Uchaguzi 2020 Kulwa Mang'ana asitisha kutia nia ya ubunge Siha baada ya kupata ajali akienda kuchukua fomu

Uchaguzi 2020 Kulwa Mang'ana asitisha kutia nia ya ubunge Siha baada ya kupata ajali akienda kuchukua fomu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria Tanzania, Kulwa Mang'ana, amepata ajali katika eneo la Boman'gombe wilayani Hai wakati akiwa njiani kuelekea wilayani Siha kwa lengo la kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi.

Siha.jpg

Nyie mnadhani Kukaa mule Bungeni kunatosha tu kuwa na 'Upako' pekee wa akina Mwamposa na Gwajima? Ndumba nazo ni lazima sana tu!

=======

Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria Tanzania, Kulwa Mang’ana amepata ajali katika eneo la Boman’gombe wilayani Hai wakati akiwa njiani kuelekea Wilaya ya Siha kwa lengo la kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi.

Kwa mujibu wa mashuhuda, ajali hiyo ilitokea majira ya saa 10:00 jioni njia panda ya kuelekea Siha ambapo dereva wa pikipiki aliigonga gari yake kwenye eneo la mlango wa dereva na kusababisha kuvunjika kwa kioo ambacho vipande vyake vilimuingia sehemu za mwili ikiwemo kichwani.

Baada ya taratibu za kisheria kukamilika katika Kituo Cha Polisi Cha Boma Ng’ombe, Kulwa alieleza kusitisha zoezi la kwenda kuchukua fomu huku akiwatakia kila la kheri wote waliojitokeza kuchukua fomu katika jimbo hilo.

Amesema atasubiri mpaka mwaka 2025, kwa sasa ataendelea kuwa mwanachama mtii, muaminifu na mzalendo kwa nchi yake.
 
Nyie mnadhani Kukaa mule Bungeni kunatosha tu kuwa na 'Upako' pekee wa akina Mwamposa na Gwajima? Ndumba nazo ni lazima sana tu!
Hichi tu kipengele kimetosha kabisa kumfahamu mleta mada kuwa hajawahi kufahamu ni Kwa nini kila mtu ni lazima atakufa!!!

Anataka kutuaminisha kwamba wote wanapataga ajali huwa wanalogwa kitu ambacho si kweli,

Amepata ajali kama ambavyo mwingine yeyote anaweza kupata ajali

Pole Sana mtia Nia, Mungu akujalie upone haraka majeraha yote
 
Hapo Mtu ' kakoswakoswa ' Mkuu na Mimi ningekuwa ndiyo Yeye baada ya hilo ' Tukio ' ningeishia hapo hapo na Kurejea Kuwakufunzi Wanachuo.
Ninayoyaona huku niliko ni shida tupu. Kama kuna kipindi uganga unalipa ni hiki.
Hivi rafiki yangu Genta huna ujuzi wowote kuhusu hii kitu teyengeneze fedha?!?
 
Hivi fikra kwamba unaweza kumchanganya Mungu na ndumba watu wameipata wapi, ndo maana waganga wa kienyeji na wajanja wajanja wa imani feki za kidini wamezidi kupata nguvu kipindi hiki, bila kuwasahau wafanya matambiko, mara utasikia mmeenda kuchinja mbuzi...hapa ndo unaelewa kwamba dini haijafanya kazi ya kuelezea ukuu wa Mungu barabara...
 
Back
Top Bottom