Kinachobishaniwa ni kutanguliza jengo hilo moja kubwa au majengo ya ofisi ndogo yaliyotapakaa nchi nzima karibu na wanachama na yanayojengwa na hao hao wanachama kwa nguvu zao wenyewe kwenye maeneo yao! Wanaofahamu historia ya nchi hii watakumbuka kwamba kazi za kujitolea ilikuwa sehemu moja ya mikakati ya kujenga nchi na utaifa mara baada ya uhuru. Ari hii ya kujitolea ilififishwa na matukio mengi ya kisiasa ya kipindi hicho. Kwa hakika kitendo tu cha kuwaunganisha wanachama, kuwaelimisha, kuwapanga na kuwashawishi kujenga ofisi kwenye eneo lao ni hatua kubwa sana katika ujenzi wa chama cha siasa. Chama cha siasa pekee kilichowahi kujaribu kufanya kazi kama hii angalau kwa muda mfupi ni TANU (ASP?).
[emoji1545][emoji1752][emoji818][emoji817][emoji817]