Kulingana na ushahidi wa kesi ndogo ndani ya kesi kubwa uliotolewa, Je unadhani maelezo ya Adamoo aliyoandikisha polisi yatapokelewa kama ushahidi..?

Kulingana na ushahidi wa kesi ndogo ndani ya kesi kubwa uliotolewa, Je unadhani maelezo ya Adamoo aliyoandikisha polisi yatapokelewa kama ushahidi..?

Naona objection ya upande wa utetezi ina nafasi kubwa ya kutoboa kwasababu;

1. Maelezo ya mshtakiwa wa kwanza na wa pili yote yamethibitisha walikamatwa bila kufuata sheria ( PGO) hawakukamatwa bali walitekwa, na zaidi ilithibitika hata polisi wetu hawavijui vizuri vifungu vya kwenye PGO.
Mkuu hii naichukua kama reference ntaangalia Jaji atatoa maamuzi gani sijasoma sheria lakini naona kama iko wazi haki ni ipi na batili ni ipi

Nitashangaa tu iwapo maamuzi ya jaji yatakuwa vinginevyo mana hii nchi hii kuna "inavyotakiwa kuwa na ilivyo" Ni vitu viwili tofaut kabisa.
 
Mkuu rejea case ya uhaini miaka ya 80s mashahidi wa serikali wakiwa kina Mabere Marando na kina Dr. Mahiga. Washitakiwa kina Hatty MacGhee, na kina Hans Poppe.

Kulikuwa na mawakili wa utetezi wazuri tu (first class) kama kina Murtaza Lakha na kina Muccaddam.

Ushahidi ulikuwa umepatikana kwa mateso kama hivi hivi. Ushahidi ulipokelewa na kutumika mahakamani dhidi ya watuhumiwa pamoja na mapingamizi kama hivi hivi.

Karibu Tanzania ambako bila katiba mpya mihimili mingine inawajibika kwa ule mmoja uliojichimbia zaidi.

Bila katiba mpya hatupaswi kuwa na matumaini, kushangilia au hata kusikitika kwa uamuzi wowote utakaotolewa.

Hata hapa pamoja na facts zote usishangae historia ikijirudia.
Nitashangaa sana mahakama ikijivua nguo mbele ya umma wa watanzania na serikali ikijivua nguo mbele ya uso wa dunia (mabalozi wa nje wanaohudhuria kesi).

Hii dunia ya leo sio ile ya 1980's.

Ukiangalia mlolongo wa matukio kwenye hii kesi uliotolewa na watuhumiwa pamoja na mke wa mtuhumiwa Lin'gwenya leo, utaona wazi kuna unyama mwingi zaidi waliotendewa watuhumiwa zaidi hata ya kile kilichofikiriwa mwanzo.

Haki za washtakiwa, na haki za binadamu kwa ujumla wake vyote vilikiukwa wakati wa kuwakamata mpaka baada ya kuwakamata, polisi kukiepuka kikombe hiki hata kwa katiba hii tuliyonayo litakuwa ni ajabu la dunia.
 
Ndiyo brazaj, mimi nakubaliana na wewe kabisa, kuwa hilo linaweza kutokea bila shaka....

Hata ikitokea watu hawa wakifungwa kwa kuonewa tu kwa sababu "wenye mamlaka na nguvu za kiserikali" wameamua hivyo, basi hiyo haitaondoa ukweli kuwa HAWA WATU HAWAKUWA NA HATIA...!!

Lakini kubwa ni hili, lazima tujue na kuzingatia kuwa NYAKATI na MAJIRA zimebadilika sana. Nyakati za kesi hiyo ya uhaini ni tofauti kabisa na nyakati hizi tulizopo hizi...

Nakuhakikishia jambo moja kuwa, kesi hakutakuwa na mashinikizo ya kuamua kunyume cha mwenye haki dhidi ya asiyekuwa na haki hata kama Jaji ni CCM kijani kupita majani yenyewe halisi...

Mazingira yatamlazimisha kusimama upande wa haki. Kama huamini, subiri utashuhudia kwa masikio na macho yako...

HAKUNA KESI HAPA hata mtoto mdogo anajua hili...!!
denoo J dudus

Mkuu ninakusoma na ningekwambia ni maombi yangu yasiyokoma kwa Mola ikapate kuwa kama ulivyo andika.

