Kumalizika kwa tembo wetu ni vita kamili kati ya askari wa wanyamapori na majangili, nguvu ya ushirikina

Kumalizika kwa tembo wetu ni vita kamili kati ya askari wa wanyamapori na majangili, nguvu ya ushirikina

Wanyama wataisha huko parini na misitu ya asili itaisha.
Cha msingi ni hizo rasilimali kwa sasa zitumike kuwatajirisha watu kwa kiwango cha juu sana.

Wanyama wote watakua wanafugwa kama Ng'ombe. Kwa hiyo itakua rahisi kuendeleza kizazi cha tembo kwa kuwafuga kwenye zoo.

Ndio maana serikali inashauriwa ishirikiane na wawekezaji ili tuanze sasa kwa kufuga wanyama kabla hawajaisha huko porini.

Hii mambo ya kuzuia baadhi ya wanyama wasifugwe na watu binafsi ndio itasababisha wanyama hao kutoweka.

Hata Faru ingekua ni vyema wakifugwa ili waongezeke kwa wingi badala ya kuwaacha porini pasipo na ulinzi wa kutosha.

Hata misitu ya asili itaisha kwa kadri binadamu wanavyoongezeka. Cha msingi ni watu kupanda misitu yao ya wenyewe mbali na hizo za asili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Niliwahi msikia Mwalimu Nyerere akisema miaka mingi sana iliyopita wazungu walikua na natural resources kama vile mapori na mbuga kama hizi zetu lakini wakaiharibu jinsi sisi tunavyoharibu vya kwetu sasa hivi

Matokeo yake hali ile ikishapotea haiwezekani tena kuirudisha. Akasema wazungu hawajui wafanye nini waeze kuirudisha waliyoiharibu mababu zao, na kwamba wamebakia kutuasa na kutushauri tulinde maliasili zetu ikiwemo misitu na wanyama tusije kua kama wao

Watalii wanakuja kwetu na kutupatia pato la kutosha kama taifa kwa kuona wanyama katika maeneo yao ya asili na hawafuati zoo au mabustani ya kuwafugia wanyama pori. maana nadhani wanyama pori wanaofugwa wapo sehemu kadhaa duniani lakini hawavutii kama waliopo katika mazingira yao ya asili na pia ni gharama kubwa sana kuwatunza kwa kuwafuga
Kwahiyo mkuu tukishamaliza hizo rasilimali kwa uchoyo na ujinga wetu ndio hatuwzi tena kuirudisha hali ya awali
 
hizo ni hekaya tu, ukienda kwa wavuvi utakutana na hekaya kama hizohizo. na sababu kuu ya kuwepo imani za kishirikina ni ukosefu wa elimu, siwatukani lakini ndio ukweli kuwa wawindaji haramu ni watu wenye upeo mdogo na akili finyu, waliokwenda shule kidogo ni ma boss wao ambao hata porini hawaendi.
Jumla ya maeneo ya nchi kavu ambayo yanalindwa (protected areas) tanzania ni kilomita za mraba 113,838 wakati eneo lote la nchi ambalo ni nchi kavu ni kilomita za mraba 886,676, hivyo utaona maeneo yanayolindwa ni 12.8% ya eneo lote la nchi kavu la nchi, hilo ni eneo kubwa sana kulilinda kwa idadi ya askari wa wanyama pori tuluonao na vifaa tulivyo navyo. ndio maana nchi zilizo endelea zinajitahidi kuunga mkono serikali katika kuyalinda hayo maeneo lakini bado kazi ni ngumu, hivyo majangiri bado wanafanikiwa kuua wanyama sio kwasababu "wana fundi" huo ni upuuzi wanaodanganyana wenyewe kwa wenyewe kutokana na akili zao finyu ila ukweli ni kwamba hatuna rasilimali za kutosha kuyalinda hayo maeneo kwa ufanisi.
Kama hujui kitu kaka kukaa kimya ni busara. Uwindaji ni elimu hakuna hata Tembo mmoja angeuawa maana askari wana elimu na vifaa vya kwa kisasa kuliko wawindaji haramu wenye silaha duni (Rifle/Gobore Mara chache SMG). Lakini kama alivyosema mleta mada Mara nyingi askari huambulia mizoga ya Tembo siku tatu au zaidi baada ya kuuawa. Mwindaji anajiandaa zaidi ya miezi 2 kwenda kuua Tembo mmoja, kabla ya hapo anakuwa amefuata au kuharibu masharti ya uwindaji Mara nyingi tu. Pori halina mwenyeji, kupotea ukikiuka masharti ni jambo la kawaida. Wawindaji HARAMU ni HARAMU hasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jangili anapoingia porini tayari ile ni vita ambayo haijatangazwa na ndiyo maana anaingia na silaha za kila aina
 
