Kulivyo Geita tofauti na mabilioni ya dhahabu yaliyopo

Bora utawala wa kimajimbo. Kila Jimbo liwe linaioatia Serikali kuu asilimia fulani, inayobaki itumike kwa maendeleo ya eneo husika.
 
Umechelewa sana,Size ya Mwanza Kwa Sasa ni Mbeya manaa hata Kwa Dom haifikii.

Karibu Jukwaani Battle: Mwanza (The Rock City) Vs Arusha ("A" Town u Chuga)

Nimeenda arusha mara kadhaa, mwaka jana nilikua kule, kamji kamebanana, kadogo sema tu kamechangamka katikati ya mji.

Mwanza jiji almost lote limechangamka kwanzia buhongwa mpaka nyakato na kuendelea mbele, ukija kwenye majengo ndio usiseme.

Arusha mshindani wake labda Mbeya

Dar
Mwanza
Dom
 
Mji ni pesa,kuchangamka na magorofa.

Nje ya Dar kuna Mji gani una skyline kama hii ya Arusha? 👇👇

View: https://youtu.be/KuP5gNj8mmA?si=J1Ua-5U_f0h9cpLZ
 
Bora utawala wa kimajimbo. Kila Jimbo liwe linaioatia Serikali kuu asilimia fulani, inayobaki itumike kwa maendeleo ya eneo husika.
Sio lazima Majimbo ,hivi hivi Mikoa inawekwa tuu kanuni ya mgawanyo wa Rasilimali Mali.

Kenya Kuna Majimbo?
 
County kwa Kiswahili ni nini?
 
Kwenye hizo serikali za majimbo si ndo wananchi wataumia zaidi sasa!? Maana michango,kodi na vitu vingine vingi, lazima vitoke kwa raia kama chanzo cha mapato
 
County kwa Kiswahili ni nini?
Kaunti au wewe umewahi sikia wanaita Province au jina tofauti na Kaunti?

Majimbo yanakuwa na Utawala wa ndani wa kiserikali kabisa na hivyo kuinda federal goveykama Nigeria,Ethiopia nk

Sasa Kenya ni federal Government Ile? Acha kukariri vitu.
 
Kaunti au wewe umewahi sikia wanaita Province au jina tofauti na Kaunti?

Majimbo yanakuwa na Utawala wa ndani wa kiserikali kabisa na hivyo kuinda federal goveykama Nigeria,Ethiopia nk

Sasa Kenya ni federal Government Ile? Acha kukariri vitu.
Hapo umenielimisha au umenikejeli? Unajua nilicholenga kukuuliza hivyo?
 
Kwenye hizo serikali za majimbo si ndo wananchi wataumia zaidi sasa!? Maana michango,kodi na vitu vingine vingi, lazima vitoke kwa raia kama chanzo cha mapato
Siwezi nikacomment maana sijajua serikali za kijimbo zinavyojiendesha practically na position ya serikali kuu ipoje, labda nitafiti kidogo
 
Hapo umenielimisha au umenikejeli? Unajua nilicholenga kukuuliza hivyo?
Kuweka kanuni za mgawanyo wa Rasilimali haihitaji ku kopi na ku paste Bali mnaweza weka Kwa kuangalia muundo wenu.Ndio maana nawasifu Kenya.

Hata sisi hatuhitaji kuiga ila tunaweza angalia Ufanisi na wekness ya mifumo mingine na kuja na WA kwetu tukawa mfano pia.

Ilivyo Sasa mgawanyo unategemea central government planning ya Toka enzi za chama kushika hatamu.

Tulianza kwa.kufanya ugatuzi au Kupeleka madaraka Wilayani via Serikali za mitaa lakini hatujafanya inavyostahili maana Serikali za mitaa zimeishia kuwa Wakala wa Serikali kuu ila hazina mamlaka ya kupanga mambo Yao,ni bortion tuu.
 
Siwezi nikacomment maana sijajua serikali za kijimbo zinavyojiendesha practically na position ya serikali kuu ipoje, labda nitafiti kidogo
Si mfumo kama wa USA labda!?
 