Niweke wazi kuwa hakuna asiyeuona ukweli huo uliouandika. Hii ni kutokea Samia, Sirro, ma W.S, Jaji, Kingai, Mahita na hata mtoto mdogo kama ulivyo sema.

Shida iko hapa:

1. Kuna mhimili unaoingilia mingine kwa mujibu wa katiba hii hii,
2. Majaji ni wanufaika wa moja kwa moja kwenye mhimili huu uliojichimbia zaidi,
3. Majaji ni wateuliwa wa moja kwa moja wa mhimili huu mrefu,
4. Majaji hawawajibiki kwa lolote katika hukumu zao.

Zaidi sana ngoma iko hapa:

Utesaji wa Dola - Agenda kubwa Uchaguzi ujao

Usisahau mkuu tunaishi kwenye jamii ambayo apparently lawlessness ndiyo law yenyewe. Vipi kuwa hajawajibishwa mtu hadi leo pamoja na haya kujulikana bayana?

Kutegemea haki kwenye hali kama hizi hakuna tofauti na kusubiria dodo kwenye mnazi!

Ninataka sana kesi hii itupiliwe mbali lakini haipo foolproof system yenye ku guarantee hilo.
 
Vyema sana...

Observation yako iko vizuri na inaonesha unafuatilia hatua kwa hatua shauri hili...

Hata mimi ndivyo hivyo nionavyo...

More over, ushahidi wa upande Wa utetezi kwa mashahidi wao wote uko very consistent na unapatana vizuri. Na kama kuna variation, basi ni ndogo sana...

Hata shahidi wa leo nwanamke (mke wa Adamoo) amethibitisha hili kuwa kila wanachoeleza ni uhalisia na siyo vitu vya kutunga mahali kisha afundishwe kuja kusema uongo. Hili hata asiyesomea psychology anaweza kujua mara moja....

Hii ni tofauti sana na upande wa washitakiwa katika kesi hii ndogo ktk kesi kubwa yaani POLISI....

Hawa wameonesha dhahiri shahiri kuwa wanafanya shughuli zao kwa kutofuata sheria na kutumia madaraka yao vibaya kunyanyasa watu (RAIA) kwa kuwatengenezea makosa kwa malengo yao mabaya na kisha kufungua kesi za uongo. Huu ni uhujumu uchumi 100%....

Hili linathibitishwa na maelezo ya ushahidi wao kukosa consistency kutoka kwa askari huyu hata kwa yule kwa mambo ya kila siku yahusuyo taratibu za kisheria na kikanuni ktk ku - execute majukumu yao ya kipolisi...

Na kwa sababu ya kutozingatia sheria, kila kitu walichokitenda hawa polisi kuanzia ktk kuanzisha shauri hili, ukamataji wa watuhumiwa, kuwahoji, kuwa - detain, kuwapeleka mahakamani na namna walivyofanya juhudi kubwa kutaka shauri hili lisikilizwe gizani ni ishara kuwa everything is vanity (ubatili mtupu) na kwa hiyo hii inathibitisha kuwa MSINGI WA KESI HII NI UONGO na HILA ZA KUKOMOANA TU isikusukumwa na misukumo ya kisiasa nyuma yake....!

Hivi ndivyo nianavyo Mimi na kama maamuzi yatafanyika kwa mujibu wa sheria na siyo "kwa mujibu wa maelekezo toka juu", basi kesi hii imeshakwisha kufikia mwisho mpaja hatua hii...!!!
Baadhi ya vitu ambavyo vinaonesha consistency ya upande wa utetezi;

- Watuhumiwa kupigwa (Lin'gwenya na mwenzake walikiri hilo) na leo mke wa Lin'gwenya kasema alipomtembelea mumewe Segerea alimkuta ana kovu mkononi.

- Watuhumiwa kukosa chakula kwa muda mrefu, wote wawili walikiri, leo mke wa Lin'gwenya kasema alipomuona mume wake Segerea alimkuta amekonda sana na macho yake yameingia ndani.

