Uchaguzi 2020 Kulwa Mang'ana asitisha kutia nia ya ubunge Siha baada ya kupata ajali akienda kuchukua fomu

Uchaguzi 2020 Kulwa Mang'ana asitisha kutia nia ya ubunge Siha baada ya kupata ajali akienda kuchukua fomu

Kwahiyo alikuwa amesafiri akiwa amevaa hilo shati?

Kalivaa baada ya ' Kukoswakoswa ' Kunyakuliwa na Israeli Mtoa Roho Mkuu. Kuna Watu wanadhani Siasa za Tanzania ni za ' Kuzivamia ' tu hivi.
 
Hahah we jamaa we we ni mmoja wa watu wanaochangamsha sana jukwaa kwa namna unavo andika

Akhsante Mkuu na Pongezi ( Kongole ) zako hizi nimezipokea kwa Mikono Miwili na zimezidi Kunipa Nguvu na Moyo wa Kuwachangamsheni hapa.
 
Inaweza kuwa ajali ya kawaida kabisa, ila sbb imetokea wakati anaenda kuchukua fomu ya ubunge basi ajali hiyo itadhaniwa imesababishwa na uchawi. Ni hisia tu.

Na labda kwa Kukusaidia tu hilo Jimbo ambalo amekuwa na ' Kiherehere ' nalo kwenda Kuligombea ' Waliomtangulia ' Kuchukua Fomu ni HATARI.
 
Mang'ana si jina la kikurya hilo uchagani anafuata nini sasa

Sasa Mara hadi kwenda Kilimanjaro wapi na wapi Mkuu? Kwanini wenye ' Kilimanjaro ' yao wasiamue tu Kumalizana na ' Kirusi ' hicho mapema tu?
 
Aache Ubwege siku nyingine asikate tamaa mapema kirahisirahisi namna hiyo yaani mlango tu kuchubuka ndio ameogopa?

Mlango Kuchubuka hivyo ni dalili tosha kabisa kuwa huko ambako alikuwa na ' Kiherehere ' nako ' Kungemchubua ' zaidi hadi huko Kaburini Mkuu.
 
Mkuu GENTAMYCINE umesema yote kabisa. Yaani mtu una drive kwa speed kuwahi fomu Jimbo ambalo hata hajawahi kuchangia Mia.

Kuna Watu wengine Vifo huwa wanavitafuta Wenyewe Mkuu. Wewe Mtu ni Mkurya huko kwa Wachagaa ( Shemeji ) zangu alifuata nini huyu Mtu?
 
Kwani ukiwa mbunge unaacha kufundisha chuo?

Kuna uliyewahi kumuona akitoka Kufundisha Chuo Kikuu kisha akawa Mbunge halafu akawa anaendelea tena na Kukufunzi Chuo? Tutolee Ujuha.
 
Back
Top Bottom