Kiukweli nitamsema Magu kwa mengi lakini at least yeye ndo alijitahidi kufanya distribution nzuri hadi mikoani, na movement ya kuifanya dodoma makao makuu, japo ilianza seriously kwa kikwete ila yeye aliingia 100% full..

Nadhani ni njia nzuri pia, hatuwezi kuufanya kila mkoa kuwa jiji lakini kuwa na jiji kubwa linalojitosheleza kwa kila kanda itawapunguzia adha ya wananchi kwenda umbali mrefu ili kupata huduma

Natamani next point iwe Mwanza na Mbeya maana hayo majiji yana potential kubwa tu kiuchumi japo mwanza, airport tu kukamilisha inachukua decades ila serious investment ikiwekwa na Vile mkoa upo diverse kiasi kiuchumi, mambo yatapendeza
 
Nadhani Kanda ya ziwa wangedai uhuru wao ile Kanda inazalisha Dhahabu kuanzia Geita, Mwanza, Simiyu,Shinyanga hadi Mara .

Shinyanga ilikuwa na bado inazalisha Madini ya Almasi lakini Mkoa ni wa kipuuzi sana.

Bado Kanda ya ziwa wanaziwa Victoria inamaana kazi za uvuvi zinafanyika kwa wingi.

Bado Mkoa wa mara inambuga ya Serengeti.

NB: Mikoa ya Mwanza, Geita, Mara, Shinyanga, Mbeya, Lindi, Arusha, Moshi,, Tanga haikupswa kuwa ilivyo Leo ni ujinga tu wa maccm.
 
Magu alifanya vyema kuikuza Dom.

Ilitakiwa the same Nguvu ielekezwe Mtwara, Mbeya na Kigoma ambako ni Makao Makuu ya Kanda za Kusini, Magharibi na Kanda ya Ziwa.

Tukiwa na Miji mikubwa maeneo hayo walau tunapata soko na pia inalwta Hali ya balance kimaendeleo.
 
Nimekusoma sana mkuu,

Mambo mengi nchini hususani kwenye miundombinu huwa yanafanywa kwa copy and pasting, ukiangalia hata hivi vivuko au madaraja marefu yanayojengwa Dar ilhali watu wanaona bora wapite chini kuliko kuzunguka sana. Utaona wakandarasi hawakufikira tabia na asili ya watanzania

Hiyo machinga complex tu ni huzuni, kiukweli kabsaa, wataalamu wetu wazingatie mahitaji yetu na watengeneze vitu vitakavyoendana nasi, including mfumo wa utawala maana tulionao kwa sasa ni wazi umefeli hivyo decentralization itakayoendana nasi ni muarobaini sahihi

Japo kama nilivyosema tukisema tuondoe utagemezi kwa serikali kuu, utaondoa ile power waliyonayo kisiasa kama "main controller and providers" Kwenye uchumi wetu na haswa katika macho ya wananchi ambao huichukulia serikali kuu kama last resort au hero wa matatizo yao. Kuiondoa hii ni kuondoa political influence ya mfumo uliopo, kitu ambacho sidhani kama kitatokea mkuu
 
Kila Kanda Nchi hii Ina Mali yake ashibu ya kuingiza pesa,ni mipango mibovu tuu ya serikali.

Kanda ya Kati ambayo unaonekana ni maskini ila Inaongoza Kwa Madini mengi sana ya Uranium na pia ndio Makao Makuu ya Nchi hivyo maendeleo ni hayawezi epukika.
 
Ni uwezo duni wa Wataalamu Wetu wa taasisi ambao huwapa maelekezo wajenzi.

Tupunguze udhibiti wa Serikali kuu kwenye Baadhi ya mambo madogo madogo.

Serikali kuu kupanga mambo ya madarasa ,sijui Barabara za mitaani nk ni ujinga.Hayo mambo yafanywe huku huku chini.

Kazi ya serikali kuu ni kutunga sheria mama ,sera na Kusimamia sera ila sio Kila kitu kama ilivyo Sasa.Unamuuliza Waziri wa Elimu mambo ya vyoo vya Liwale huko atajua saa ngapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…