- Polisi kutofuata sheria wakati wa ukamataji na ku search nyumba ya mtu, wote wawili watuhumiwa hawakujua kama wanakamatwa na polisi, walivamiwa tu, leo mke wa Lin'gwenya kasema hakujua mume wake alipo na simu yake iliita bila kupokelewa, mwishowe haikupatikana kabisa.

- Watuhumiwa kupewa majina bandia ili ndugu zao wasijue walipo, mtuhumiwa namba mbili alikiri hili akasema aliambiwa ataitwa Johnson John, na mke wa Lin'gwenya na wa Bwire leo wamethibitisha walizunguka vituo vyote vikubwa vya polisi Dsm kuwatafuta waume zao bila mafanikio, coz walipewa majina ya uongo.

Upande wa mashtaka wao wanaegemea zaidi vitu vidogo; mfano.

- Usahihi wa tarehe ya tukio, wanasahau kinacho-matter mahakamani ni tukio likiunganishwa na sheria, sio lilifanyika tarehe gani, hapa judge keshawaambia kuhusu hili.

- Usahihi wa mtuhumiwa (mf. kwamba kama mke hakuwepo nyumbani alijuaje waliokagua walikuwa polisi) wakati mke alishasema afisa upepelezi aliacha namba yake nyumbani ili mke akirudi amtafute.
 
Mkuu hii naichukua kama reference ntaangalia Jaji atatoa maamuzi gani sijasoma sheria lakini naona kama iko wazi haki ni ipi na batili ni ipi

Nitashangaa tu iwapo maamuzi ya jaji yatakuwa vinginevyo mana hii nchi hii kuna "inavyotakiwa kuwa na ilivyo" Ni vitu viwili tofaut kabisa.

Ninakazia:

'"hii nchi hii kuna 'inavyotakiwa kuwa na ilivyo' Ni vitu viwili tofaut kabisa."

Tusilalie mlango wazi bado katiba mpya yenye kushinikiza na kusimamia uhuru kamili wa mihimili hatuna. Si mbaya kufahamu Hangaya asingependa tuwe nayo kabla hajakwiba chaguzi 2024/25.
 
Ndiyo brazaj, mimi nakubaliana na wewe kabisa, kuwa hilo linaweza kutokea bila shaka....

Hata ikitokea watu hawa wakifungwa kwa kuonewa tu kwa sababu "wenye mamlaka na nguvu za kiserikali" wameamua hivyo, basi hiyo haitaondoa ukweli kuwa HAWA WATU HAWAKUWA NA HATIA...!!

Lakini kubwa ni hili, lazima tujue na kuzingatia kuwa NYAKATI na MAJIRA zimebadilika sana. Nyakati za kesi hiyo ya uhaini ni tofauti kabisa na nyakati hizi tulizopo hizi...

Nakuhakikishia jambo moja kuwa, kesi hakutakuwa na mashinikizo ya kuamua kunyume cha mwenye haki dhidi ya asiyekuwa na haki hata kama Jaji ni CCM kijani kupita majani yenyewe halisi...

Mazingira yatamlazimisha kusimama upande wa haki. Kama huamini, subiri utashuhudia kwa masikio na macho yako...

HAKUNA KESI HAPA hata mtoto mdogo anajua hili...!!
denoo J dudus
Kimsingi, ukamatwaji wa watuhumiwa toka mwanzo ulilenga kuwakomoa kwa nini wameajiriwa na Mbowe (kiongozi wa upinzani), ndio wakawapachika kesi ya ugaidi ili wajihalalishie kuwaweka ndani muda mrefu (kuwabambika kesi kama kawaida yao).

Mbowe aliposema anaenda Mwanza kwa ajili ya lile kongamano la Katiba Mpya wakaona nae wamkamate ili asitimize lengo lake la kudai Katiba Mpya.

Baada ya hapo, ndio wakamchukua Mbowe wakamuunganisha na wale walinzi wake waliokamatwa na kwa pamoja wakapachikwa kosa la ugaidi, leo hii ndio tunaona hizi sarakasi mahakamani, ni kesi ya kutengeneza hii.
 
Nitashangaa sana mahakama ikijivua nguo mbele ya umma wa watanzania na serikali ikijivua nguo mbele ya uso wa dunia (mabalozi wa nje wanaohudhuria kesi).

Hii dunia ya leo sio ile ya 1980's.

