Kumbe ACT-Wazalendo wamepanga nyumba ya Maalimu Seif

Kumbe ACT-Wazalendo wamepanga nyumba ya Maalimu Seif

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Hii "Self"ni ya Seif Hamad, lilitumika na CUF Maalimu baada ya ugomvi na Lipumba.

Baada ya CUF Maalimu kuhamia ACT makao makuu yamehamia hapa. Tumefanya vikao vingi hapa katika uchaguzi Kinondoni. Sasa lina rangi ya ACT.

Hakuna ugomvi tuna jibu nia OVU tu ya CCM na washirika wake. - Godbless Lema.

NB: Kwanini wanadanganya kuwa imejengwa na chama.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetangaza kwamba mpaka sasa kimejenga ofisi mpya za kisasa zinazofikia idadi ya 457, nchi nzima.

Jambo hili limefichuliwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho, John Mnyika akiwa Mkoani Rukwa kwa ajili ya mpango wa kisasa wa kusajili wanachama unaoitwa Chadema Digital.

Mnyika amedai kwamba Chadema iliona ni vema kupeleka majengo kwenye mzizi wa wanachama nchi nzima badala ya kuweka jengo moja lenye vyumba 450 Makao Makuu, na kwamba mchakato wa Ujenzi wa Makao Makuu utaanza baada ya kusimika ofisi nchi nzima.
 
Hii
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetangaza kwamba mpaka sasa...
Hii Maana yake nini Mnyika kutoa maelezo hayo kipondi hiki cha uzinduzi mjengo wa kifahari wa ACT?

Chadema wameona wamebugi, wanajaribu kuzima kelel za wafuasi wao wanaoulizia mabilioni ya Sabadoo na ruzuku na join the chain yametumikaje.

Mnyika alitakiwa akae kimya kibanda kile cha Ufipa hakifanani na mijengo ya viongozi wa Chadema, wenye akili watajua Chadema ni kikundi cha wapiga dili tu.

Ndio maana wapo viongozi walipokosa ubunge wamekimboa Ulaya wanasubiri uchaguzi waje wagombee tena.
 
Hii

Hii Maana yake nini Mnyika kutoa maelezo hayo kipondi hiki cha uzinduzi mjengo wa kifahari wa ACT?

Chadema wameona wamebugi, wanajaribu kuzima kelel za wafuasi wao wanaoulizia mabilioni ya Sabadoo na ruzuku na join the chain yametumikaje. Mnyika alitakiwa akae kimya kibada kile cha Ufipa hakifanani mijengo ya viongozi wa Chadema, wenye akili watajua Chadema ni kikindi cha wapiga dili tu. Ndio maana wapo viongozi walipokosa ubunge wamekimboa Ulaya wanasubiri uchaguzi waje wagombee tena.
Ni ufafanuzi unaohitajika kwa wakati sahihi kuepesha kupotosha
 
Hakuna upotoshaji hapo mkuu, Chadema kutokua na Ofisi inayolingana hadhi yake ni mfano mbaya kwa Upinzani, chama kinachojiita chama kikuu cha uponzani kilotakiwa kifanye tofauti.
Hivi @AIPOLO hadhi ni sera na maono au ni vitu vya kifahari? Haya mambo ndio yametufikisha hapa kama taifa .. Mtu akishakuwa waziri basi apewe gari la mamilion kuonesha hadhi yake
 
hadhi ni sera na maono au ni vitu vya kifahari?
Suala hapa hizo ruzuku, mamilioni ya Sabadoo na mapesa ya join the chain yamefanya nini, au yamechaapisha vitabu vya sera na kuvigawa kwa wanachama? Msichukulie kila anae hoji hili ni mpinzani wenu tu, wapo wanachama wa chadema wenye akili wanaongalia mambo kwa kutumia akili zao sio utetezi wa kina Mnyika.
 
Hizi sasa ni hoja nyingine nje ya mada husika.. Kama kuna ufisadi umefanyika anayethibitisha ni mkaguzi mkuu wa serikali.. Je CHADEMA wana hati chafu kwenye hili?
 
Hizi sasa ni hoja nyingine nje ya mada husika.. Kama kuna ufisadi umefanyika anayethibitisha ni mkaguzi mkuu wa serikali.. Je CHADEMA wana hati chafu kwenye hili?
No! Hoja ni ileile kwanini chama chenye umri zaidi ya miaka 30, chama amabacho kimesha pata mabilioni ya pesa, chama kinachojiita chama kikuu cha upinzani bado kinaishi kwenye vibanda vichochoroni? Je chama hiki kipo serious kweli, au ni kindi cha wapiga dili tu?
 
Hizi sasa ni hoja nyingine nje ya mada husika.. Kama kuna ufisadi umefanyika anayethibitisha ni mkaguzi mkuu wa serikali.. Je CHADEMA wana hati chafu kwenye hili?

Mshana uko sahihi, je viongozi wa juu wa CDM ndani ya hii miaka 10, majengo yao binafsi wanayomiliki kupitia kufaidika na CDM, bado ni duni kama hiyo ofisi yao ya makao makuu?
 
No! Hoja ni ileile kwanini chama chenye umri zaidi ya miaka 30, chama amabacho kimesha pata mabilioni ya pesa, chama kinachojiita chama kikuu cha upinzani bado kinaishi kwenye vibanda vichochoroni? Je chama hiki kipo serious kweli, au ni kindi cha wapiga dili tu?
Nataka tuzungumzie kwa ithibati za nyaraka kaka haya mengine tutakuwa tunafanya hekaya, vyama vinakaguliwa hesabu zao za matumizi na hii kazi inafanywa na organ ya serikali
 
Mshana uko sahihi, je viongozi wa juu wa CDM ndani ya hii miaka 10, majengo yao binafsi wanayomiliki kupitia kufaidika na CDM, bado ni duni kama hiyo ofisi yao ya makao makuu?
Tindo sijui chochote kuhusu maisha yao binafsi na sidhani kama ni sahihi kufanya hivyo kwakuwa hata sisi sote maisha tuliyokuwa nayo huko nyuma miaka 10 iliyopita ni tofauti kabisa na sasa
 
Ccm wameidumaza nchi kimbilio lao eti Chadema hawana office! Kubalini tume huru muone office inasaidia nini
Chama hakiwezi kuwa na ofisi kichochoroni ya hovyo hovyo kikaaminika. Chama kikubwa kinaendeshwa kihuni.
 
Back
Top Bottom