Niliwahi msikia Mwalimu Nyerere akisema miaka mingi sana iliyopita wazungu walikua na natural resources kama vile mapori na mbuga kama hizi zetu lakini wakaiharibu jinsi sisi tunavyoharibu vya kwetu sasa hivi

Matokeo yake hali ile ikishapotea haiwezekani tena kuirudisha. Akasema wazungu hawajui wafanye nini waeze kuirudisha waliyoiharibu mababu zao, na kwamba wamebakia kutuasa na kutushauri tulinde maliasili zetu ikiwemo misitu na wanyama tusije kua kama wao

Watalii wanakuja kwetu na kutupatia pato la kutosha kama taifa kwa kuona wanyama katika maeneo yao ya asili na hawafuati zoo au mabustani ya kuwafugia wanyama pori. maana nadhani wanyama pori wanaofugwa wapo sehemu kadhaa duniani lakini hawavutii kama waliopo katika mazingira yao ya asili na pia ni gharama kubwa sana kuwatunza kwa kuwafuga
Kwahiyo mkuu tukishamaliza hizo rasilimali kwa uchoyo na ujinga wetu ndio hatuwzi tena kuirudisha hali ya awali
Ni kweli wazungu nao walikua na rasilomali zao za asili lakini ziliisha.
Ziliisha kwa sababu ya kutafuta maendeleo.
Aendeleo makubwa ya kiteknolojia yanasababisha hali ya hewa inabadilika lakini pia binadamu anapotafuta mahitaji yake Mara nyingi anaathiri uoto wa asili.

Mfano hata wingi wa watalii kwenye mbuga za wanyama muda wote kunawadistabu wanyama lakini ndio maendeleo.
Tulipaswa tuwaache wanayama wawe na maisha yao ya asili kama walivyokua wanaishi na babu zetu.
Leo hii kuna magari yanatoa moshi mwingi huko kwenye maeneo yao ya hifadhi. Hii inawaathiri wanyama kibiolojia. Haikwepeki maana ndio maendeleo yenyewe.

Kuwafuga kwenye zoo ni muhimu ili kuendeleza kizazi cha wanyama bila kujali kuwa wanakuja watalii au laa.

Waafrika tumekua na hulka ya tofauti kidogo kila kitu tunakifanya ili kuwavutia wazungu waje kutalii. Maendeleo yakiwepo na kuwapa watu wetu fursa ya kutajirika na kuweka akiba tunaweza kuwa na kutalii wa ndani Au wa Afrika wenyewe kwa wenyewe. Tunawekeana vikwazo vingi wakati watu wetu hawana fedha za kutosha hata kula mila miwili.

Turuhusu sehemu kama Zanzibar wanyama wa aina zote wafugwe na wawekezaji wa ndani. Twiga ,Tembo, Faru wapatikane Zanzibar kwa lengo la kulinda kizazi cha wanyama hao.
Mtu akimfuga Faru ni lazima kuna siku Faru huyo atazeeka na kufa basi atauza pembe yake.

Angalia mfano kwenye hifadhi ya taifa kuna pembe na meno ya tembo kwa matani lakini wanashinikizwa wachomwe moto wakati kuna soko.
Kwa nini wasiuzwe wakati kuna tembe wengine wengi tu wamekufa kwa umri mkubwa au ugonjwa?