Ukiangalia mlolongo wa matukio kwenye hii kesi uliotolewa na watuhumiwa pamoja na mke wa mtuhumiwa Lin'gwenya leo, utaona wazi kuna unyama mwingi zaidi waliotendewa watuhumiwa zaidi hata ya kile kilichofikiriwa mwanzo.

Haki za washtakiwa, na haki za binadamu kwa ujumla wake vyote vilikiukwa wakati wa kuwakamata mpaka baada ya kuwakamata, polisi kukiepuka hiki kikombe hata kwa katiba hii tuliyonayo litakuwa ni ajabu la dunia.

Leo kweli ni 2021 lakini tokea 2015 mahakama zetu zimepoteza kujisimamia kwake labda kuliko hata 1980s. Credit nyingi kwake mwendazake 😂😂😂!

Yuko wapi Lijenje. Wako wapi Ben na kina Azory? Haya hayakutokea enzi za 1980s.

Nani alitaka kumshambulia Lissu? Nini kimefanyika kuhusiana na jaribio kwenye maisha ya Lissu?

Mikutano ya kisiasa imepigwa marufuku kinyume cha katiba. Tunaweza kukimbilia mahakamani kupata haki zetu?

Vipi rafu za kwenye uchaguzi wa 2019/20 kulikuwa na possibility ya kupata haki kwa kukimbilia mahakamani?

Bila katiba mpya yenye kuweka mahakikisho thabiti "there can't be joy yet."

Kwa hali ilivyo kufurahia kwa lolote au kuweka matumaini kwenye lolote ni wishful thinking au kama kujilisha upepo tu.
 
Kama maamuzi yata andikiwa Ikulu/ Lumumba basi ushahidi wa kubumba wa polisi uta pokelewa. Lakini kama Jaji ana maamuzi yake binafsi, basi hakuna ushahidi utapokelewa.. Na hakuna kesi...

Nini kinamfunga jaji kuwa na maamuzi yake binafsi? Dhamira yake tu?

Kumbuka tulisikia yule mwingine aliyekataliwa akisemekana kuwa alikuwa pale kwa malengo maalumu.
 
Mazungumzo yapo, ila kuna pande moja kichwa ngumu, wanataka kulazimisha kuishi kama walivyoishi awamu ya 4 bila kutambua kuwa kila awamu ina mtazamo tofauti na awamu nyingine!! Siku wakikubali kuevolve kutokana na vipindi tofauti tofauti basi hii mikwaruzano yote itaisha!! Wewe hapo kazini kwako umesoma miongozo yote, kila nukta yahusuyo kazi yako?
Wewe so hauhitaji hata kuusoma kwa kuwa hautendi kwa kufuatamiongozo, hiyo hivyo hunahaja nao. 😆
 
alieanza kuharibu hii movie ni kingai ... amekamata madawa ya kulevya... haonyeshi ameyathibitisha kwa mkenya mkuu ... kituko zaidi ni watuhumiwa hawajafunguliwa charge ya madawa ... haya madawa ya kulevya kingai aeleze ameyatoa wapi
 
Pale mwishoni siku Mahita alipofanyiwa cross examination na Kibatala.
Mimi ni mbumbu wa sheria hivyo naomba nieleweshwe hili kama kuna mtu anajua sheria. Mshtakiwa anapopelekwa mahakamani na kukataa kuwa maelezo aliyotoa hakutoa kwa hiari bali aliteswa, kwa nini mahakama isikubali moja kwa moja? I mean kama mwenye maelezo anayakana mwenyewe kwa nini anatiliwa shaka? Kwa nini zisitumike njia nyingine tu za kumtia hatiani? Najua ndivyo sheria ilivyo lakini kwangu mimi naona kuna ukakasi na kunatoa loophole kwa polisi kutumia njia ya mateso ili kupata maelezo kutoka kwa mshtakiwa. All in all, watuhumiwa wa kesi kama hii naweza kusema kwa uhakika kabisa ni IMPOSSIBLE kwa polisi wa Tanzania kuwakamata na kuwafikisha mahakamani bila kuwatesa.
 
