Kulipia huduma ya choo stend wakati umelipa getini ni jambo la ovyo

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Chukulia mfano wa bar, guest and chakula. Ukiingia sehemu hizo ukalipia huduma ya msingi basi huduma ya choo unaipata bure. Maana yake huwezi kulipia chumba gest halafu ukitaka kunya unalipia tena choo.

Hali ni tofauti katika stendi za Magufuli, Nanenane na Msamvu. Bila shaka ile 200 nayolipa getini sio kwamba stend inajiendesha kibiashara, lah hasha bali ni gharama za uendeshaji mf usafi nk. Sasa ni ujuha kulipa 200 getini hakafu ukienda kunya unalipishwa 300 tena.

Kwa stend ambazo hazitozi getini ni sahihi kwa sababu choo inabidi kijiendeshe. Lakini hawa wa getini ilitakiwa iwe huduma ya bure kwa watumiaji wa huduma za stend.

Ajabu ni kwamba Chama cha Walaji kiko kimya kinashindwa kuona mambo madogo kama hayo.

Ushauri wangu ni kwamba kanuni na miongozo itolewe kuondoa ada hizi mara moja katika bajeti ijayo. Kinyume na hapo basi na wengine turuhusiwe kutoza huduma za choo kwenye guest, bar nk
 
lipa kodi wewe huo ndio ukubwa

Nani akusafishie mikojo na kinyesi chako kwa kutegemea hela za kuunganishwa unganishwa.
 
Tatizo sio kulipa,
Tatizo ni vyoo kuwa vichafu pamoja na gharama zote wanazotozwa wanainchi.
itakua vyoo vya wilaya yako ila sehemu nyingi za mijini wanafanya vyema kwa usafi kwa gharama ambazo ht mtu wa kawaida anaweza kuzimudu.
 
itakua vyoo vya wilaya yako ila sehemu nyingi za mijini wanafanya vyema kwa usafi kwa gharama ambazo ht mtu wa kawaida anaweza kuzimudu.
Nyie ndio kutwa ... anaupiga mwingi hata akiingia kuswali
 
Nyie ndio kutwa ... anaupiga mwingi hata akiingia kuswali
Hiyo ID yenye picha hii inatumika kushabikia hoja flani za mfumo husika uliopo madarakani awamu hii, na wakati huo huo unaiponda kupitia awamu ya 5, tena ziko zaidi ya ID 300 na ushee humu JF.

Mi huwa nazizuum kwa jicho la 3 na kucheka kwa sauti ya Hayati Dr JPM "hiiiii...iiiii" [emoji28] kisha naelewa zinatumika kwa malengo gani hususani mambo ya kisiasa [emoji6]
 
Mwendazake alijibu hili "Kama hutaki baki na mavi yako nyumbani "

Ha ha ha ila mwendazake alikuwa ana kauli za kukera sana

Ingawa mkuu hoja yako ni ya msingi sana hela ya getini ndiyo ilipaswa kucover mahitaji yote ya stand na siyo kutenganisha items Hivyo
 
Tafuta helaaa uache kulalamikia vitu vidogovidogo kama hivi
 
Mambo ya serikali ni magumu sana. Ukiwaukiza watasema hyo 200 ya getini haitoshi kucover hayo mambo ya usafi vyooni. Wakipandisha hadi 500 ili kucover usafi, hapo wananchi tutalalamika kua sio wote tunaenda kunya stendi.
Ustaarabu umetukosa tu ndo shida yetu.
 
Vyoo vya kulipa vya stendi siyo sekta binafsi au vya manispaa pia?
 
itakua vyoo vya wilaya yako ila sehemu nyingi za mijini wanafanya vyema kwa usafi kwa gharama ambazo ht mtu wa kawaida anaweza kuzimudu.
Mkuu hivi ushawahi tembelea wapi na wapi?
Ukaona jinsi vyoo vilivyo visafi?

Isije ikawa kwako harufu ya kinyesi na mkojo sio uchafu hadi ulione Gogo linaelea kwenye sink.

Maana usafi wa mtu na uchafu wa mtu tunatofautiana viwango.

Hakuna sehem penye public toilets ni kusafi [emoji817] hapa tanzania.
nambie ni wapi?
Tuanze na mbezi daladala stands..
Nk.
 
umenena vema na sasa ili kukwepa lawama serikali imewapa watu binafsi waendeshe vyoo hivyo tena nadhani serikali inachukuwa mapato fulani kwa hao.
 
Inawezekana, anayesimamia choo, na anayesimamia stendi ni idara mbili tofauti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…