Tusipoanza kuwafuga wanyama sasa basi miaka 100 ijayo baadhi ya wanyama hatutakua nao iwe wameuawa au laa .Hali ya hewa haitaruhusu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
uruhusu sehemu kama Zanzibar wanyama wa aina zote wafugwe na wawekezaji wa ndani. Twiga ,Tembo, Faru wapatikane Zanzibar kwa lengo la kulinda kizazi cha wanyama hao.
Mtu akimfuga Faru ni lazima kuna siku Faru huyo atazeeka na kufa basi atauza pembe yake.
Niliwahi kuwasikia wawekezaji wa Dar es laam Zoo wakisema wao peke yao wasingeweza ku i maintain ile zoo bila msaada wa wahisani toka nje maana gharama za kuwahudumia wale wanyama wanaowafuga pale ni kubwa sana na viingilio wanavyokusanya kutoka kwa watu wanaokwenda kuwaona hao wanyama havikidhi hata budget ya siku tano ya kuwalisha wamyama

Ni tamaa yangu hili la kuwaruhusu watu wafuge hao wanyama liwe na tija ya kweli lakini kwa uwelewa wangu mdogo kuhusu masuala haya naamini tafiti za jambo hilo zilishafanyw na wasomi wetu na mamlaka husika, na pengine ikaonekana ni jambo ambalo linachangamoto nyingi, sina hakika na hilo mkuu
 
Tatizo kuna wanyama ambao ni vigumu kwa mtu binafsi kuwafuga na nadhani pia utaratibu na sheria ya kuwafuga ni ngumu sana ;sio tu kuwafuga bali hata kuwa na ngozi yake ndani ni ishu.

Hata hivyo ni vyema tukaanza sasa kuwatafuta wawekezaji wenye mitaji mikubwa hata kwa kuwapa maeneo makubwa kwa masharti ya kuwazalisha wanyama na kutunza vizazi vyao.

Hii ya kutegemea serikali tu kuwalinda ni ngumu mana wakati mwingine kuna mambo kama hayo ya ushirikina nani atawajibika kuloga ili alinde Mali za umma. Matokeo yake kila siku wanyama wanauawa bila majangili kuonekana.
Wanachofanya Majangili ni kuwashirikisha wenyeji wa maeneo ya wanayama mana wanajua dawa za kuwapumbaza wanyama.

Kuna jamaa aliniambiwa kuna kabila Fulani nchi moja wanaishi porini na wanyama. Ukipita huwezi kuwaona kama hawataki uwaone. Utawaona kwa mbali ukifika karibu wanapotea .Ukipita unawaona kwa nyuma.Sasa dawa zao ndizo wanazotumia majangili kuwinda hata kama kuna askari.

Zoo nyingi zina baadhi ya wanyama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hizo ni hekaya tu, ukienda kwa wavuvi utakutana na hekaya kama hizohizo. na sababu kuu ya kuwepo imani za kishirikina ni ukosefu wa elimu, siwatukani lakini ndio ukweli kuwa wawindaji haramu ni watu wenye upeo mdogo na akili finyu, waliokwenda shule kidogo ni ma boss wao ambao hata porini hawaendi.
Jumla ya maeneo ya nchi kavu ambayo yanalindwa (protected areas) tanzania ni kilomita za mraba 113,838 wakati eneo lote la nchi ambalo ni nchi kavu ni kilomita za mraba 886,676, hivyo utaona maeneo yanayolindwa ni 12.8% ya eneo lote la nchi kavu la nchi, hilo ni eneo kubwa sana kulilinda kwa idadi ya askari wa wanyama pori tuluonao na vifaa tulivyo navyo. ndio maana nchi zilizo endelea zinajitahidi kuunga mkono serikali katika kuyalinda hayo maeneo lakini bado kazi ni ngumu, hivyo majangiri bado wanafanikiwa kuua wanyama sio kwasababu "wana fundi" huo ni upuuzi wanaodanganyana wenyewe kwa wenyewe kutokana na akili zao finyu ila ukweli ni kwamba hatuna rasilimali za kutosha kuyalinda hayo maeneo kwa ufanisi.[/QUOTE huna point
 
Jambo usilolijua ni vigumu mno kulikubali. Mbugani, ziwani/baharini, migodini. Ushirikina unaofanyika huko kama hufahamu ukisimuliwa huwezi amini. Wacha niishie hapa kwa sasa.
 
Back
Top Bottom