Wewe so hauhitaji hata kuusoma kwa kuwa hautendi kwa kufuatamiongozo, hiyo hivyo hunahaja nao. 😆
Kwa kutumia uzoefu wa mtaani ni wazi kabisa hii kesi ni ya kutunga. Nilipomsikia rais Samia anasema wana ushahidi nilidhani kuwa wana jambo la maana kumbe siyo. Na laiti polisi wangekuwa na hata ka-ushahidi kidogo kabisa kabisa, hii kesi ingeonyeshwa kwenye TV moja kwa moja.
 
Una utaalamu wowote wa Sheria? Kama huna basi kuwa na subira, muda ndiyo utatoa majibu, sidhani kama hapa JF utapata jibu sahihi zaidi ya mihemko ya ki CCM na CDM.
Wewe unadhan hapa JF wote ni vilaza hakuwa wanasheria, majaj na mahakim na ata wa ufaham wa sheria ambao kwa mujibu wa mtoa mada hawawez kuchangia chochote mpaka mahakam? Au wee ni Mahita nn? Au kingai?
 
Weee mbona ume elezea mikanganyo ya upande wa ushahidi wa washtakiwa, bila kueleza mapungufu ya PGO. Mahita alisemalisema hajui alipoulizwa PGO

Mpaka akasema muheshimiwa Hakim huyu ananionyesha kitu kingine. Hakim akamjibu... Unafikiri mm siijui PGO? Hukuona hayo mapungufu? Kote Kuna shida Ila Mungu atasimama tu
Ushahidi una mikanganyiko
1. Ushahidi unaonesha waliteswa.
Japo shahidi ameonesha makovu ila ajabu amesema yapo mapya na ya zamani mahakama itachagua.

2. Shahidi ameonesha tena kwa kuhojiwa na wakili wa serkali kuwa alisaini pasipo mateso yapo baadae alisema kwenye Re examination kuwa alitishwa na Kingai, na kitendo cha kuwa na pingu ni mateso.

3. Hatari zaidi ni pale shahidi amedai akili yake haiko sawa kwa ajili ya Battle confusion, na wakili wa serkali kuiita kama mental disoder,iliyosabibishwa na utumiaji wa madawa ya kulevya kupita kiasi. Hivyo kuwa wakati akili yake haikumbuki mambo kisawasawa.
Yote kwa Yote HAKI ITENDEKE
 
Nitashangaa sana mahakama ikijivua nguo mbele ya umma wa watanzania na serikali ikijivua nguo mbele ya uso wa dunia (mabalozi wa nje wanaohudhuria kesi).

Hii dunia ya leo sio ile ya 1980's.

Ukiangalia mlolongo wa matukio kwenye hii kesi uliotolewa na watuhumiwa pamoja na mke wa mtuhumiwa Lin'gwenya leo, utaona wazi kuna unyama mwingi zaidi waliotendewa watuhumiwa zaidi hata ya kile kilichofikiriwa mwanzo.

Haki za washtakiwa, na haki za binadamu kwa ujumla wake vyote vilikiukwa wakati wa kuwakamata mpaka baada ya kuwakamata, polisi kukiepuka hiki kikombe hata kwa katiba hii tuliyonayo litakuwa ni ajabu la dunia.

Tuendelee kuweka rekodi sahihi pia - mdada wa leo ni mke wa Adamoo.
 
Leo kweli ni 2021 lakini tokea 2015 mahakama zetu zimepoteza kujisimamia kwake labda kuliko hata 1980s. Credit nyingi kwake mwendazake [emoji23][emoji23][emoji23]!

Yuko wapi Lijenje. Wako wapi Ben na kina Azory? Haya hayakutokea enzi za 1980s.

Nani alitaka kumshambulia Lissu? Nini kimefanyika kuhusiana na jaribio kwenye maisha ya Lissu?

Mikutano ya kisiasa imepigwa marufuku kinyume cha katiba. Tunaweza kukimbilia mahakamani kupata haki zetu?

Vipi rafu za kwenye uchaguzi wa 2019/20 kulikuwa na possibility ya kupata haki kwa kukimbilia mahakamani?

Bila katiba mpya yenye kuweka mahakikisho thabiti "there can't be joy yet."

Kwa hali ilivyo kufurahia kwa lolote au kuweka matumaini kwenye lolote ni wishful thinking au kama kujilisha upepo tu.
Kila jambo hatua.
 
Back
Top Bottom