Kumbe Askofu Gwajima anaweza kuanzisha chama cha siasa na kikawa na nguvu kuliko CHADEMA

Kumbe Askofu Gwajima anaweza kuanzisha chama cha siasa na kikawa na nguvu kuliko CHADEMA

SOPINTO

Senior Member
Joined
Oct 19, 2020
Posts
155
Reaction score
387
Askofu Gwajima siku zinavyozidi kwenda anazidi kuwaaminishia watanzania kuwa yeye si mtu wa kuyumbishwa yumbishwa na wachumia tumbo hata kama yupo chama cha CCM , ana uwezo wa kumpinga Mwenyekiti wake pamoja na viongozi wote wa CCM kama sehemu ya misimamo yake pamoja na imani yake. Nguvu hii anayoipeleka moja kwa moja kwa wafuasi wake waliotapakaa nchini kupitia makanisa yake kuwa tusiyumbishwe na misimamo feki ya Serikali kuhusu chanjo ya Korona.

Tafsiri hii inaniambia kuwa Mchungaji Gwajima kama watu wanavyomwita jina la utani Gwaji Boy kama kiongozi wa wafuasi wake ameonesha kutotetereka na kusimamia misimamo thabiti kulingana na miongozo yake ya imani toka hapo awali , hii inaonesha kuwa Gwajima ni binadamu ambaye ni kiongozi kwa imani mwenye misimamo imara ambayo ipo tofauti sana na hii ya wasaka tonge kama kina Mnyika , Tundu Lissu , Mbatia , Zitto Kabwe na viongozi wengine wa kisiasa.

Gwajima akianzisha chama chake cha kisiasa na akaongeza miundombinu na akaweka sera nzuri ambazo zinatekelezeka zenye mlengo wa kutatua matatizo ya watanzania na kwasababu mpaka sasa tayari anawafuasi karibia mikoa yote nchini basi kwa hali hiyo anaweza kuwa kiongozi wa kisiasa mwenye mapinduzi makubwa nchini.

Sifa kubwa ya ushawishi aliyonayo hii ni moja ya kigezo kikubwa kwake.

Nileteeeni Gwajimaaa
Nileteeni Gwajimaaaa
Nileteeeeni Gwajimaaaaaaaaaaaaa .... maneno ya mwendazake JPM.....
 
Afadhali abaki hivi wanaweza wakamuonea onea huruma,akianzisha chama atakomeshwa kiwazi wazi,gari yake ya kutembelea itakuwa karandinga nyumba ya kulala Central..
 
Mchungaji Gwajina a.k.a Askofu Gwajima siku zinavyozidi kwenda anazidi kuwaaminishia watanzania kuwa yeye si mtu wa kuyumbishwayumbishwa na wachumia tumbo hata kama yupo chama cha CCM , anauwezo wa kumpinga mwenyekiti wake pamoja na viongozi wote wa CCM kama sehemu ya misimamo yake pamoja na imani yake .
Hayo makeke yake yote anayafanya sababu yupo ccm, lingine ccm ya sasa inamakundi hata kama hayaonekani so inawezekana yeye ni speaker tu walioshika mic (vigogo wa chama) wapo nyuma. Siro kamjibu waziri wa Afya kama vile anamjibu Mnyika, ndio ufahamun kuwa hata Siro anakundi lake linalomtumia.
 
Anaweza kuwa mwanasiasa mwenye ushawishi wakimtimua CCM wakimkimbiza kwenye uaskofu akaanzishe chama
 
... kwa kuutumia vizuri mtaji alioachiwa na Jiwe kwakweli namshauri Gwajiboy ye 'ata aanzishe tu chama maana kanda ya ziwa yote keshaiteka!
😅
1629266772585.png
 
Askofu Rashid siku zote ana mwanzo tu,kila jambo analolianzisha halina mwisho wa kueleweka.

Train ya umeme

Wapiga kura Kawe kupelekwa USA

Boat za uvuvi Kawe

Ujenzi wa Ghorofa refu kuliko yote Tanzania

Hataki Ubunge yeye ni mkubwa kuliko Rais na Wabunge....

Kumfufua Amina Chifupa.
 
Acha kuamisha magoli, usiingize CHADEMA kwenye suala hili ili mpate pa kutokea. Watu wasio na misimamo ni CCM kuanzia mwenyekiti wao mpaka wanachama na imeambukiza mpaka Selikari yote. Miezi 6 nyuma msimamo ulikuwa kujifukiza na mashine ya kujifukiza ikawekwa Mhumbili National Hospital na Waziri huyu Dorothy na manaibu wake wote walikataa chanjo.

Mtu pekee CCM mwenye credibility ya kusapoti chanjo kwa sasa ni Ndungulile maana alikataa bungeni na ikamgharimu uwaziri wake wakati huo
 
Mnaosema Gwajima ana msimamo siwaelewi

Huyu si alimkana Lowassa ilihali alizunguka naye nchi nzima

Hyu alidai hana shida na JPM ila ana chukia CCM leo hii mbona yupo CCM

Mwaka 2014 alidai katiba mpya hadi kumtukana Ask Pengo kwa kugoma kuendorse katiba. Leo hii mbona kaufyata kuhusu katiba mpya??

Alidai ubunge ni mdogo sana kwake leo hii ni mbunge

Hyu Mzee ni mpenda kiki tu lakini kuhusu msimamo hana otherwise asingekuwa CCM leo
 
Kungekuwa na mgombea binafsi hapo sawa .Alivyo bahiri hawezi kuendesha chama huyo.
 
Unafikiri huyu mtu wafuasi wake kanisani ndio wote wana msimamo mmoja wa kisiasa pia?

He will be suprised!
 
Back
Top Bottom