Kati ya Diamond na Kiba nani anayeonyesha kupambana na mwenzake.?
Punguza mkari
Diva hamuwezi kushindana na Diamond bila kutumia mbinu mbadala.
Kama alivyosema Wema yeye ni team Kiba lakini anaukubali mziki wa Diamond, na atamshangaa mtu atakaeuponda mziki wa Diamond.
Hivi unafiki Diamond alichukuwa KORA sababu anapendwa sana Tanzania? Hapana ni juhudi zake pamoja na uongozi ulio bora.
Tanzania tunahitaji kuwa washindani wengi hasa kwenye tuzo za kimataifa kitu ambacho team Kiba mmefeli.
Hampo kwa ajili ya kumsaidia Kiba kitaifa na kimataifa, ila kumshusha Diamond awe majalala mpate cha kuongea.
Ningependa Team Kiba mngeanzisha kampeni maalumu ya kumpaisha Kiba kimataifa, kama ilivyo Nigeria kati ya Davido na Wizkid.
Hizi kampeni zenu mnafaidisha zaidi matapeli wa mziki Tanzania kuliko Kiba.
Jana tu pale Mwanza Wakati wasanii wengine walilipwa kwa makadirio Diamond alilipwa kwa kila tiket kitu ambacho team Kiba mmeshindwa.