudia kwa masikio na macho yako...

HAKUNA KESI HAPA hata mtoto mdogo anajua hili...!!
denoo J dudus
 
Mahita alinichekesha sana.Kibatala alimuuliza alitumia PGO katika ukamataji ule?Mahita akajibu kuwa hajawahi kutumia PGO katika ukamataji wake wowote ule.

Kibatala alichanganywa na jibu hili ikabidi amuombe jaji ruhusa ya kuishia hapo na akaenda kukaa kabisa.Baada ya ishu hii ya mahita upande wa jamhuri ilibidi wafunge upande wa mashahidi.It was a big blow.
Hii ilikua ni lini?
 
Back
Top Bottom